Sex ni afya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sex ni afya

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by mzambia, Mar 13, 2011.

 1. m

  mzambia JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  SEX NI AFYA
  Wengi huja na sababu lukuki linapokuja suala la kuwa mwili mmoja (kwenye ndoa) “mara kichwa kinauma” au “nimechoka sana leo” au “sijisikiii vizuri”lengo ni kukwepa SEX.

  Hata hivyo tafiti nyingi zinaonesha kuwa kuna faida kubwa sana kupata huduma ya tendo la ndoa angalau mara mbili au tatu kwa wiki, kumbuka too much is harmful

  FAIDA SEX KWA AFYA YA MWILI
  Huimarisha immune system kwenye mwili.
  Wanandoa ambao hushiriki angalau mara mbili kwa wiki walionesha kiwango kikubwa cha antibody zinazosaidia kupigana na magonjwa.

  Huongeza umri wa kuishi.
  Wanaume ambao walikuwa wanafika kileleni (orgasm) zaidi ya miaka 10 wali- boost uwezo wa kuishi miaka zaidi kuliko wale ambao walikuwa na hawafiki kileleni.

  Hupunguza uwezokano wa kupata prostate cancer.
  Wanaume ambao wali ejaculate zaidi ya miaka 35 walikuwa na asilimia 33 pungufu kupata prostate cancer.

  Hupunguza cholesterol (mafuta)
  Kutokana na zoezi la kufanya mapenzi (sex) ni zoezi tosha kuweza kupunguza cholesterol na kuondokana na kupata magonjwa ya moyo.

  Huimarisha mzunguko wa damu mwilini
  Tunapofanya mapenzi mapigo ya moyo huongezeka na mzunguko wa damu huwa na speed zaidi na damu huongezekana maradufu kwenye ubongo na sehemu zingine za mwili na matokeo ni mzunguko wa damu kuwa mzuri mwili mzima.

  Huongeza uwezo wa kukua (growth)
  Watafiti wengi wanakiri kwamba sex huongeza uwezekano wa mifupa kukua na kuimarisha repair ya tishu kwenye mwili.

  Huimarisha uwezo wa kunusa
  Baada ya sex, kuzalishwa kwa homoni ya prolactin huongezeka na huwezesha stem cells zilizopo kwenye ubongo kuzalisha neurons ambazo husaidia kunusa vizuri.

  Hupunguza maumivu (pain relief)
  Unapokaribia kufika kileleni kiwango cha homoni za oxytocin huongezeka mara tano zaidi kuliko kiwango cha kawaida, matokeo ni kutolewa kwa endorphins ambayo hupunguza maumivu ya kila kitu kuanzia kichwa, arthritis nk.

  Huimarisha kibofu cha mkojo
  Wakati wa sex unatumia muscles zile zile unatumia kukojoa (urine), kutumia mara kwa mara kwa hii misuli huwezesha kuwa na uwezo wa kuthibiti kibofu cha mkojo.

  Huimarisha uke
  Wanawake ambao huamua kutoshiriki sex wanakuwa na uwezekano wa kujisikia maumivu wakati wa SEX (vaginal atrophy) kwa kushiriki mara kwa mara uke huwa mwepesi kutoa lubricant na hakuna maumivu.
  Hapa kuna kanuni “use it or lose it!

  Husaidia healing ya vidonda
  Baadhi ya evidence zinapendekeza kwamba sex huweza kusaidia vidonda kupona haraka, ushahidi ni kwamba homoni za oxytocinhusaidia vidonda kupona kwa regeneration ya seli mwilini na oxytocinhuzalisha pale ukishiriki sex.

  Hupunguza uwezekano wa kupata cancer ya matiti.
  Wanawake ambao hawajawahi kuzaa walionekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata cancer ya matiti, hii ina maana kwamba kujihusisha na sex hupunguza kupata cancer ya matiti.

  FAIDA YA SEX KWA AFYA YA AKILI

  Hupunguza stress
  Sex huweza kupunguza stress kwa kupunguza kiwango cha masumbuko (anxiety) na kuongeza relaxation na kusaidia kuwa na usingizi mzuri.

  Hupambana na depression
  Wanawake ambao walijihusisha na sex kwa kuwa contact na semen walikuwa less depressed kuliko wale wambao hawakufanya.

  Hupambana na kuthibiti alama za kuzeeka
  Sex hufanya mtu kuonekana kijana zaidi.
  Katika utafiti mmoja watu ambao walishiriki sex zaidi ya mara 3 kwa wiki walionekana ni vijana zaidi ya miaka 10 pungufu ukilinganisha na wale ambao walikwepa sex.

  Huimairsha kujisikia upo fit
  Dakika 30 za kufanya mapenzi huweza kuchoma kiasi cha 150 calories.
  Na mtu anayeshiriki sex kila mara 3 kwa wiki huweza kupunguza kilo 2.5 za uzito kwa mwaka. Pia sex huweza kunyumbua misuli na kupelekea mtu kuwa fit, pia hekaheka za milalo mbalimbali huweza kufanya contractions ya mapaja, mikono, mabega, shingo, tumbo, kifua, mgongo, ******, miguu, kiuno na pia sex huzalisha testosterone ambayo huimarisha mifupa na misuli.

  Husaidia nywele kung’aa na ngozi kuwa imara
  Sex huongeza kiwango cha estrogen ambayo husaidia nywele kung’aa na ngozi kuwa imara kwa mwanamke.

  Husaidia meno kuwa imara
  Mara nyingi kabla ya sex wahusika hujitahidi kusafisha meno (brushing) kwa njia hii una kuwa imeimarisha afya ya kinywa.
  Pia wakati wa sex hasa maandalizi huhusisha kissing ambayo hufanya kazi nzuri kusafisha meno na fizi.
  Seminal plasma zinazozalishwa huwa na zinc, calcium na madini mengine muhimu kwa afya ya meno.


  FAIDA YA SEX KWA AFYA YA UZAZI
  Husaidia kuwa na mzunguko mzuri za siku za mwanamke.
  Wanawake ambao hujihusisha na sex angalau siku moja kwa wiki huwa na mzunguko wa siku uliosawa tofauti na wale ambao hutoa visingizio.

  Huimarisha fertility
  Kwa kuwa kushiriki sex hufanya mzunguko kuwa regular inakuwa rahisi mwanamke kushika mimba na kuzaa tofauti na mwanamke akiwa na mzunguko wa siku ambao ni irregular.

  FAIDA KATIKA KIROHO
  Watafiti wengi wanakiri kwamba kuna sexual energy kama energyzingine ambayo wakati wa sex ikiunganishwa kati ya mwanaume na mwanamke hasa wakati wa kufika kileleni huweza kuwaunganisha wawili in deepest part of of selves.
  Na hii energy (non physical) huweza kuimarisha maeneo mengine ya maisha yetu, hutufanya kujisikia ni kitu kimoja na kuwa strongerzaidi katika nafsi na mahusiano kwa ujumla.
  Hivyo matokeo ni kujisikia vizuri wewe mwenyewe, mwenzi wako na maisha kwa ujumla.

  TAHADHARI:
  Hii mada ni kwa ajili ya kupeana habari tu (ndiyo maana hakunareference links, ingawa unaweza mwenyewe ku- Google),
  Jambo la msingi ni kwamba kuna umuhimu wa hali ya juu sana kuzingatia kwamba hapa tunazungumzia sex katika ndoa tu na si zaidi ya hapo.
  Pia ni muhimu kuzingatia kwamba ili kushiriki sex ni muhimu kuangalia afya ya mwenzi wako, maadili na kutii sheria na amri za Mungu otherwise badala ya sex kukupa afya inaweza kukuua kimwili na kiroho.

  FANYA SEX UONGEZE UPENDO DAIMA
   
 2. DAUDI GEMBE

  DAUDI GEMBE Member

  #2
  Mar 13, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  FANYA SEX UONGEZE UPENDO DAIMA
  ya kweli hayaaaaaa
   
 3. m

  mzambia JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  We nyimwa unyumba wiki nzima ka upendo utakuwepo.
   
 4. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2011
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,819
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  yote mazuri ya mada yanaharibiwa na kipengele hicho cha "TAHADHARI" wengine hatujakidhi hicho kipengele cha "NDOA" sasa ndio tukose "AFYA"?
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,337
  Likes Received: 19,507
  Trophy Points: 280
  ngoja niiprint nikawasambazie watoto wa secondari/shule za kata muone kazi yake
   
 6. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Duh! umenigusa sana
   
 7. m

  mzambia JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Hapana usiiprint no kwa ajili ya wakubwa tu
   
 8. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #8
  Mar 13, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Huwa sina kawaida ya kusoma thread ndefu ila hii nimeisoma yote imetulia sana mkuu big up.
   
 9. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  kweli eh basi inapendeza sana Gaga
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  Mar 13, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hii imetulia..
   
 11. LD

  LD JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wale ambao hatuna ndoa, tutakuwa hatuna afya mpaka tupate ndoa au?
  Hebu tusaidieni na sisi tupate hiyo afya, kama tunafanya kwa afya kwani kuna dhambi hapo?
  Nauliza tu jamani. Sex kwa afya hata na mume wa mtu?? Si kwa afya?
  Kwani vibaya kuupatia mwili afya?
   
 12. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #12
  Mar 13, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Safi sana mkuu!! hivi ndo vitu ambavyo jamii yetu baadhi yetu inabidi tuvipate kila wakati ili kujimaarisha katika masuala ya afya na ndoa.
   
 13. c

  chelenje JF-Expert Member

  #13
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii inanifaa
   
 14. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #14
  Mar 13, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  atanikoma,je?ni round ngapi tuzipige a day.
   
 15. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #15
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,353
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Piga round kumi na nane(18) mzee!! maumivu kwisaa kabisa na UPENDO juuuu kaka!!
  Raha iliyoje mkuu!!
   
 16. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #16
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Vp mastabeshen??inaleta yote haya??coz wengine hatujaanza sex tunasubiri ndoa na umri unazidi kwenda
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Mar 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,075
  Trophy Points: 280
 18. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #18
  Mar 13, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi ipo kama Sex ni Afya basi hata asiye na mke au mume anafanya kwa afya.
   
 19. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #19
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuna ka ukweli aisee
   
 20. M

  Mutambukamalogo JF-Expert Member

  #20
  Mar 13, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hilo nalo neno.......
   
Loading...