Haya wadau baada ya kutoka wenye database mdudu server anahamia kwenye WEBSERVER
Wikipedia wanasema
webserver ni either hardware au software. Lakini Kama nilivyobainisha kwenye comment za mwanzo nitalezea zaidi software sababau naamin software ndio inayofanywa server kufanya kazi fulani na server hiyo kupewa jina fulani.
Kazi kubwa ya webserver ku kuwasiliisha kurasa ambazo mtumiaji(client) kaomba kupitia kwenye browser yake. Katika webserver kurasa hizi zinakuwa zimehfahiwa katika mfumo amabao sio wa kirafiki binadamu kuuulewa ( PHP, ASP. NET etc ) Nitakupa mifano baadae tuendeleee
Webserver kwa lugha nyepesi zinafanya kazi kwa mfumo wa client- server archtecture kama zilivyo server nyingine . Client computer ina omba (request )ukurasa fulani na server ina hudumia(serve) maombi ya mteja yaani client kwa kurudishas ule ukurasa au kutoa error msesage kama ukurasa haupatikani.
Kupunguza longolongo Tutumie mfano hai kuelezea nini kinatokea. . Hapa tuta assume kuwa mtumiaji ameunganishwa na internet. Maana bila net web seva ni bila bila .,,,,,,,,,,,
- Mtumiaji katika browser yake( ( IE, frefox,chrome,safri etc) anatype website au tovuti anayotaka kutembelea eg jamiiforums.com
- Browser inaanzisha mawasiliano kwa kutumia protocol ya HTTP kwenda kwenye websever uliyoomba. Sisi binadamu ni rahisi kujua tovuti kwa majina lakini mashine na server urahisi wa kutambua jamiiforums.com au yahoo.com ni nini ni kwa utumia IP adress. kwa hiyo kuna vitu vinafanyika nyuma ya pazia ile jamiiforums.com uliyonadika inabadilishwa kuwa IP adress kutumia DNS( Hili nalo ni somo na topic kamili na ndefu......) Kama una kiu ya kujua zaidi jinsi inavyofanya kazi basi chimba chimba zaidi kuhusu DNS
Kifupi kazi ya DNS ni kutafsiri jina kuwa IP adress na IP adress kuwa jina. Bila DNS tungetakiwa kukariri website zote kwa IP adress zake
Ebu tu run vi command hivi kwenye command prompt type maneno haya
tracert jamiiforums.com. kama picha invyoonyesha chini.
Kisha gonga enter. utakachoona baada ya hapo ni maelezo ya kiteniki kukuambia hatua au vituo au DNS maombi yako yanapitia mpaka kufika kwenye webserver husika uliyoomba ukihudumie ukurasa fulani . Kwa maelezo zaidi kuelewa hii kitu soma
Jinsi ya kutrace route traffic inapopita kutoka kwenye compuer mpaka kwenye webserver
So kwa msaada wa IP, HTTP, ISP na DNS server mbali mbli zilizoena dunia nzima, kitendo cha kuomba ukurasa na ukurasa kutokea kwenye screen kinaonekana ni cha haraka hata kama webserver na ukurassa huo uko marekani, . sabbau ya teknolijia nyingine mbali mbali kama
proxy,
caching, na hata
DNS yenyewe nzido zinarahisha mambo
So websever ya jamiiforum iliyopo USA ikipata maombi (request) kuwa IP adress ya mtazamaji katika port fulani anaomba ukurasa katika hii seva nini kinatokea ?
Kwenye webserver kuna mafile ya
Php, au
ASP. Hizi scripting language zina maelezo na ufafauzi jinsi gani kila ukurasa unatakiwa kuonyeshwa. Kama uliomba ukurasa wa dini kwenye jf kutakuwa na script itayokurudishia ujumbe kuwa inabidi uwe umesajiliwa na kuomba kuona ukurasa huu. kama ilibofya ukurasa wa jukwaa la teknolojia basi utapelekwa ukurasa huo moja kwa moja hata kama hujasajili
Sasa tutumie mfano hai kuona tofauti ya ukurasa anaoona mtumiji unavyokuwa na jinsi uanavyokuwa umehifadhiwa kwenye webserver .
Hii ni sura ya tovuti anayooona mtembalaji upande wa client.
Home page ya Tovuti hii ya ni ya wordprpes. Upande wa client unaonekana ni ukurasa moja lakini kwenye web server ukurasa huu umeundwa na php files nne ambazo ni
Home.php.,
sidebar.php.
footer.php na
header.php
cheki mfano wa PHP file unavyokuwa ukiwa kwenye server side. --- Ukiona kizungu zungu ruka au uliza teh teh teh
PHP:
<?php get_header(); ?>
<div id="main-content">
<p id="intro">Tovuti-blogu Hii itajaribu kuwa inatoa habari za fursa na chngamoto mbali mbali na jisni Teknolojia ya Habari na mawasilino(ICT) ina nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko edelevu .Iwe na kwa mtu mmoja, taasisi, mashirka au kampuni.Michango maoni na Mapendekezo vitakaribishwa </p>
<blockquote id="main-quote">Tutapiga Hatua tukiwa na Taarifa sahihi,wakati sahihi. <cite>- Mtazamani, </cite></blockquote>
<h2>Tochi ya Mtazamaji</h2>
<ul id="featured-widgets">
<li>
<h3>TBC</h3>
<p>Wiki hii Namulika chombo hiki cha Utangazaji cha Umma. Mapungufu ya Ki ICT nitakayonegela yanagusa vyombo vingi lakini msisitizo wangu unabaki hapa sababu TBC ni mali ya umma.Mpungufu yaliyopo ni makubwa na yanatikiwa kufanyiwa kazi <!--more--> </p>
<div class="image-and-button">
<img src="product-images/tbcsmall.png" alt="Image of tbc worker at office" />
<a href="http://teknohama.x10.mx/tbc/" class="button">NIYAPI?</a>
</div>
</li>
<li>
<h3>Muziki</h3>
<p>Wasanii wetu na mameneja wao bado wanaweka msisitizo na nguvu zao za kusambaza kazi za wasanii kwa kuuza CD. Muelekeo kwa wenzetu walioendelea unaonyesha manunuuzi ya ya CD yanazidi kupungua sababu ya furana teknolojia mbali mbali zinazoibuka <!--more--></p>
<div class="image-and-button">
<img src="product-images/musicsmall.png" alt="Image of music note" />
<a href="http://teknohama.x10.mx/muziki/" class="button">Wafanyeje?</a>
</div>
</li>
</ul>
<br />
<h2>UJUMBE <em> wa </em> WIKI</h2>
<div class="coupon">
When all you have is a hammer, every problem looks like a nail. This is a common mistake that a lot of technical security practitioners make when dealing with security issues. Always focusing on technology- <a href="http://www.backtrack-linux.org/blog/">Backtrack </a>
</div>
</div> <!-- END main-content -->
<?php get_sidebar(); ?>
<?php get_footer(); ?>
Zaidi ya hizo file za php pia kuna kuna file lina a maagizo ukurasa uliimbwa utokeeee kwa
style gani .Yaani
font gani,
rangi gani
size gani urefu na upana wa screen ya tovuti. Malelezo hayo yamo kwenye file la
CSS linatwa style.css
So unapoomba kuutembelea tovuti yeyote ya worpdpress , webserver inarudisha taarifa za hayo mafile manne pamoja na CSS. Then browser yako tena ndio inazitafsiri hizo files na CCS na kuzi display vizuri bila longo longo.. Mfano huu wa wordpress hauna tofauti na tovuti nyingine unazotembelea.
Ukitaka kujua kabla browser yako haijatafsiri muonekano wa ukurasa ulirudishwa na webserver ukoje basi Kwenye file menu nenda kwenye
view alafu
page source kwa wale wanaotumia Mozilla .
Vile vile Kweye jamiforums na tovuti nyingine ukibofya kitu kama "reply "au "reply with quote" au "like" login kule kwenye server kuna php codes au file zinashughuliiaa hiyo request.
Mwisho webserver nyingi za kisasa ni
database driven . So leo hii ukitaka kujua mambo ya web ni vizuri pia ujue pia mambo ya Database. Thread zote za jf, comments zote, user wote inforamtion zao ziko kwenye database. Kwenye blogs articles zote cmments zote zinahifadhiwa kwenye databse japo mtumiaji wa domain kama blogdpot.com anaweza aswie na acess ya moja kwa moja kwenye websever na database ya blog yake
Apache ndio webserver inayotumiwa kwa kias kikubwa sana iikifuatiwa na
IISya microsoft. Wanaotumia APache kama websever kwenye databse mara nyingi wanatumia Mysql na watumia IIS kwenye dataabse wanatumia MSqlserver
Wapi unaweza kupata websever za kufanyia mazoezi wa vitendo?
- kwenye laptop au computer unaweza kuinstall Visual Studio kama unataka kuanza na micrsoft au unaweza kusimika WAMP au XAMP. Kwa kusimika moja kati ya hizo utaifanya mashine yako kuwa na mazingira ya websever na datbase server na hapo hapo itakuwa client pia.
- Njia nyingine kama una network nzuri na unlimted kutumia ni free webserver . Binafis ndi natumia kufanya mazoezi. Japo zip nyingi sana changuo langu ni X10Hosting. Kuweka file kwenye websever kama hii utahitaji FTP client program kama fileziila. Hii ni njia nzuri ya kupata feeling halisi jinsi real life webserver zinavyofanya kazi............
kwa maeneo mengine ya watalaam tembelea
HOW WEBSERVER WORK
kama kawa nawachilicha kwa michango kukosoa, kuongeza na kuuliza ......