Server ni mdudu gani

Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,937
1,437
Wadau google is my best friend so msishangee naleta maswali haya ambayo wengi wana majibu lakini kuna baadhi tuna mtazamo usio sahihi kuhusu neno Server. So usishanage mwisho wa thread hii tukaijikuta tulikuwa una jibu sahihi lakini lisilo kamili.

enhee mswali ni yapi chacha

  • Server ni ni nini?
  • Maximum na minimum specification ya server inatakiwa kuwaje?
  • Unaweza kutambura server kwa umbo?
  • Kuna aina ngapi za server?

Nawachilicha.
 
Dah! Nadhani hapa nitafunguka zaidi mie napenda kumjua huyo mdudu kwa undani.
 
Tukisoma kwa makini maana ya seerver hapa na hapa basi nadhani wengi tutakubalina na kuwa server ni software na sio hardware. Kwamba kinachofanya mashine kuwa sever ni software na kazi inayofanya.

Kwa hiyo ukiweka Mysqlserver au SqLserver express edition au Orace hata kwenye laptop au dekstop tayari inakuwa databaseserver. Sio mara zote kutambua server lazima iwe au umbo au sura kama ya picha niliyoweka. hapo chini

Ukiiisntall WAMP kwenye estop tayari dekstop na latop inakuwa ni Database(Mysql) na na hapo hapo webserver(Apache). Kwa widows pia kuna database(SQLserver) na na webser(IIS) ambazo zinaweza kuwa installed kwenye laptop au desktop ya kawaida.

Aina za server znatofautina na majukumu. kama
  • Streaming server- Server inayowezesha kupublish video na Audi oatika kiwango kizuri . Tovuti kama Jusiti tv na Usteam Tv youtube na mashirika makubwa ya utangzaji kama aljazeera ba BBC zaidi iya kuwa na webserver na hata database server zitakuwa pia na streaming server zinazoweesha kupiblish matangazo yao online live
  • Aina nyingine za server waweza kuzisoma Server Types - Webopedia.com
Kwa hiyo nini mchango wa hardware kwenye sever?

Mchango wa hawrdware maalum ni kuongeza utendaji(performance) na Usalama (Security) katika level ya hardware. Mfano Server tunazoona kubwa nyingine zina Hard disk za OS mbili , moja iki fail nyingine inatumika bila server kuzima wala mtumiaji kujua kitu ambacho kwenye laptop na pc sio rahisi. Kwenye database server tunazoona kubwa kwa umbo zina usalama sababu zinatumia RAID katika level ya hardware lakini kwenye laptop au desktop njia rahisi ya RAID ni kwenye OS tu.

Kwa hiyo server sio lazima iwe hivi
220px-Rack001.jpg


Kwenye computer neno sever limetoholewa kutoka kwenye service na ni Kwa hiyo ni fucntion(s) zinazofanya na hardware ndio za kuamaua kama ni server au ni client na sio umbo au sura au brand.

Mtazamaji amewai kuandika kuhusu sever siku za nyuma na unaweza kusoma makala nyingine inayhusu server kwenye Gym yake ya mazoezi ya ICT

Nawasilisha kwa nyongeza, ukosoaji , kuponda na kupenda
 
hii bonge la shule. ngoja niipitie kwanza nitakupa matokeo ya nini nilichoelewa.
 
Sasa nitajitahid kwa kiswahili na msaada wa madesa ya google, bing na wikipedia nikichanganya na za kwangu kufafanua aina na majukumu ya server chache moja baada ya nyingine. Pale itakapobidi nitatoa viunganisho vya reference kwa watakapenda kuchimba na kuchimbua zaidi....... kama kawa .... kuponda , kukosoa na kupenda kukanarisbihwa nisije ni kawalisha watu kasa teh teh teh

enhee Tuendeleeeee
Teknoljia ya ICT ilipofikia sasa program zinateganiswha na data. na data zinatengansihwa na kanuni za biasharaau ofisi( Business logic) Kwa kitaalma kuna makundi yainaitwa N -archtecture .

kitu hiki ni cha muhimu kwa mtu yeyote anatengeza application kisasa. Na kwenye taasisis nyingi Mifumo yao mingi ya computer sana sana iko katika Two tier au three tier archtecture. Muundo huu inasaidia sana.

Layer tatu kuu zinazotumika kudesign application ni PRESENTATION, LOGIC au kwa jina lingine BUSINESS Logic na DATA. Kama uko kwenye ofisi iliyo na server na wewe sometime unashidnwa kufanya kazi zao za kiofisi server ikiwa na matatizo basi ofisi au shirika lenu linatumia moja wapo ya archetucture hizi. kwa maelezzo zaidi unaweza kuanza kwa kusoma hapa na hapa bila kusahau daraja la maarifa google.

Machoro chini unaonyesha computer system archtecture mbili kuu zainanzotumika kwenye makampuni na mashirika mengi
3508f2.jpg 3508f3.inline.jpg
Two tier archtecture Threee Tier archtecture


Sasa ufafanuzi wa aina ya sevrer.
DATA base server- iwe ni shirika binafsi, serikali , CIA, Mosad , Dafatari la mpiga kura, Kitambulisho cha Taifa, ATM, facebook ni muhimu :-

  • kuhifadhi data ili ziwe salama , zisipotee, yaani security.
  • kuwe na copy moja ya data inayotumika ili kusiwe na haja marekebisho kwa kila copy na kuondoa uttata na dublication . Jiulize ingekuwaje kama kila tawi la benki lingekuwa na kumbu kumbu zake kuhusu wateja????
  • Data Ziwe rahisi kupatikana na kutumika wa watu wengi wakati mmoja kwa kutumia network. Mfano mtu akichomoa fedha kwenye accout yake kwa utumia ATM na wakati huo huo kuna mtu kadeposit fedha wenye account hiyo hiyo akiwa tawi jingine lisitokee tatizo

Sasa umuhimu wa data ndio umesabaisha uwepo na database sevrer amabyo yenyewe kazi yake ni kuweka data tu. Sasa kutofatisha server nyingine na database sever ni kuwa database server kama MYSQL, SQLSERVER ORACLE , zina sifa ya kiteknini kama

kwa hiyo shirika au kampuni linaweza kuwa na aina nyingi ya server lakini seva ya muhimu na crtical ni ile yenye data ambayo ni database sever . Cables za ubaloz wa USA ziliibiwakutoka kweye database server sababu kuna mtu alipata acess right kwa njia halalai au zizoso halalai then akazichukua katika soft copy..............


nawasilisha
 
Mtazamaji LDAP nayo inahusika vp katika server?pia kuna kitu umegusia hapo juu.APPLICATION.pia naomba unijuze uzuri kama hizi server zipo za offline na online?
 
Mtazamaji LDAP nayo inahusika vp katika server?pia kuna kitu umegusia hapo juu.APPLICATION.pia naomba unijuze uzuri kama hizi server zipo za offline na online?

Mhhh LDAP mhhhh nukweli hili jibu niju nitalotoa ni desa 100% sabu hata kwenye kumbukumbu zangu imeshapotea na katika mazigira ya vitendo sijakutana nalo na kulissia mara kwa mara. ila nio umuhmu wa jukwaa kama hili maswali yansaidia kuelimisha pia.

LDAP ni protocol na prtotocol kwenye mambo ya data communication kazi yake kubwa ni kuwa na kanuni zinazowezesha server( Eg Web au Database au Application server ) na client ziwasiliane bila matatizo. Kwa lugha nyepesi unaweza kuiita LDAPP kama mkalimani kati ya server na clinet kwa mambo fulani fulani
.......As a protocol, LDAP does not define how programs work on either the client or server side. It defines the "language" used for client programs to talk to servers (and servers to servers, too).......

kwa kuwa ni mchovu kwa hii issue ya LDAP unaweza kusoma hapa . May be kuna wataalam wengine wanaiifahamau watafafanua zaidi wa lugha nyepesi na ya kueleweka zaidi.

Kuhusu online na offiine kwa server sijui kama nimekupata vizuri . Navyoelewa kuna taaisi amabazo zina kazi muhimu kiasi kwamba inabidi wawe na database server mbili. Moja inakuwa online na nyingine inakuwa haitumiki lakini inakuwa ina mirror au inachukua copy ya logs na transaction kutoka kwa ile ilyo online ( Kwa hiyo haiwi offline)

Kwa Microsoft SQL server kuna kitu kinaitwa Logshipping . So ikitokea ile database ya online ikapata tatizo kubwa then wataalam wanafanya switiching haraka ili ile standby database au secondary database au offline kama ulivyoita wewe server itumike sababu inakuwa ina data kama ile iliyokuwa online. Kama ni usumbufu unatokea usumbufu wa dakika chache tu

Kwa hiyo sababu ya umuhimu wa data ,database server ndio server zinalindwa sana kuanzia server zenyewe eg hard disk za kwenye database server kubwa zinalindwa kulindwa kwa kutumia RAID kama nilvyotoa link kule juu

Pia kuna backup ambapo data za kila databaase zinawekwa kwenye Tape ili hata ile stanbby sever ikigoma au kukitokea moto na kuunguza seever kuwe na kinzio. So ikilazma kufanya isnataalition mpya na unua sevrer mya basi zile ata za kwenye tape zinakuwa RESTORED na hivyo mali na vifaa vinakuwa vimepotea lakini data zipo......

Huu ni mfano wa tape amabzo ofisi na mashiria yanatumia kuchukua backup ya data kila siku. Chini ya hio tape ndio if Tape drive yenyewe

300px-Dds_tape_drive_01.jpg



Na swali lako la APPLICATION sijaelewa ulitaka kuelewa kuhusu nini hasa. kama hutajali rudia.
 
Kweli sikueleweka nilisoma haraka haraka pale kwenye mstari unaoelezea kuhusu atm na fb nimepitia post tena na kuona kumbe ni Dublication na si application ndio maana nikataka kuzua mjadala ili ni vune maujuzi mengi.
 
LDAP kwa lugha rahisi ni protocol inayokuwezesha ku login mara moja ktk multiple application. Yaani unwakuwa unaweza kutumia same credentials kulogin ktk apps zote zilizokuwa connected na Active directory. Mfano nina app X, Y na Z. Zote ziko connected ktk AD kwa kutumia LDAP. Then kwa domain username yangu na password nitaweza ku login ktk app yoyote. No password per app
 
mkuu mtazamaji muda wangu ni mdogo sana lakini natamani nisome hii na kuijua server,jioni leo nitafanya hii kazi,thank you for sharing brother
 
:brick:

Jamani nawapigia salute, lakini hamuwezi kuwa mnatumwagia mambo ni mpaka tuulizeeee eeeh,au ndio utaratibu.
I can now talk about servers!Asante muulizaji!
 
Haya wadau baada ya kutoka wenye database mdudu server anahamia kwenye WEBSERVER

Wikipedia wanasema webserver ni either hardware au software. Lakini Kama nilivyobainisha kwenye comment za mwanzo nitalezea zaidi software sababau naamin software ndio inayofanywa server kufanya kazi fulani na server hiyo kupewa jina fulani.

Kazi kubwa ya webserver ku kuwasiliisha kurasa ambazo mtumiaji(client) kaomba kupitia kwenye browser yake. Katika webserver kurasa hizi zinakuwa zimehfahiwa katika mfumo amabao sio wa kirafiki binadamu kuuulewa ( PHP, ASP. NET etc ) Nitakupa mifano baadae tuendeleee

webserver-basic-sm.gif


Webserver kwa lugha nyepesi zinafanya kazi kwa mfumo wa client- server archtecture kama zilivyo server nyingine . Client computer ina omba (request )ukurasa fulani na server ina hudumia(serve) maombi ya mteja yaani client kwa kurudishas ule ukurasa au kutoa error msesage kama ukurasa haupatikani.

Kupunguza longolongo Tutumie mfano hai kuelezea nini kinatokea. . Hapa tuta assume kuwa mtumiaji ameunganishwa na internet. Maana bila net web seva ni bila bila .,,,,,,,,,,,

  • Mtumiaji katika browser yake( ( IE, frefox,chrome,safri etc) anatype website au tovuti anayotaka kutembelea eg jamiiforums.com
  • Browser inaanzisha mawasiliano kwa kutumia protocol ya HTTP kwenda kwenye websever uliyoomba. Sisi binadamu ni rahisi kujua tovuti kwa majina lakini mashine na server urahisi wa kutambua jamiiforums.com au yahoo.com ni nini ni kwa utumia IP adress. kwa hiyo kuna vitu vinafanyika nyuma ya pazia ile jamiiforums.com uliyonadika inabadilishwa kuwa IP adress kutumia DNS( Hili nalo ni somo na topic kamili na ndefu......) Kama una kiu ya kujua zaidi jinsi inavyofanya kazi basi chimba chimba zaidi kuhusu DNS
Kifupi kazi ya DNS ni kutafsiri jina kuwa IP adress na IP adress kuwa jina. Bila DNS tungetakiwa kukariri website zote kwa IP adress zake

Ebu tu run vi command hivi kwenye command prompt type maneno haya tracert jamiiforums.com. kama picha invyoonyesha chini.
tracert.JPG
Kisha gonga enter. utakachoona baada ya hapo ni maelezo ya kiteniki kukuambia hatua au vituo au DNS maombi yako yanapitia mpaka kufika kwenye webserver husika uliyoomba ukihudumie ukurasa fulani . Kwa maelezo zaidi kuelewa hii kitu soma Jinsi ya kutrace route traffic inapopita kutoka kwenye compuer mpaka kwenye webserver

So kwa msaada wa IP, HTTP, ISP na DNS server mbali mbli zilizoena dunia nzima, kitendo cha kuomba ukurasa na ukurasa kutokea kwenye screen kinaonekana ni cha haraka hata kama webserver na ukurassa huo uko marekani, . sabbau ya teknolijia nyingine mbali mbali kama proxy, caching, na hata DNS yenyewe nzido zinarahisha mambo

So websever ya jamiiforum iliyopo USA ikipata maombi (request) kuwa IP adress ya mtazamaji katika port fulani anaomba ukurasa katika hii seva nini kinatokea ?

Kwenye webserver kuna mafile ya Php, au ASP. Hizi scripting language zina maelezo na ufafauzi jinsi gani kila ukurasa unatakiwa kuonyeshwa. Kama uliomba ukurasa wa dini kwenye jf kutakuwa na script itayokurudishia ujumbe kuwa inabidi uwe umesajiliwa na kuomba kuona ukurasa huu. kama ilibofya ukurasa wa jukwaa la teknolojia basi utapelekwa ukurasa huo moja kwa moja hata kama hujasajili

Sasa tutumie mfano hai kuona tofauti ya ukurasa anaoona mtumiji unavyokuwa na jinsi uanavyokuwa umehifadhiwa kwenye webserver . Hii ni sura ya tovuti anayooona mtembalaji upande wa client.

Home page ya Tovuti hii ya ni ya wordprpes. Upande wa client unaonekana ni ukurasa moja lakini kwenye web server ukurasa huu umeundwa na php files nne ambazo ni Home.php.,sidebar.php. footer.php na header.php

cheki mfano wa PHP file unavyokuwa ukiwa kwenye server side. --- Ukiona kizungu zungu ruka au uliza teh teh teh
PHP:
<?php get_header(); ?>
<div id="main-content">

            <p id="intro">Tovuti-blogu Hii itajaribu kuwa inatoa  habari za fursa na chngamoto mbali mbali na  jisni Teknolojia ya Habari na mawasilino(ICT) ina nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko edelevu .Iwe na kwa mtu mmoja, taasisi, mashirka au kampuni.Michango maoni na Mapendekezo vitakaribishwa </p>

            <blockquote id="main-quote">Tutapiga Hatua tukiwa na Taarifa sahihi,wakati sahihi. <cite>- Mtazamani, </cite></blockquote>

            <h2>Tochi ya Mtazamaji</h2>

            <ul id="featured-widgets">
                <li>
                    <h3>TBC</h3>
                    <p>Wiki hii Namulika  chombo hiki cha Utangazaji cha Umma. Mapungufu ya Ki ICT  nitakayonegela yanagusa vyombo vingi lakini msisitizo wangu unabaki hapa sababu TBC  ni mali ya umma.Mpungufu yaliyopo ni makubwa na yanatikiwa kufanyiwa kazi <!--more--> </p>
                    <div class="image-and-button">
                    
                        <img src="product-images/tbcsmall.png" alt="Image of tbc worker at office" />
                        <a href="http://teknohama.x10.mx/tbc/" class="button">NIYAPI?</a>
                    </div>
                </li>
                <li>
                    <h3>Muziki</h3>
                    <p>Wasanii wetu na mameneja wao  bado wanaweka msisitizo na nguvu zao za kusambaza kazi  za wasanii kwa   kuuza CD. Muelekeo  kwa wenzetu walioendelea unaonyesha manunuuzi ya ya CD yanazidi kupungua sababu ya furana teknolojia mbali mbali zinazoibuka <!--more--></p>
                    <div class="image-and-button">
                
                        <img src="product-images/musicsmall.png" alt="Image of music note" />
                        <a href="http://teknohama.x10.mx/muziki/" class="button">Wafanyeje?</a>
                    </div>
                </li>
            </ul>

            <br />

            <h2>UJUMBE <em> wa </em> WIKI</h2>

            <div class="coupon">
                When all you have is a hammer, every problem looks like a nail. This is a common mistake that a lot of technical security practitioners make when dealing with security issues. Always focusing on technology- <a href="http://www.backtrack-linux.org/blog/">Backtrack </a>
            </div>

        </div> <!-- END main-content -->

<?php get_sidebar(); ?>

<?php get_footer(); ?>
Zaidi ya hizo file za php pia kuna kuna file lina a maagizo ukurasa uliimbwa utokeeee kwa style gani .Yaani font gani, rangi gani size gani urefu na upana wa screen ya tovuti. Malelezo hayo yamo kwenye file la CSS linatwa style.css


So unapoomba kuutembelea tovuti yeyote ya worpdpress , webserver inarudisha taarifa za hayo mafile manne pamoja na CSS. Then browser yako tena ndio inazitafsiri hizo files na CCS na kuzi display vizuri bila longo longo.. Mfano huu wa wordpress hauna tofauti na tovuti nyingine unazotembelea.
Ukitaka kujua kabla browser yako haijatafsiri muonekano wa ukurasa ulirudishwa na webserver ukoje basi Kwenye file menu nenda kwenye view alafu page source kwa wale wanaotumia Mozilla .

Vile vile Kweye jamiforums na tovuti nyingine ukibofya kitu kama "reply "au "reply with quote" au "like" login kule kwenye server kuna php codes au file zinashughuliiaa hiyo request.

Mwisho webserver nyingi za kisasa ni database driven . So leo hii ukitaka kujua mambo ya web ni vizuri pia ujue pia mambo ya Database. Thread zote za jf, comments zote, user wote inforamtion zao ziko kwenye database. Kwenye blogs articles zote cmments zote zinahifadhiwa kwenye databse japo mtumiaji wa domain kama blogdpot.com anaweza aswie na acess ya moja kwa moja kwenye websever na database ya blog yake

Apache ndio webserver inayotumiwa kwa kias kikubwa sana iikifuatiwa na IISya microsoft. Wanaotumia APache kama websever kwenye databse mara nyingi wanatumia Mysql na watumia IIS kwenye dataabse wanatumia MSqlserver

Wapi unaweza kupata websever za kufanyia mazoezi wa vitendo?

  • kwenye laptop au computer unaweza kuinstall Visual Studio kama unataka kuanza na micrsoft au unaweza kusimika WAMP au XAMP. Kwa kusimika moja kati ya hizo utaifanya mashine yako kuwa na mazingira ya websever na datbase server na hapo hapo itakuwa client pia.
  • Njia nyingine kama una network nzuri na unlimted kutumia ni free webserver . Binafis ndi natumia kufanya mazoezi. Japo zip nyingi sana changuo langu ni X10Hosting. Kuweka file kwenye websever kama hii utahitaji FTP client program kama fileziila. Hii ni njia nzuri ya kupata feeling halisi jinsi real life webserver zinavyofanya kazi............
kwa maeneo mengine ya watalaam tembelea HOW WEBSERVER WORK

kama kawa nawachilicha kwa michango kukosoa, kuongeza na kuuliza ......
 

Attachments

  • tracert.PNG
    tracert.PNG
    2.6 KB · Views: 48
Mtazamaji utatupasua vichwa nimesoma hiyo mpaka jasho limenitoka hasa kwenye html code.
 
Mtazamaji utatupasua vichwa nimesoma hiyo mpaka jasho limenitoka hasa kwenye html code.

Pole sana mkuu hata kama umebamba kidogo sio mbaya. Otheriwise kama unapenda chukuaa free hosting na hawa jamaa. chagua domain name unayopenda then tutaendelea kwa vitendo siku nyingine.
  • Jinsi ya kuistalll, na kuchakachua CMS kama za worpdress, joomla na drupal
  • Tutaangalia mambo ya CSS
  • Bila kusahau mambo ya MySQL
 
Pole sana mkuu hata kama umebamba kidogo sio mbaya. Otheriwise kama unapenda chukuaa free hosting na <a href="http://x10hosting.com/" target="_blank">hawa jamaa</a>. chagua domain name unayopenda then tutaendelea kwa<b> vitendo</b> siku nyingine. <ul><li>Jinsi ya kuistalll, na kuchakachua CMS kama za worpdress, joomla na drupal</li><li>Tutaangalia mambo ya CSS</li><li>Bila kusahau mambo ya MySQL</li></ul>
ok unamaanisha ni create site kabisa?kama ni hivyo itakuwa poa sana coz naitengenza mpaka mwisho kwa maelekezo toka kwako ...pia naweka link hapa kila mtu aone hatu kwa hatua.
 
Back
Top Bottom