Nina Daktari wawili na wote walishaniambia PUMZIKA, ikabidi niwambie ukweli kuhusiana na majukumu niliyo nayo na uiumu wa kila jukumu. Wakanishauri (karibia kwa mawazo sawa) kuwa niwaambie waajiri wangu wanipe likizo... Ni mmoja alokubali kunipa likizo ya wiki mbili lakini wengine walilalamika sana huku wakitaja ongezeko la dau katika kazi zao kitu ambacho binafsi kwangu hakikuwa mtego tena! Ni mwezi Septemba mwaka jana hiyo.Mkuu wangu Invisible. Kwanza nakupa pole sana kwa hali hili. Inaonekana kabisa you are too much overloaded!!! You need to offload!!! Kabla sijasema mengi, nakuomba sana kabla ya kwenda kupumzika kmwone kwanza Physician wako na akufanyie vipimo fore most blood sugar level and presha ndipo aendelee na diagnosisi nyingine as per his/her suggestion. For sure atakushauri upumzike, upate usingizi wa kutosha bila bughuda. Ila katika kutekeleza hilo ni vema familia yako wafahamu hali yako na utapumzika wapi. Kuwa away from mawasiliano is ok but not with family members contact.
Also nikuulize ratiba yako ya kula ikoje???
Usikute unatumia nguvu nyingi sana na replacement ni ndogo.
Nashauri nenda kwa Physician sasa usisubiri majibu hapa kwa sasa hivi.
Na hivi ndivyo ninavyoambiwa na waajiri wangu... Nilitarajia unambie "Pumzika na iache JF kwa muda tukutane baada ya mwezi hivi"Please, we need you most here at our sacred Jamvi.
Very simple nenda muhimbili au hospitali yenye hadhi, cheki jamaa waombe wakulaze hapo kwa siku tatu, then kila kitu fresh! We used to call this medical rescue!!
Oh,Pole sana Invisible!
Kama binadamu unahitaji muda kupumzika baada ya shughuli zako za kila siku. Naamini mwili wako unachoka sana kwanza unafanya kazi nne bado hujaingia JF tena siyo kama member tu wa kawaida ila una majukumu makubwa na hii forum nionavyo.
Jitahidi upate muda wa kupumzika,unaweza ukachukua holiday kwa muda kutoka kazini.
Kitaalamu sijui ni tatizo gani ila naamini unafanya sana kazi either mentally or physically hivyo tafuta muda upumzike.
Unaweza hata kuanguka siku nyingine! Na hizo kazi nne hata kama ni masaa 3 kila moja kwa siku ila ni stressful kutokana na demand zake tofauti hata kama profession ni moja. Majukumu yamezidi na hupati muda wa kupumzisha mwili wako!
Pia zingatia ratiba nzuri ya chakula.
Na hivi ndivyo ninavyoambiwa na waajiri wangu... Nilitarajia unambie "Pumzika na iache JF kwa muda tukutane baada ya mwezi hivi"
Hahaha, huu ndo ugumu ninaokumbana nao mkuu Maane.
Am trying to be frank!
Mkuu,Halafu kufanyia kazi 4 companies na bado JF is hectic!!! Yaani mkuu wangu ni kuwa fedha haitoshi mpaka uamue kufanyia hizo consultancy makampuni hayo yote??? Chagua hapo mawili then uyaambie yakuongeze mshahara/fees as compensation for the other 2 forgone. Please do that Mkuu wangu.
Oh,
Asante mkuu BelindaJacob,
Nalilia kupumzika... Nahisi ndo suluhisho. Tatizo ni vipi nifanye? Baadae nahisi tatizo jingine labda ni la kisaikolojia na wala si uchovu.
Laba niseme zaidi:
Nina watoto 8 mpaka sasa (Nyumbani Tanzania) ambao hawana wazazi (yatima) na wengine wana wazazi lakini uwezo uko chini ninaowasomesha na sidhani kama inawezekana kupita dakika bila kuwawazia, hawa sidhani kama unaweza kunishauri kuwa niwabwage! Sintokusikiliza...
Hii hali inanitatiza SANA mpaka nafikia hatua ya kusema mbele zenu wakuu, kama kuna ambaye anaweza kunishauri kama kuna cha kunywa ama kula kunifanya nirejee kwenye form basi naomba sana anipe ushauri...
Hizo kampuni ninazozifanyia kazi ni kuwa nafanya kazi ya aina moja kwa wote isipokuwa kampuni tatu zimeridhia kuniacha nibaki kwa mwajiri wa mwanzo zenyewe zinatuma kazi zake kwa njia tofauti na wakti mwingine kuleta ofisini kwangu physically.
I see, ni mara ya kwanza naleta tatizo langu kwenu wakuu.
Nina matatizo ambayo nahitaji ushauri wa haraka au wa kina ikiwezekana,.
Najisikia uchovu wa hali ya juu... Najisikia kucha kila aina ya kazi... Natamani kupumzika japo siku tatu tu niweze kurejea katika hali yangu ya kawaida.
Ugumu:
Nahitaji kuzima simu, kuwa mbali na pc kuwa mbali na familia yangu kabisa na kukaa alone kwa muda huo.
Si rahisi kuwambia familia kuwa nawaacha kwa muda huo, nahisi watajisikia vibaya.
Si rahisi kukaa mbali na JF, nikifanya hivyo nafsi inakuwa inanisuta all the times.
Si rahisi kuwaacha kwenye mataa makampuni manne ambao wameniajiri na kazi zao kulala siku moja kwao wanaona kama ndo mwisho wa makampuni yao (ilhali kuna wataalam wengi lakini wananikomalia).
Sina hamu na pesa zao hata kama wanasema wanavunja mkataba nami kwani mwili hauwezi kuvumilia hali niliyo nayo kwa sasa... Yani niko tayari kuacha na kupumzika liwalo na liwe.
Mbaya zaidi:
Nikiwa naendesha gari natamani kutokanyaga hata mafuta wala breki kwani nahisi vinanichosha mwili tu, nikiwa mbele kwenye foleni ya magari najikuta nimekuwa mwingi wa mawazo hata taa zikiruhusu nisipopigiwa kelele na wenzangu kushtukia inakuwa tatizo.
Je, wakuu nifanye nini???
Yes my boy........asikuambie mtu sijui unywe asprini sijui umuone dokta mashoka hamna tiba hapo......tafuta katoto kadogodogo kazuriiiiii kaka na wala usiogope kuingia gharama za kwenda nako mahali kama ngurudoto, kakuchuechue misuli na kukunyoosha viungo.