Serikali za Tanzania na Uturuki kwa pamoja zatiliana saini mikataba 9, Magufuli aalikwa Uturuki

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Habari wanaJF,

Fuatilia kila kinachojiri katika ziara ya rais wa Uturuki nchini.



=====

Serikali za Tanzania na Uturuki kwa pamoja zatiliana saini mikataba 9 katika sekta za Usafiri wa anga, Elimu na Utafiti, Mashirika ya habari ya TBC na lile la Uturuki la TRT pia sekta za Viwanda vidogo na Utalii.

Aidha mikataba mingine ni ya Afya na miradi ya maendeleo pamoja na ushirikiano katika elimu ya diplomasia.



=====

Serikali ya Tanzania na Serikali ya Uturuki zimesaini mikataba tisa ya makubaliano ya kiuchumi inayolenga katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa maendeleo baina ya nchi hizo.

Mikataba hiyo inahusisha sekta za uchukuzi, mawasiliano, habari, elimu, utalii, utafiti, viwanda, afya na ulinzi.

Akizungumza mara baada ya kusaini kwa mikataba hiyo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alisema ujio wa Rais wa Uturuki na ujumbe wake ni kielelezo cha ukuaji wa mahusiano baina ya Tanzania na Uturuki katika nyanja ya biashara na kimaendeleo baina nchini hizo.

Rais Magufuli alisema katika mazungumzo yake aliyofanya na Rais Recep Erdogan kuhusu ujenzi wa Reli ya Standard Gauge nchini, alimjulisha kiongozi huyo kuwa miongoni mwa wakandarasi walioomba zabuni ya ujenzi wa reli hiyo kuwa ni kampuni kutoka Uturuki, hivyo endapo itashinda zabuni hiyo itasaidia kukuza uhusiano uliopo baina ya nchi hizi mbili.

Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa, Serikali ya Tanzania inatarajia kuomba mkopo kupitia Benki ya Exim ya Uturuki katika kujenga sehemu ya kipande cha ujenzi wa reli hiyo.

Rais magufuli alisema Tanzania inaendelea kunufaika na uwepo wa Shirika la Ndege la Uturuki kwa kufanya safari zake za moja wka moja kutoka nchini Uturuki, kwa kuwa utasaidia kuongezeka kwa idadi ya watalii nchini na hivyo kukuza uchumi wa nchi hizo.

Kwa upande wake Rais wa Uturuki, Recep Erdogan alisema kuwa uwepo wa mikataba hiyo baina ya Tanzania na Uturuki itasaidia kupata matokeo mazuri ya uhusiano pamoja na fursa mbalimbali za ushirikiano katika nyanja ya Kilimo, Utalii, Ulinzi, Reli ambazo zitawezesha kukuza uchumi wa mataifa hayo.

Rais Erdogan alisema kuwa Uturuki imelenga kukuza ushirikiano uliopo baina yake na Tanzania kupitia makongamano ya wafanyabiashara yenye malengo ya kukuza uchumi, kuongeza ajira pamoja na kukuza ujasiriamali baina ya Tanzania na Uturuki.

“Kiwango cha Biashara ya uwekezaji katika nchi ya Uturuki ni Dola za kimarekani 150 ambapo lengo letu ni kufika Dola za kimarekani 500” alisema Rais huyo.Aidha Rais Erdogan alisisitiza kuwa kufanya kazi kwa pamoja kutasaidia nchi hizi kusonga mbele na kufanikiwa katika nyanja mbalimbali.

Nae Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe alisema kuwa makubaliano ya mkataba baina ya Tanzania na Uturuki katika Sekta ya Utalii yatasaidia katika kutangaza vivutio vilivyopo nchini, kubadilishana wataalamu, kubadilishana taarifa na kuongeza idadi ya watalii nchini.

Prof. Magembe aliongeza kuwa makubaliano hayo yatakuza sekta ya utalii katika kuvutia uwekezaji wa katika maeneo ya hoteli, fukwe na mbuga za wanyama zilizopo nchini.
 
Nchi za Tanzania na Uturuki leo zimetiliana saini mikataba tisa ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo baada ya kuwasili kwa Rais wa Uturuki kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.

Akizungumza baada ya kutiliana saini mikataba hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amesema, ujio wa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan umejumuisha wafanyabiashara 150 na kwamba, mikataba iliyosainiwa itasaidia kukuza uchumi pamoja na mahusiano baina ya mataifa hayo mawili.

Rais Magufuli ameitaja baadhi ya mikataba iliyosainiwa kuwa ni ya sekta za afya, elimu, ulinzi, na viwanda ambapo amesema, amemuomba Rais Erdogan kuikopesha Tanzania kiasi cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge yenye urefu wa zaidi ya kilometa 400.

Rais Magufuli pia amesema Rais huyo wa Uturuki amekubali kuongeza nafasi za wanafunzi wanaokwenda kusoma nchini Uturuki kutoka idadi ya wanafunzi 48 iliyopo hivi sasa, na katika masuala ya ulinzi, amesema Uturuki imekubali kutoa mafunzo ya ulinzi kwa watanzania nchini Uturuki.

Hadi sasa kampuni 30 za Uturuki zimefanya uwekezaji nchini Tanzania wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 305.08 na zinatarajiwa kutengeneza ajira 2,959 na hadi kufikia Februari 2016 biashara kati ya nchi hizi mbili iliongezeka kutoka Dola za Marekani milioni 66 sawa na shilingi bilioni 145.2 mwaka 2009 na kuwa Dola za Kimarekani milioni 160 sawa na shilingi bilioni 352.
 
Habari wanaJF,

Fuatilia kila kinachojiri katika ziara ya rais wa Uturuki nchini.



=====
Serikali za Tanzania na Uturuki kwa pamoja zatiliana saini mikataba 9 katika sekta za Usafiri wa anga, Elimu na Utafiti, Mashirika ya habari ya TBC na lile la Uturuki la TRT pia sekta za Viwanda vidogo na Utalii.

Aidha mikataba mingine ni ya Afya na miradi ya maendeleo pamoja na ushirikiano katika elimu ya diplomasia.


Aisee
 
Huyu Raisi anaiwinda Feza tu
Rais wa Uturuki kaja ili lile dili la Reli lifanikiwe maana ni dili kubwa

Tujiulize swali kama watanzania
Hawa China, Uturuki mikataba hii wanayoiweka sahihi mbona haijawahi kuwa na la maana lolote
Kumbuka zile 17 za Rais wa China
 
Ni jambo jema kwa kusainiana mikataba ya maendeleo, itasaidia kuinua hata uchumi wa nchi yetu. hongera sana raisi wa uturuki na mwenyeji wake raisi john mgufuli, sisi tunataka maendeleo pamoja na mahusiano mazur baina ya hizi inchi mbili
 
Back
Top Bottom