jose mjasiriamali
JF-Expert Member
- Sep 17, 2014
- 1,772
- 1,614
Hahahahahaha, mkuu umenifurahisha.wengi ni walimu kwa sababu hakukuwa na namna (wengi sio wote), ila kama unaona mishe haziendi ukiwa mwl, piga chini. kuna mambo mengine ya kufanya badala ya kulalamika. suala la kuajiriwa sio issue. wewe unaweza kufanya makubwa kuliko unavyofikiri nje ya ualimu au unaweza ukaendelea kuchomekea mashati huku unapitwa kipato mbali na muuza chipsi
mbona kila kukicha ni walimu tu! ni kada nyingi sana wanamaisha magumu kuliko ata hao walimu.
Tena bora ata kuna walimu wanaoishi kwenye nyumba za shule kuliko uyu mtendaji wa mtaa wetu anaeridhika kwa kuitwa jina tu la Afisa mtendaji na wakati ata hana vigezo vya kuwa afisa.
ni kazi flani hivi unakuwa una mawazo ya kutoboa unashindwa yanaongezeka majukumu unaamua ku relax usubiri ustaafu.Hahahahahaha, mkuu umenifurahisha.
Alafu mikopo yenyewe midogo tu kisha wanakatwa na mabenki miaka hadi mitano,njaa ndoinazidi kuwa Kali kwao.Shida sana
Tuwape muda tuone mkuuKwakweli walimu ni watu wa ajabu sana,mwenzako anashushwa cheo ninyi wengine mnashangilia.
Cha ajabu zaidi viongozi wengi wakuu wa awamu hii ya 5 waliwahi kupitia kwenye ualimu lakini sijui watafanye kwa walimu wenzao walipo makazini kwa sasa? Je watajitahidi kuboresha masrahi ya hawa walimu wetu au business as usual?
Ni sahihi kabisa mkuu,siku hizi hakuna kabisa hali ya walimu kuheshimika na wananchiEnzi zile tunasoma,ukiulizwa unataka kuwa nani,kwa kujivuna kabisa unasema mwalimu,mwalimu alikuwa anaheshimika ila siku hizi kuwa mwalimu ni kama uko jehanamu vileee, heshima hakuna tena
Halafu siamini kama wanaopondea ualimu wote ni walimu...walimu wenyewe wanajua nini kipo ktk ualimu....waache mashabiki wabaki wamejikaririsha...Ualimu siachi, napenda from deep inside my heart....
Hayo mengine nawacheki
Kwani wewe hujui kuwa serkali zetu toka Uhuru zimekuwa zikiongozwa na ccm?Ungetuambia katika mambo yapi usitake kujumuisha masuala unataka kutuambia kila shida ya Waalimu ni kutokana na serikali ya CCM au?
Tuambie dharau katika nini hasa?