Serikali yetu Kuitwa "Sinister" na "Authoritarian": Je, ni kweli? Kama si kweli, Tusiukubali Uongo huu, Tuukanushe!

Serikali yetu Kuitwa "Sinister" na "Authoritarian": Je, ni kweli? Kama si kweli, Tusiukubali Uongo huu, Tuukanushe!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
57,103
Reaction score
128,723
Wanabodi,

Huu ni uzi wa swali kuhusu Serikali Yetu Kuitwa "Sinister" na "Authoritarian", Jee ni Kweli?. Kama Sii Kweli, inamaanisha ni uongo!, Tusikubali Uongo Huu!, Tuukanushe, maana uongo ukisemwa sana bila kukanushwa, mwisho wake hugeuka kuwa kweli!. Na uzalendo ni pamoja za kutokubali nchi yako isemwe vibaya kwa kuzushiwa uongo na media za nje, huku sisi wenyewe, tumenyamaza tuu!. Kunyamaza huku kutapelekea dunia kuamini yote yanayosemwa kuhusu Tanzania ni kweli.

Nakiri kupandisha uzi huu kutokana na bandiko la Mkuu Return Of Undertaker
Gazeti la Uingereza laimulika serikali ya Magufuli na kusema ...

Jarida la Africa Confidential toleo la 58, story number 20 lililochapishwa Oktoba 6, limesema hivi kuhusu Tanzania.
Vol 58 No 20
Published 6th October 2017
"Magufuli on the warpath
6TH OCTOBER 2017
An assassination attempt against an opposition leader raises suspicions about sinister government tactics
When 40 bullets were pumped into the car carrying Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) member of parliament Tundu Lissu outside his Dodoma home on 7 September, claims of the country's descent into authoritarianism suddenly became more credible".

Hawa jamaa wamesema serikali yetu ni "sinister" na pia inaendesha nchi kwa mtindo wa "authoritarianism"!. Haya sio maneno mazuri kwa serikali iliyoingia madarakani kwa ushindi halali katika sanduku la kura, kupitia uchaguzi ulioendeshwa na Tume huru ya Uchaguzi, hivyo uchaguzi ulikuwa ni huru na wa haki, hivyo matokeo ni halali, na nchi yetu inaendeshwa kwa kufuata misingi ya katiba, na kuheshimu utawala wa sheria.

Ikulu yetu, Waziri Mwakyembe na Idara yetu ya Habari, tusikalie kuyafungia tuu magazeti ya ndani kwa kutoa habari za kweli msiopendezwa nazo, huku tukikaa kimya wakati habari za uongo kuhusu nchi yetu zikienezwa na media za nje!, habari yoyote ambayo sii ya kweli, kuihusu Tanzania na rais wetu, ikitolewa, tusikae kimya, ikanushwe!, vinginevyo itaonekana ni kweli!.

Mbona Kikwete alipotuhumiwa kwa kitu kitu kidogo tuu, kuhongwa suti, Ikulu yetu ilikanusha, kwa nini hizi media za nje, zinaituhumu serikali yetu kwa mambo makubwa, na mabaya hivi, halafu serikali yetu imekaa kimya, imenyamaza?.

Hata kama serikali imenyamaza, lets say iko too bize na mambo muhimu zaidi kwa taifa, hivyo haina time na vituhuma hivi vya media za nje, jee wako wapi Watanzania walendo wa kweli wa kuitetea nchi yetu yetu inaposemwa vibaya?!.

Mimi naomba kujipambanua kuwa ni Mtanzania Mzalendo, na kwa mujibu wa fani yangu, kazi yangu na uwezo wangu ni kuandika tuu au kusema!, rais wetu alipotuhumiwa kuhongwa suti nilisema.
Tuhuma za Rais wetu kuhongwa suti: Marekani ituombe radhi ...

Hata kelele kuhusu udikikiteta wa Magufuli ziliposhika kasi nilisema
Udikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka ...

Magufuli aliposemwa vibaya na SABC, nilisema
Serikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu ...

Magufuli aliposemwa vibaya kuhusu Mimba za utotoni, pia nilisema
Je, Huku Sio Kudhalilishwa Kwa Rais Wetu na Media za Nje?. Jee ...

Na sasa hapa serikali yetu inaposemwa vibaya, nimeandika na kushauri tusikubali, tusikae kimya, tukanushe unless kama yanayosemwa kuihusu serikali yetu ni kweli!.

Mungu ibariki Tanzania.

Jumapili Njema.

Paskali.
 
Ni kweli kwani walifanya jaribio au walitamani Lissu awe RIP kwa kumwaga Risasi 40 wameishakamatwa??

Kila wale wanataka kumwombea wanawekqa mahabusu ni ajabu kweli kweli

Ni Polisi gani inapoitwa inafika kwenye tukio zaidi ya masaa mawili baada ya tukio??

Je,wale walinzi wa nyumba za Area D specifically flat anayokaa Lissu wameishahojiwa??

Imagine Lissu na Dereva wangekuwa RIP ina maana uchunguzi usingefanyima au wangeende Makaburini kuwafanyia mahojiano??

Hivi pale Rais anaposema wanaokosoa utendaji au vita ya uchumi wapotezwe na baada ya masaa machache action ya kupoteza Lissu inafanyika unataka tuamini kitu gani??

Hivi waliofanya wizi,wakaandika mikataba mibovu akina Kalemani mbona ndiyo wamepewa post kubwa zaidi au sababu ni wakunyumba??

Wale wa Escrow na Kivuko Kibovu cha Bilioni nane wameishapotezwa??

Ukifika mahali watawala wanafanya double standard na kutaka kuua wanaowakosoa ni bora tuandikwe tu

Waache tuandijwe tu tena hata hilo jina wametuonea huruma
 
politicians (1).jpg
HIVI TUKANUSHE KWA MANENO AU VITENDO NA NANI ANATAKIWA AKANUSHE! NGOJA NISUBIRI WATAALAMU WATUSHAURI.ANDIKO ZURI!!!
 
HIVI TUKANUSHE KWA MANENO AU VITENDO NA NANI ANATAKIWA AKANUSHE! NGOJA NISUBIRI WATAALAMU WATUSHAURI.ANDIKO ZURI!!!
Hata uingereza kuna magazeti Ya udaku Kama hilo. Huwezi poteza muda kujibu gazeti la udaku liwe la Ndani Ya nchi au nje Ya nchi Liwe la udaku la uingereza au somalia au popote
 
Wanabodi,

Huu ni uzi wa swali kuhusu Serikali Yetu Kuitwa "Sinister" na "Authoritarian", Jee ni Kweli?. Kama Sii Kweli, inamaanisha ni uongo!, Tusikubali Uongo Huu!, Tuukanushe, maana uongo ukisemwa sana bila kukanushwa, mwisho wake hugeuka kuwa kweli!. Na uzalendo ni pamoja za kutokubali nchi yako isemwe vibaya kwa kuzushiwa uongo na media za nje, huku sisi wenyewe, tumenyamaza tuu!. Kunyamaza huku kutapelekea dunia kuamini yote yanayosemwa kuhusu Tanzania ni kweli.

Nakiri kupandisha uzi huu kutokana na bandiko la Mkuu Return Of Undertaker
Gazeti la Uingereza laimulika serikali ya Magufuli na kusema ...

Jarida la Africa Confidential toleo la 58, story number 20 lililochapishwa Oktoba 6, limesema hivi kuhusu Tanzania.
Vol 58 No 20
Published 6th October 2017
"Magufuli on the warpath
6TH OCTOBER 2017
An assassination attempt against an opposition leader raises suspicions about sinister government tactics
When 40 bullets were pumped into the car carrying Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) member of parliament Tundu Lissu outside his Dodoma home on 7 September, claims of the country's descent into authoritarianism suddenly became more credible".
Je umeisoma article yote? Kama hukuisoma pole sana Pascal Mayalla!
 
Ni dikteta John Pombe Magufuli, huyu hakuna namna ila watanzania tukubali, tuvumilie na kuomba Mungu 2020 ifike salama! Tuombe sana ingawa tayari tumeshapata madhara makubwa juu ya huyu dikteta ila tuendelee kuomba tusitumbuke zaidi!

Tuombe kwa ajili ya usalama wetu huku tukijua fika kuwa tunaye kiongozi asiye na nia nzuri na Tanzania na watanzania!
 
Wanabodi,

Huu ni uzi wa swali kuhusu Serikali Yetu Kuitwa "Sinister" na "Authoritarian", Jee ni Kweli?. Kama Sii Kweli, inamaanisha ni uongo!, Tusikubali Uongo Huu!, Tuukanushe, maana uongo ukisemwa sana bila kukanushwa, mwisho wake hugeuka kuwa kweli!. Na uzalendo ni pamoja za kutokubali nchi yako isemwe vibaya kwa kuzushiwa uongo na media za nje, huku sisi wenyewe, tumenyamaza tuu!. Kunyamaza huku kutapelekea dunia kuamini yote yanayosemwa kuhusu Tanzania ni kweli.

Ikulu yetu, Waziri Mwakyembe na Idara yetu ya Habari, tusikalie kuyafungia tuu magazeti ya ndani kwa kutoa habari za kweli msiopendezwa nazo, huku tukikaa kimya wakati habari za uongo kuhusu nchi yetu zikienezwa na media za nje!, habari yoyote ambayo sii ya kweli, kuihusu Tanzania na rais wetu, ikitolewa, tusikae kimya, ikanushwe!, vinginevyo itaonekana ni kweli!.

Mbona Kikwete alipotuhumiwa kwa kitu kitu kidogo tuu, kuhongwa suti, Ikulu yetu ilikanusha, kwa nini hizi media za nje, zinaituhumu serikali yetu kwa mambo makubwa, na mabaya hivi, halafu serikali yetu imekaa kimya, imenyamaza?.

Hata kama serikali imenyamaza, lets say iko too bize na mambo muhimu zaidi kwa taifa, hivyo haina time na vituhuma hivi vya media za nje, jee wako wapi Watanzania walendo wa kweli wa kuitetea nchi yetu yetu inaposemwa vibaya?!
.

Mimi naomba kujipambanua kuwa ni Mtanzania Mzalendo, na kwa mujibu wa fani yangu, kazi yangu na uwezo wangu ni kuandika tuu au kusema!, rais wetu alipotuhumiwa kuhongwa suti nilisema.

Paskali.
Mkuu Paschal, watu wanapoacha wajibu wao na kujiona wao ni wazalendo kuliko wananchi wenzao Uzalendo na mapenzi kwa nchi huondoka kwani kila mmoja huanza kupigania nafsi yake.
Hakuna asiyejua maana ya uzalendo baina ya wenye miaka 45+ kwani kulikuwa na chipukizi iliyojenga uzalendo mioyoni japokuwa wengine walikengeuka na kuwa mafisi wajiitao wazalendo huku wakihakikisha si nyama tu bali hata mifupa wanaiguguna kwa jina la uzalendo.

Ndio tunaweza kuandika sana kuitetea kwa mapenzi makubwa nchi yetu tuliyozaliwa, nchi iliyotulea na nchi tunayoipenda kuendelea kuiishi sisi na vizazi vyetu, nchi ambayo wazazi na wazazi wa wazazi wetu wamezaliwa na kuturithisha,kinachotisha ni kwamba tutakapoandika sisi na kutetea kama tunavyotetea maslahi ya nchi na mshikamano siku zote je ambao waliwajibika kujibu ili tuwaunge mkono watakubaliana nasi?

Je hatutaonekana kuwashwawashwa kwa kujitia vimbelembele? Je wakati tunajitahidi kutetea serikali yetu na Mheshimiwa Rais Je? wale "visababishi matukio" wanaosababisha tuchafuliwe watakuwa katika nafasi gani ili tusichafuliwe tena?

Kwa nia njema kabisa nimeandika mara kadhaa kwamba '' Mpendwa Rais wetu anapaswa kuwachunguza waliomzunguka yawezekana hawako safari moja na yeye, niliandika pamoja na nia yake njema ya kutuvusha wapo WAZALENDO waliokaribu nae wanamuangusha na kujitahidi kumtenganisha na wanaoonekana VIKWAZO katika miradi yao" Kukaa kimya kwa wanaohusika kujibu kunakhofisha watu wengine kujibu kwa maana haijulikani kwanini tuhuma zisizo na ukweli zikaliwe kimya!

Kimsingi inajulikana kwamba uzalendo upo mioyoni, kinachosikitisha wengi wetu wazalendo wa hisia.

Niishie hapa.
 
Hata uingereza kuna magazeti Ya udaku Kama hilo. Huwezi poteza muda kujibu gazeti la udaku liwe la Ndani Ya nchi au nje Ya nchi
HIVI MAGAZETI YA UDAKU YA TANZANIA YALIPOKUWA YANAANDIKA KUWA DIAMOND KAZAA NA HAMISA MOBETO ULIKUWA NI UONGO AU NI KWELI NA ALIYETUSAIDIA KUJUA UKWELI NI DIAMOND MWENYEWE KWA KUANZA KUKANUSHA NA BAADAYE KUKUBALI. BADO KICHWANI NETWORK YANGU HAIJASOMA VIZURI!! WATAALAMU TUSAIDIENI!!! UKWELI UKIANDIKWA NA MAGAZETI YA UDAKU UNAKUWAJE UWONGO NA NANI ATATUSAIDIA TUJUE UKWELI!
 
Tatizo kubwa na chuki ni watu kukosa kuingia ikulu ikiwa hapa nyumbani kuna watanzania halisi wanaweza kusema rais kapanga mpango wa kumuua fulani vyombo vya nje vimepata wapi habari kama si huyu alieweza kutamka hapa kwao dawa ni kuwapuuza kama wanavyopuuzwa hapa,hawazimi jua wala hawaleti mvua!
 
You over protect him than what you do to protect your creator and your family. Rais ni mwanasiasa na sijui mnatoa wapi dhana ya mwanasiasa asikosolewe. Maamuzi yake yana positive and negative effects to millions of people inside and outside the country sasa hao wanaokuwa affected either positively or negatively wakitoa positive comments mnashangilia ila wakitoa negative comments mnawaka.

I assure you there will be no single hour ambayo watu wooooote kwa 100% watamsifia Rais wenu...never so mnajitaabisha kwa kitu ambacho hakipo na hakitakuwepo. Kusifia na kukosoa are both feelings.....hutaki kukosolewa basi kataza kusifiwa pia.

Huyo JPM mmefanya kuwa zaidi ya Mungu. Mnakufuru. Hata kwenye biblia kuna mistari michache Mungu anakiri makosa/anajuta then who is JPM? Kuna mamilioni ya wanadamu wanamkosoa/wanamkufuru Mungu and yet He loves us all then who is JPM? Acheni kumuabudu JPM. Ameamua kuwa mwanasiasa, afanye siasa including kukosolewa/kusahihishwa.
 
Kwa kweli tumeonewa sana na hao mabepari uchwara, wanatuita madicteta bila hata aibu. Tutaendele kuwanyoosha kwa kupora miradi yao wasioilipia kodi. Mpaka watakapoelewa kuwa sisi ni: one man show true democratic state, chini ya Kabaka Yekka Political party.
 
Kwa kweli tumeonewa sana na hao mabepari uchwara, wanatuita madicteta bila hata aibu. Tutaendele kuwanyoosha kwa kupora miradi yao wasioilipia kodi. Mpaka watakapoelewa kuwa sisi ni: one man show true democratic state, chini ya Kabaka Mwene Political party.
Hahahaha.,,dah
 
Mleta uzi samahani sana naomba ukasome kwanza alafu urudi tena labda utaleta mabadiliko kidogo katika uzi wako...ukweli hauwezi kupingika hata kidogo je vitendo anavyofanya wewe huvioni??
 
Back
Top Bottom