Serikali yetu ilivyotelekeza ELIMU na kuwaachia secta binafsi.

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Ni jambo la kusikitisha sana ukitafakari mwenendo wa utoaji elimu kuanzia ya msingi mpaka Sekondari ya juu(A level) kwa hapa Tanzania. Kiukweli hali inasikitisha hasa kwa mtanzania wa hali ya chini. Kwa mfano; wakati zamani mtoto akichaguliwa shule ya serikali yeye pamoja na wazazi walifurahi kwani mtoto alionekana kuwa na uwezo mzuri wa kumudu masomo lakini sasa hivi mtoto hata kabla ya kufanya mtihani wa darasa la saba, mzazi anaanza kuhangaika kutafuta fom za shule mbalimbali za taasisi au watu binafsi! Sasa hapa ndipo wazazi na walezi wengi hutapeliwa na "kulankuliwa"kwani huchukua fom shule nyingi ambazo nyingine hufikia hadi Tsh25,000/ kwa form na mwisho wa siku unakuta shule husika inahitaji wanafunzi wachache tu lakini huuza form nyingi. Kwa mfano; mwaka huu shule ya Rosmin Tanga walihitaji wanafunzi si zaidi ya 90 kwa mujibu wa mazungumzo na mwalimu wa pale siku ya interview, lakini waliuza form zaidi ya ELUFU MOJA! Na zote ziliwekwa namba na muhuli wa shule na risiti zilikatwa. Swali kwa wataalam wa elimu na wahusika wa shule kama hizi; inawezekanaje kufanya mchujo kati ya watu zaidi ya 1,000 na kuchagua watu 90 tu kwa interview moja tu! Kweli hapa kigezo cha wastani kwa kila somo kinaweza kuzingatiwa vizuri!? Na mzazi haishíi hapo tu, atachukua form huku na kule. Hii yote ni kutokuwa na imani na shule za serikali! Ni kawaida sana wazazi wanapokutana siku hizi kuulizana mwanao "anasoma wapi"na mzazi mwenye mwanae shule za serikali anaonekana kama mtu ambaye hajali elimu ya mwanae achilia mbali kama ni hizi za kata. Imekuwa kama fashion wazazi kuhangaika na shule zenye majina makubwa ambazo nyingi(sio zote!) ziko kibiashara zaidi huku wakikazania watoto kujua kiingereza kana kwamba siku hizi Elimu ni kujua kiingereza. Ki ukweli haya ni matokeo ya Serikali kutelekeza shule zake na Elimu kwa ujumla. Shule nyingi za siku hizi hakuna kazi za mikono hata kufagia maeneo ya shule na madarasa kuna vibarua wameajiriwa! Mbaya zaidi serikali inaangalia tu.TUTAFIKA? Taifa lisilo na msingi mzuri wa Elimu haliendelei!
 
Back
Top Bottom