Serikali yazitaka taasisi binafsi zinazotoa elimu kuhusu Ukimwi kusitisha zoezi hilo

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeagiza taasisi na mashirika yote yasiyo ya kiserikali (NGO’s) yanayohusika na utoaji wa elimu ya Ukimwi kusitisha huduma hizo hadi itakapo toa muongozo mpya wa utoaji huduma katika ngazi ya jamii.

Waziri wa Wizara ya Afya, Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, alisema kumekuwepo na ongezeko kubwa la NGO’s ambazo zinasababisha muingiliano katika utoaji huduma za kijamii pamoja na kufanya kazi katika mikoa michache, ambapo amemuagiza Mganga Mkuu wa Serikali kuzipangia mikoa taasisi zinazotaka kufanya kazi.

“Serikali inaendelea kuzuia utolewaji wa huduma hizo kwa ngazi ya jamii hadi pale ambapo wizara itapitia mwongozo mpya wa utoaji huduma ngazi za kijamii kwa makundi maalumu. Shughuli za NGO’s kwenda kwa jamii kugawa vilainishi au kutoa elimu zitasimama hadi itakapotolewa mwongozo mpya wa utoaji huduma kwa jamii,” alisema.

Amesema wizara imeweka utaratibu mpya wa kusajili taasisi hizo na kwamba kabla ya kuanza kufanya kazi zinatakiwa kutoa taarifa kwa mkurugenzi wa halmashauri anayotaka kufanyia kazi.

“Kumekuwepo na ongezeko kubwa la idadi ya wadau wanaohitaji kusaidia serikali, ili kuleta huduma hizo kwa ngazi ya jamii, na kwamba ili kuleta tija, uwajibikaji na uwazi katika utolewaji wa huduma hizo, mganga mkuu wa serikali atawapanga wadau katika mikoa kulingana na idadi yao,” alisema.

Amesema NGO’s hizo zinatakiwa kutambuliwa na halmashauri husika kabla ya kuanza kazi.

“Mkurugenzi wa halmashauri atatambulisha wadau au NGOs na kutia kibali, tunazuia asasi hizi kutoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam kufanya kazi pasipo kuthibitishwa na wamurugenzi wa halmashauri,” alisema.

Kutasainiwa makubaliano ya kufanya kazi kusudi muweke makubaliano ya namna ya ufanyaji kazi. Lengo letu kumsaidia waziri wa katiba na sheria, hatutaki watu kuitumia wizara ya afya kukiuka sheria kwa kigezo cha kusaidia jamii.

Mkakati wa usambazaji vilaini hauruhusiwi kuendelea ili kuzuia ukimwi, kama wanataka waende dukani kunua

“Serikali itaendelea kutoa afua za ukimwi kwa kundi lolote lile katika kipindi hiki ambacho taasisi hizo hazifanyi kazi,” alisema.

Aidha, waziri Ummy amezitaka taasisi hizo pindi zitakapoanza kufanya kazi kutoa huduma kwa makundi maalumu yaliyo katika mazingira hatarishi ya kuambukizwa na kuambukiza ukimwi.

“Taasisi hizo zinatakiwa kutoa huduma na afua za ukimwi kwa makundi maalumu, serikali inapenda kusisitiza kwamba kwa mantiki ya Tanzania makundi yatakua kwa ujumla siyo tu wanaume wanaojihusisha na mapenzi na wanaume wenzao, watoa huduma wazingatie vijana na wasichana walio katika umri wa balehe, wafungwa, na makundi mengine,” alisema.

Amezitaka NGOs kuzingatia misingi ya sheria za nchi na ya mashirika yasiyo ya kiserikali.

“Kila mdau anayetoa huduma za afya asa za kupambana na ukimwi anatakiwa kuzingatia sheria za nchi hasa sheria ya kanuni ya adhavu sura 16 ya sheria ya Tanzania ambayo Inakataza vitendo vya mapenzi ya jinsia moja zinazokataza mapenzi ya jinsia moja,” amesema.


Chanzo: Dewji Blog
 
NGOs briefcase!huu wimbo wa kuisoma namba naamini ndani ya miaka mitano LIZABONI nae lazima atauimba,hali jinsi inavyokwenda hatutakiwi kuchekana maana wote tuko kwenye mzunguko wa system ya uchumi ambayo inafanyiwa MABORESHO

NB;
Kuna mzee mmoja uswahili alikua anacheka wenzake lakini sasa hivi yuko kimya maana yeye amekamatwa kwenye uhakiki wa vyeti
 
NGOs briefcase!huu wimbo wa kuisoma namba naamini ndani ya miaka mitano LIZABONI nae lazima atauimba,hali jinsi inavyokwenda hatutakiwi kuchekana maana wote tuko kwenye mzunguko wa system ya uchumi ambayo inafanyiwa MABORESHO

NB;
Kuna mzee mmoja uswahili alikua anacheka wenzake lakini sasa hivi yuko kimya maana yeye amekamatwa kwenye uhakiki wa vyeti
 
Back
Top Bottom