Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli imeendelea kuonyesha kwa vitendo ni kwa namna gani imedhamiria kuboresha maisha ya Wananchi wake. Kupitia Benki kuu ya Tanzania (BOT) imepunguza Kiwango cha akiba kinacho paswa kuwekwa na benki za kibiashara katika benki hiyo kutoka asilimia 10 (10%) mpaka asilimia 8 (8%). Pia BOT imeshusha riba ya mikopo inayotoa kwa benki hizo za kibiashara kutoka asilimia 16 (16%) mpaka asilimia 11(11%).
Hatua hii imefanya mabenki mengi yanayo jiendesha kibiashara kupata nafasi nzuri ya kutoa mikopo kwa wateja wake. Jambo hili limeifanya Benki ya CRDB kupunguza riba yake kutoka asilimia 21(21%) mpaka kufikia asilimia 17 (17%) pamoja na kupunguzwa kwa riba, Benki ya CRDB imeongeza muda wa marejesho kutoka miezi 60(miaka 5) mpaka miezi 84(miaka 7).
#Tanzania_mpya
#Matokeo+
*Shilatu E.J*