Serikali yayafungulia makampuni zaidi ya 150 ya Uwakala wa Forodha yaliyokuwa yamefungiwa

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
49,681
39,008
Wanaukumbi.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali aende Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ili akague taarifa za mapato ambazo zilikuwa zikilipwa na mawakala wa forodha na bandari kupitia benki ya CRDB lakini hazionekani kwenye mifumo ya benki.

Ametoa agizo hilo leo jioni (Jumatatu, Machi 17, 2016) wakati akizungumza na mamia ya mawakala wa forodha na bandari waliohudhuria mkutano aliouitisha ili kusikiliza kero zinazowapata katika utendaji kazi wao.

Akizungumza na mawakala hao kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu alisema kuna dalili za kutupiana lawama baina TPA na CRDB kuhusu malipo yaliyikuwa yakifanyika benki halafu fedha hazionekana na wakala anaidaiwa kuwa hajalipia mzigo wakati alishaulipia.

"Kimsingi bado liko tatizo baina ya Mamlaka ya Bandari pamoja na Benki ya CRDB. Naona kila mmoja hapa anamkana mwenzake. Nitamtuma CAG ili akafanye ukaguzi wa kina ili tujue ni nani kati yao amehusika na upotevu wa fedha,” alisema huku akishangiliwa na mawakala hao.

Alimwagiza pia Kaimu Mkurugenzi wa Bandari, Eng. Aloyce Matei aandae dispatch zote walizotumia kupokelea malipo za kuanzia mwaka 2015 na ikibidi aandae za kuanzia mwaka 2014 ili CAG anapozopitia aweze kupata picha halisi.

Vilevile, Waziri Mkuu alimwagiza Eng. Matei kuhakikisha wananunua mashine ya photocopy ili iwekwe kwenye chumba cha kupokelea stakabadhi za malipo ya benki (bank pay in slip) ili mteja anapoleta nakala ya benki aweze kutolewa photocopy na kubakia na nakala ya malipo aliyofanya.

Waziri Mkuu alisema Serikali inatambua bandari ni eneo nyeti katika kuinua uchumi na mapato ya nchi lakini pia ni eneo muhimu katika kutengeneza ajira.

“Ninapenda niwahakikishie kuwa bado tutaendelea kukagua bandari hadi pawe safi. Hii bandari ni yenu na mtafanya kazi kama kawaida,” alisema.

Mapema, akizumgumza kwa niaba ya mawakala hao, Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha nchini (TAFFA), Bw. Stephen Ngatunga alieleza matatizo mbalimbali ambayo wao kama mawakala wa forodha wamekuwa wakikumbana nayo kuanzia ulipaji, utoaji wa mizigo na kuitaka Serikali iongeze nguvu katika kuikabilia sekta hiyo.

Alizikosoa baadhi ya sheria ambazo zinaruhusu wamiliki wa bandari kavu kumiliki pia makampuni ya uwakala wa forodha, sheria kadhaa zinazochangia kukwamisha utoaji wa mizigo bandarini, ukaguzi hafifu wa kwenye scanner na uwepo wa vituo vinane vya mizani kuanzia Dar es Salaam hadi Tunduma ambavyo vimegeuka kuwa kero kwa wasafirishaji wa mizigo kwenda nchi jirani.

Wakati huohuo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani amesema Serikali imeamua kuyafungulia makampuni zaidi ya 150 ambayo yalikuwa yamefungiwa kufanya kazi za uwakala wa forodha kutokana na madai ya kuhusishwa na ukwepaji wa kodi.

Hapa tumegundua kuwa wote siyo wasafi iwe ni mawakala, benki ama bandari. Mkurugenzi wa Bandari, kuanzia leo watu hawa waruhusiwe waanze kufanya biashara lakini nyaraka za nyuma zisiguswe hadi CAG atakapokamilisha uchunguzi wake,” alisema kuibua kelele za shangwe kwenye ukumbi huo.

Source: Ritz wa JF
 
Hii habari ya January mwaka huu...

Makontena zaidi ya 11, 000 yaliyotolewa Bandari Kavu (ICD’s) bila kulipiwa tozo ya Mamlaka ya Bandari (TPA), limechukua sura mpya baada ya Chama cha Mawakala wa Forodha (Taffa), kuwasilisha kwa Waziri ushahidi wa malipo waliyofanya kwa Bandari.Aidha, Taffa inataka kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi ili kupata ukweli wa sakata hilo.Wanachama wa Taffa walituhumiwa na TPA kwamba walipitisha makontena hayo bila kulipia tozo ya bandari, lakini wenyewe wamekuwa wakikanusha na kuwarushia lawama watumishi wa bandari na benki ya CRDB.Akizungumza na Nipashe jana, Katibu Mkuu wa (Taffa), Tony Swai alisema unahitajika umakini wa hali ya juu wakati wa kulishughulikia jambo hilo ili ukweli uweze kufahamika na wahusika kuchukuliwa hatua kali.Alisema wanachama wa chama hicho wameshawasilisha vielelezo vyao vyote kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kwa ajili ya kumsaidia kubaini ukweli.“Wanachama wetu walilipia tozo na nyaraka zote wanazo na wamepeleka kwa Waziri kama ushahidi, tumeomba iundwe tume maana ndiyo itabaini pumba ziko wapi na mchele uko wapi," alisema Swai. "Hatuwezi kusema kwamba wanachama wetu wote wako safi maana waswahili wanasema msafara wa mamba kenge nao wamo, lakini kwa hili ushahidi wa malipo yote tuliyofanya upo thabiti.”Alisisitiza kuwa tume hiyo ndiyo itakuwa na uwezo wa kubaini watu waliokula fedha zilizotokana kwa malipo ya tozo hiyo, na kwamba utaratibu wa sasa wa kila taasisi kufanya uchunguzi wake hautakuwa na manufaa yoyote.Alisema ni vyema na ikaundwa tume itakayoishirikisha wajumbe kutoka Taffa, Taasisi ya Usalama wa Taifa(TISS), Mamlaka ya Bandari (TPA), Benki ya CRDB na Polisi ili kuchunguza nani hasa walihusika na utolewaji wa kontena hizo bila kulipiwa tozo za bandari na kusababisha upotevu wa mamilioni ya fedha za umma.Katibu huyo alisema katika hali ya kawaida, wakala wa forodha hawezi kutoa kontena kwenye bandari kavu bila mmiliki wa bandari hiyo kuthibitisha malipo yaliyofanywa kwenye benki ya CRDB.“Mwenye ICD akishajiridhisha kwamba umelipa tozo ya TPA ndipo nayeye anakupa gharama za kuhifadhi mzigo wako kwenye bandari yake kisha unachukua mzigo wako," alisema Swai."Sasa cha kujiuliza waliruhusu vipi kontena (11,000) zitoke bila kulipiwa tozo za TPA? Nani wanahusika na walifanyaje fanyaje? "Tume huru pekee ndiyo itakuja na majibu ya mchezo wote huu.”
 
Huo ni muendelezo wa kukurupuka,walikurupuka tu
 
Naona na wewe umeanza kufuata nyayo za pasco ili kuwashawishi watawala wakufikirie kimtindo
 
karibu mkuu,where have been,these few days?
 
serikali kurupukaji ... watalipa pia fidia ya kuwafungia kimakosa
hata wasipo lipa,furaha yangu ni kuwa yameumbuka
pole sana utasubiri sana mpaka upandwe na mchwa ili kufidiwa
matusi yanini tena kada?kama mada imekuzidi kimo chuchumia,ukishindwa hilo,weka kisturi,usimamie hata ukucha,na ukishindwa hilo basi pita hivi
Maigizo tu, unafungia makampuni kesho unayafungua
naona mijitu ya hapa kazi tu yanaumbuka,ahahaha
 
Back
Top Bottom