Serikali yaweka malengo ya kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa 85% ifikapo mwaka 2030

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imejipanga kupunguza maambukizi mapya ya VVU hadi kufikia Asilimia 85 ifikapo mwaka 2030, ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwaka 2010.

Hayo yamesemwa na Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI (NACP) Drk. Beatrice Mutayoba wakati akiwasilisha taarifa ya Mpango huo kwa niaba ya Waziri wa Afya Dkt.Dorothy Gwajima mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Dawa za Kulevya, katika ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.

“Mikakati hii pia imeainisha malengo makuu ya matokeo makubwa (impact results) ya mwitikio wa UKIMWI ambayo ni kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa asilimia 85 ifikapo 2030 ikilinganishwa na hali ilivyokuwa mwaka 2010,” alisema Dkt. Beatrice Mutayoba.

Aliendelea kusema kuwa, mikakati hiyo imelenga kupunguza vifo vitokanavyo na UKIMWI kwa asilimia 80% ifikapo mwaka 2030, ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwaka 2010 na kutokomeza unyanyapaa ifikapo 2030.

Aidha, Dkt. Beatrice amesema kuwa, kwa mwaka 2020 Tanzania ilikadiriwa kuwa na watu takribani 1,700,000 wanaoishi na Virusi vya UKIMWI, huku akidai kuwa mpaka mwisho wa robo ya Oktoba - Desemba 2020, takribani watu wanaoishi na VVU (WAVIU) walikuwa milioni 1.4, sawa na asilimia 83 ya WAVIU wote walikuwa wanatambua hali zao za maambukizi.

Vilevile amesema kuwa, WAVIU milioni 1.36 sawa na asilimia 98 walikuwa kwenye tiba na matunzo ya dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI (ARV) na asilimia 92 ya waliokuwa kwenye tiba ya dawa hizo (ARV) walikuwa na kiwango cha chini cha Virusi vya UKIMWI (VVU) mwilini.

Hata hivyo, Dkt. Beatrice alibainisha kuwa, inakadiriwa kuwa watu 77,000 walipata maambukizi mapya ya VVU kwa mwaka 2019, huku kiwango hiki cha maambukizi mapya kikionekana kushuka kwa 19%, ikilinganishwa na lengo la kupunguza maambukizi mapya kwa asilimia 75% iliyotegemewa kutoka mwaka 2010.

Dkt. Beatrice alisisitiza kuwa, asilimia 28% ya maambukizi mapya yalikuwa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 24, huku asilimia 67% ya maambukizi katika kundi la vijana.
 
Lengo kubwa ni kukaa kimya bila kuwatangazia raia wake kuchukua tahadhari dhidi ya covid 19/21 ili wafe wapungue.
 
Mbona mbali sana tutakuwepo kweli si tutakuwa tumesombwa na hilo gonjwa
 
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imejipanga kupunguza maambukizi mapya ya VVU hadi kufikia Asilimia 85 ifikapo mwaka 2030, ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwaka 2010.
Agenda kuu kwa sasa ni breathing complication
 
Back
Top Bottom