Trust None
JF-Expert Member
- Feb 12, 2018
- 1,260
- 4,421
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa, amesema atazingatia maslahi ya watumishi wa umma ikiwamo nyongeza ya mishahara, malipo ya wastaafu na kupandiswa kwa madaraja kwa mujibu wa sheria.
Mchengerwa alisema hayo juzi jijini hapa alipokuwa akizungumza na watumishi wa wizara hiyo katika kikao kazi pamoja na kujitambulisha rasmi.
Alisema akiwa katika nafasi hiyo, moja ya vipaumbele vyake itakuwa kuhakikisha maslahi ya watumishi wa umma yanazingatiwa ili kuongoza ufanisi na kuleta tija katika maeneo mbalimbali.
Masuala kama nyongeza ya mishara, kupandishwa kwa madaraja ya watumishi, malipo ya wastafu, alsiema ni mambo ambayo yapo kwa mujibu wa sheria hivyo utekelezaji wake ni wa lazima na si hiari.
“Mtumishi kuongezwa mshahara, kupandishwa madara au kupandishwa vyeo haya yapo kwa mujibu wa sheria na si ombi wala huruma ya mwajiri wake, hivyo tutahakikisha tunatekeleza kwa mujibu wa sheria inavyoelekeza,” alisema Mchengerwa.
Pia alsiema alisema pamekuwapo na malalamiko ya watumishi wa umma juu ya kupandishwa madaraja kazini na wengi wao kukaimu nafasi kwa muda mrefu.
“Sheria inatutaka kupadisha madaraja mtumishi kwa muda fulani lakini wengi bado hawajapatiwa haki yao, hivyo tutahakikisha tunafanya kwa kuzingatia sheria,” alisema.
Waziri pia alipiga marufuku watumishi kukaimishwa nafasi moja kwa zaidi ya miezi sita kama ambavyo imekuwa mazoea katika utumishi wa umma katika maeneo mbalimbali.
“Sheria inakataza mtumishi kukaimishwa katika nafasi kwa miezi sita lakini leo hii kuna maeneo wako watu wamekaimu kwa zaidi ya miaka sita, hivyo kuanzia leo (juzi) ni marufuku mtu kukaimu zaidi ya miezi sita” alisisitiza Mchengerwa.
Pia alisema moja ya maeneo ambayo watayafanyia kazi pia ni pamoja na malalamiko ya malipo ya wastaafu kucheleweshwa na kuwapa wakati mgumu kumudu maisha yao na familia zao.
Alisema watumishi wengi ambao wamemaliza muda wao wa kulitumikia taifa na kustaafu kwa mujibu wa sheria, bado wamekuwa wakikumbana na kero ya kucheleweshewa malipo kinyume cha sheria.
“Haki hizi kwa mtumishi aliyefanya kazi kwa kuzingatia kanuni na maadili ya utumishi wa umma ni jambo la lazima na si la kuomba, hivyo ni lazima azipate kama sheria inavyoelekeza” alisema Mchengerwa.
Kadhalika alisema kuwa katika uongozi wake atahakikisha stahiki zote za mtumishi zinapatiknaa kwa wakati ili kuongeza morali kwa kujituma katika maeneo yao.
Vilevile, aliwataka wakuu wa wilaya wa mikoa ambao wamekuwa na tibia ya kutumia mamlaka yao vibaya kwa kuwaweka ndani watumishi, kuacha mara moja na kutumia busara.
“Serikali inazingatia sheria na utawala bora. Niwaombe viongozi wenzangu kutumia busara pale inapobidi kwani kumekuwapo na viongozi ambao wanafanya mambo ambayo yanakiuka hata katiba ya nchi. Viongozi wote wanatakiwa kufanya mambo kwa kuzingatia kanuni na sheria,” alisema Mchengerwa.
Chanzo: IPP Media