Fidel80
JF-Expert Member
- May 3, 2008
- 21,947
- 4,445
Elizabeth Suleyman
SERIKALI kupitia taasisi zake,imetumia zaidi ya Sh176 millioni, kugharimia salamu 217 za pongezi katika vyombo vya habari, utafiti wa shirika moja lisilokuwa la kiserikali umeonyesha.
Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo la Sikaka kwa vyombo vya habari, Salamu hizo zilichapishwa katika magazeti mbalimbali katika kipindi cha kati ya Novemba 8 hadi Desemba 9 mwaka jana, baada ya uchaguzi mkuu wa urais, wabunge na madiwani, uliofanyika Oktoba 31.
Taarifa hiyo ilisema matangazo mengi yalihusu salamu za pongezi kwa washindi wa kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yule wa Zanzibar.
Utafiti huo umesema kiasi cha Sh108.2 milioni zilitumika kugharimia salamu 132 za pongezi.Taarifa ilisema utafiti pia unaonyesha kuwa kiasi kingine cha Sh25.3 millioni, kilitumika kugharamia matangazo 32 yaliyompongeza rais na Waziri Mkuu.
Ilisema utafiti uliofanywa na Sikika, imeonyesha jinsi matangazo ya pongezi yalivyotumia fedha za walipa kodi hasa ikizingatiwa kuwa taasisi zilizotoa matangazo hayo, yanagharimiwa na serikali.
Kulingana na taarifa hiyo, Shirika la Maendeleo ya Taifa, ndilo linaloongoza kwa kulipia matangazo nane kwa gharama ya Sh10 milioni, ukifuatiwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) uliotumia Sh9.5 milioni, kugharimia matagazo 16.
Mfuko wa Pensheni wa PPF, ulitumia Sh8.3 milioni kugharimia matangazo 12. Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika Irene Kiria, alisema fedha hizo zingetumika katika kuboresha huduma za afya, hali katika sekta hiyo ingekuwa ya kuridhisha.
"Kiasi hiki cha fedha kingeweza kutumika katika miradi ya maendeleo katika afya na elimu. Sekta ya afya inakabiliwa na matatizo mengi kama ukosefu wa rasilimali watu, fedha na madawa," alisema Kiria.
Alisema shirika lake limekuwa katika mstari wa mbele, kuikumbusha serikali, kuhusu umuhimu wa kuondokana na matumizi yasiyo ya lazima.
Alisema kutuma matangazo ya pongezi kwa viongozi, ni moja ya mambo yasiyowasaidia walipa kodi.Taarifa hiyo iliwashauri wananchi kutofumbia macho pale wanapogundua kuwa fedha zao zinatumika vibaya.
Serikali yatumia Sh176 mil kugharimia pongezi