Serikali yatumia Milion 176 kupongeza ushindi wa JK na Dr. Shein!

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,813
11,126
Elizabeth Suleyman - Gazeti la Mwananchi

SERIKALI kupitia taasisi zake, imetumia zaidi ya Sh176 millioni, kugharimia salamu 217 za pongezi katika vyombo vya habari
, utafiti wa shirika moja lisilokuwa la kiserikali umeonyesha.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo la Sikaka kwa vyombo vya habari, Salamu hizo zilichapishwa katika magazeti mbalimbali katika kipindi cha kati ya Novemba 8 hadi Desemba 9 mwaka jana, baada ya uchaguzi mkuu wa urais, wabunge na madiwani, uliofanyika Oktoba 31.

Taarifa hiyo ilisema matangazo mengi yalihusu salamu za pongezi kwa washindi wa kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yule wa Zanzibar.

Utafiti huo umesema kiasi cha Sh108.2 milioni zilitumika kugharimia salamu 132 za pongezi.Taarifa ilisema utafiti pia unaonyesha kuwa kiasi kingine cha Sh25.3 millioni, kilitumika kugharamia matangazo 32 yaliyompongeza rais na Waziri Mkuu.

Ilisema utafiti uliofanywa na Sikika, imeonyesha jinsi matangazo ya pongezi yalivyotumia fedha za walipa kodi hasa ikizingatiwa kuwa taasisi zilizotoa matangazo hayo, yanagharimiwa na serikali
.

Kulingana na taarifa hiyo, Shirika la Maendeleo ya Taifa, ndilo linaloongoza kwa kulipia matangazo nane kwa gharama ya Sh10 milioni, ukifuatiwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) uliotumia Sh9.5 milioni, kugharimia matagazo 16.

Mfuko wa Pensheni wa PPF, ulitumia Sh8.3 milioni kugharimia matangazo 12. Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika Irene Kiria, alisema fedha hizo zingetumika katika kuboresha huduma za afya, hali katika sekta hiyo ingekuwa ya kuridhisha.

"Kiasi hiki cha fedha kingeweza kutumika katika miradi ya maendeleo katika afya na elimu. Sekta ya afya inakabiliwa na matatizo mengi kama ukosefu wa rasilimali watu, fedha na madawa," alisema Kiria.

Alisema shirika lake limekuwa katika mstari wa mbele, kuikumbusha serikali, kuhusu umuhimu wa kuondokana na matumizi yasiyo ya lazima
.

Alisema kutuma matangazo ya pongezi kwa viongozi, ni moja ya mambo yasiyowasaidia walipa kodi.Taarifa hiyo iliwashauri wananchi kutofumbia macho pale wanapogundua kuwa fedha zao zinatumika vibaya.
 
Sasa kuna kitu gani kibaya hapo, kupeana pongezi kwa mtu aliyeshinda ni utamaduni wetu watanzania.

Na mbali ya hapo hizo salam za pongezi zimeendana na kuongeza publicity ya hizo taasisi, huwa tunawashauri waweke logo zao na contacts vile vile.

Hatuoni ubaya hata kidogo.

Tuache kuongelea vitu vyepesi vyepesi tujikite kwenye maslahi ya Taifa kwanza.
 
Hii imenisikitisha sana;makampuni tanzu ya serikali yanatoa hela zetu kupongeza then viongozi hao hao waliotoa hizo hela wanakuja kwenye media na kutuzuga kuwa tusikubali hela zetu zitumike kwa maabo yasiyo na faida kwa walipa kodi!

Why walitoa kama walijua kumpongeza mshindi HAITAKIWI ITUMIKE HATA SENTI MOJA YETU?
 
Sasa kuna kitu gani kibaya hapo, kupeana pongezi kwa mtu aliyeshinda ni utamaduni wetu watanzania.

Na mbali ya hapo hizo salam za pongezi zimeendana na kuongeza publicity ya hizo taasisi, huwa tunawashauri waweke logo zao na contacts vile vile.

Hatuoni ubaya hata kidogo.

Tuache kuongelea vitu vyepesi vyepeshi tujulite kwenye maslahi ya Taifa kwanza.

Kumbe sio jungu......wewe ni SALVA
 
Hii hapana. Nitarudi.

Kukaa kimya nitapata laana. Kwenye kata yangu Milioni 50 zinatosha kuondoa tatizo la maji safi na salama milele. Kata ina wananchi zaidi ya elfu 20! Huu ni upuuzi.
 
Sasa kuna kitu gani kibaya hapo, kupeana pongezi kwa mtu aliyeshinda ni utamaduni wetu watanzania.

Na mbali ya hapo hizo salam za pongezi zimeendana na kuongeza publicity ya hizo taasisi, huwa tunawashauri waweke logo zao na contacts vile vile.

Hatuoni ubaya hata kidogo.

Tuache kuongelea vitu vyepesi vyepesi tujikite kwenye maslahi ya Taifa kwanza.

haya ndio maslahi ya taifa kwanza!tunapongezana kwa lipi?fedha hizi zingetumika kuwazawadia au kuwapongeza watumishi bora wa afya hapo ningeona tuna akili!
 
Hii ni shule ya Msingi Wilayani-Bagamoyo;wangewekeza milion 10 tu kati ya hizo walizotumia kumpongeza JK watoto wetu hawa wasingesoma kwenye mazngira bora zaidi! View attachment 27742
 
Sasa kuna kitu gani kibaya hapo, kupeana pongezi kwa mtu aliyeshinda ni utamaduni wetu watanzania.

Na mbali ya hapo hizo salam za pongezi zimeendana na kuongeza publicity ya hizo taasisi, huwa tunawashauri waweke logo zao na contacts vile vile.

Hatuoni ubaya hata kidogo.

Tuache kuongelea vitu vyepesi vyepesi tujikite kwenye maslahi ya Taifa kwanza.

piga kimya!
 
Wakati umefika kila mwenye nafasi ya kuiibia serikali aibe maana hao wenye dhamana na mali zetu wamegeuka kuwa majangili
 
Kuwapongeza kwa mamilioni yote hayo,wakipiga simu ya Dk 5 hazitoshi kufikisha ujumbe?! ubadhirifu mwingine huu ni lazima ukomeshwe..
 
Jamani haya magamba hayako huko chamani tu, hata kwenye taasisi na mashirika ya umma, kuna haja gani taasisi moja kupongeza mara 16 au zaidi, ili iweje?

Walikua wanapongeza nini sasa?!! Kwani wangejenga maabara kwenye shule za kata au wakaongeza vitanda kwenye mahospitali, au hata wakachimba visima virefu kwenye vijiji vyenye shida ya maji wasingejitangaza, mbona kuna mambo mengi sana ya kufawafanyia wananchi na TZ nzima ikakufahamu.

Hizo ni sifa za kijinga.
 
Sasa kuna kitu gani kibaya hapo, kupeana pongezi kwa mtu aliyeshinda ni utamaduni wetu watanzania.

Na mbali ya hapo hizo salam za pongezi zimeendana na kuongeza publicity ya hizo taasisi, huwa tunawashauri waweke logo zao na contacts vile vile.

Hatuoni ubaya hata kidogo.

Tuache kuongelea vitu vyepesi vyepesi tujikite kwenye maslahi ya Taifa kwanza.

Yaani 176.0m kutumika kupongeza tuu ni jambo jepesi? na ukiangalia hayo ni matangazo yaliyofanyika kwa kipindi cha mwezi mmoja tu, you are not serious. nilitegemea utasema hii ni serious issue na mtatafuta ukweli wa matumizi haya kama yalikua halali au watu walijitafutia ulaji.
 
Sasa kuna kitu gani kibaya hapo, kupeana pongezi kwa mtu aliyeshinda ni utamaduni wetu watanzania.

Na mbali ya hapo hizo salam za pongezi zimeendana na kuongeza publicity ya hizo taasisi, huwa tunawashauri waweke logo zao na contacts vile vile.

Hatuoni ubaya hata kidogo.

Tuache kuongelea vitu vyepesi vyepesi tujikite kwenye maslahi ya Taifa kwanza.

Boy you are naked.....you forget to take your clothes.....Au ndio provisions za mkataba wa ajira uliyopewa na wafu wenzako

Be ashamed.................Utachakaa kwa kutumiwa sana tena nje ya ufahamu wako...bul****it
 
Ngoja tusimame kwa dakika moja na kuwakumbuka wale wote waliokosa elimu bora, waliotangulia mbele ya haki kwa ajali za uzembe barabarani, ukosefu wa huduma bora za afya, njaa na ukame. Pia tuwakumbuke walimu na manesi wanaofanya kazi katika mazingira magumu, wajane na watoto waliofiwa na baba zao, yatima wanaoteseka, tuzikumbuke barabara zetu, hospitali zetu, maktaba na maabara zetu, polisi wetu. Tukumbuke pia ofisi zetu za serikali kama idara ya ardhi na mahakama.

Kwa ruhusa yenu naomba tutumie dakika 5 au zaidi maana dakika 1 haitoshi.

Ila, hii ni dharau kwa watanzania. Ni kuiga maisha tusiyoyastahili. Kumpongeza Raisi sio lazima gazetini. Wangetuma kadi ya pongezi au barua ingetosha. Huu ni wizi na ubadhirifu. Matumizi mabaya ya fedha kidogo tulizonazo.

Hakuna sababu ya kujitangaza kwa gharama za wananchi. Taasisi yeyote ijitangaze kwa ufanisi na sio magazeti.
 
Kuna kikao fulani cha harusi nahudhuria michango imeshafikia milioni 42. Watanzania ndivyo tulivyo hata katika maisha yetu ya kawaida.
 
Back
Top Bottom