Serikali Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Line Za Simu

Serikali Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Line Za Simu

Serikali Imetoa Ufafanuzi Kuhusu Tamko Lake La Awali Kuhusu Umiliki Wa Line Za Simu.Tamko La Awali Lilieleweka Kuwa Mtu Anatakiwa Kuwa Na Line Moja Tu Ya Simu.

Ufafanuzi Huo Umesema Kuwa, Ni Line Moja Kwa Mtandao Mmoja Wa Simu!

Chanzo: ITV HABARI[/QUOTE kiswahili kinaeleweka ufafanuzi wa nini. mi nasgauri kabla hawajatoa taarifa yoyote kwa jamii .wajipange ...kwakweli yajayo yanasikitisha.
 
Sijaona waziri asiyejiamini kama yule aliyetoa lile wazo la kua na laini moja. Inaelekea lile wazo alipewa na mkewe ali amonite mienendo ya mchepuko wa waziri. Bure kabisa. Eti ukinunua laini nyingine TUNAKUONA. mnione nyie majini ?
 
Yah. kwamba hauruhusiwi kumiliki gari aina ya Toyota zaidi ya moja. Kama unataka changanya viwanda au omba kibali.
Yeah Mkuu,
Na kwa sie tulioruhusiwa kuoa mke zaidi ya Mmoja basi huruhusiwi kuoa Wake kutoka Kabila moja, kama unataka basi changanya makabila au omba kibali.
 
Serikali Imetoa Ufafanuzi Kuhusu Tamko Lake La Awali Kuhusu Umiliki Wa Line Za Simu.Tamko La Awali Lilieleweka Kuwa Mtu Anatakiwa Kuwa Na Line Moja Tu Ya Simu.

Ufafanuzi Huo Umesema Kuwa, Ni Line Moja Kwa Mtandao Mmoja Wa Simu!

Chanzo: ITV HABARI
Mbona ndo inavyotakiwa hivyo
 
Wamebugi bado.
Kwanini wanikwaze mimi ninayetaka kuwa na laini moja ya voda (simu yangu) laini nyingine ya voda (watoto wangu nyumbanj plus beki tatu) laini nyingine ya voda kwenye (modem ya voda), au ndio kunilazimisha ninunue laini ya TTCL?
Upeo huu wa kufikiria mambo ni mdogo sana
 
Wamebugi bado.
Kwanini wanikwaze mimi ninayetaka kuwa na laini moja ya voda (simu yangu) laini nyingine ya voda (watoto wangu nyumbanj plus beki tatu) laini nyingine ya voda kwenye (modem ya voda), au ndio kunilazimisha ninunue laini ya TTCL?
Ndiyo ujieleze sasa, kufafanua matumizi yako!
Ile, FEDHA HIYO WEKA KWENYE NAMBA HII........zitapungua!
 
Niji
Ndiyo ujieleze sasa, kufafanua matumizi yako!
Ile, FEDHA HIYO WEKA KWENYE NAMBA HII........zitapungua!
Nijieleze nini sasa?
Nini umuhimu wa kusajili laini?
Walipoanzisha utaratibu wa kusajili walitutangazia kuwa mtu uko huru kuwa na laini idadi yoyote kwa mtandao wowote alimradi tu zisajiliwe.
Sasa ya nini kuanza kusumbuana tena?
Unless uniambie wafanyakazi wa TCRA wamejikuta hawana shughuli ya kufanya na wameamua kujiongezea kazi.
Kama wameshindwa kukamata matapeli ni uzembe wao, wasitusumbue sie raia wema.
 
Mkuu,
Sio kubadilisha maneno. Ignorance, watanzania asilimia kubwa hawana elimu hivyo uelewa ni mdogo hapati maagizo yalitolewa kwa umakini na kuyaelewa kisha mtu huyu ndiye mpashaji mkuu.
Ukiwatathmini watanzania kwa umakini, kama ingewezekana wote wangekuwa waandishi wa habari kama ingewezekana....wanapenda ushuhuda!
Marekani alishangaa Bomu la ubalozi wa marekani hapo Laibon badala ya kukimbia janga wanakimbilia janga ili wawe na la kuwajuza wasioona. Habari zinazotoka kwa mashuhuda zinakuwa za upotoshaji.
Radio mbao ni nyingi ndio sababu taarifa za kipuuzi nyingi!
Aliyetoa tamko alipaswa kuhskikisha kuwa kila mtanzania ataelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata aliyetoa kauli ya " mtu mmoja line moja ya simu" haelewi alitaka kusemaje.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu,
Kwani yeye nani? Si walewale! Wakati mwingine ubabe, wakati mwingine sifa aonekane amefanya jambo la maana, sasa pupa zoote hizo anajikuta hawezi kutoa tamko linaloeleweka. Akili ni nywele kila mtu ana zake lakini waliozaliwa ni wajinga ni wengi. Kusoma au kuchaguliwa uwakilishi au ungozi maana yake umewazidi halaiki akili hapana!
 
Bado ufafanuzi wa serikali kuhusu laini moja ni tata! Kwa nini wanakosa akili ndogo tu ya kuangalia aina za huduma zitolewazo na makampuni haya ya simu ili waweze kutunga vizuri hizo sheria zao za kishamba!
Binafsi ninamiliki laini tatu za mtandao mmoja, na zote zinatumika kwasababu ni huduma halali zinazotolewa na huo mtandao.
1. Laini ya simu kwa maongezi.
2. Laini kwenye modem.
3. Laini kwenye GPS kit ndani ya gari.
Hizi ni huduma zinazotolewa na makampuni yote ya simu na kila mtu ana uhuru wa kuchagua mtandao wake kwa sababu zake na mahitaji yake. Akili za hawa watu huwa wanazitoa wapi! #vodacomtz #tigo #airtel
 
Back
Top Bottom