Ilumine
Senior Member
- Dec 27, 2008
- 196
- 4
WAKATI jana Waislamu nchini waliungana na wengine duniani kusherehekea Sikukuu ya Idd El Hadj, Serikali imetoa tumaini jipya la kuwapatia Mahakama ya Kadhi.
Tumaini hilo jipya kwa Waislamu nchini limetolewa jana na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal wakati akijibu salamu za Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata), zilizotolewa wakati wa Baraza la Idd na Mwanasheria wa baraza hilo, Abdallah Rashid Matumla jana Msikiti wa Simba Mbali Temeke Dar es Salaam ambapo pia ilifanyika Swala ya Idd kitaifa.
Katika salamu hizo, Matumla aliitaka Serikali kurakishe utaratibu wa urejeshaji wa mahakama hiyo nchini ili kuwawezesha Waislaam kuendesha shughuli zao za kiimani kama ilivyoelekezwa katika Kur-an na Sunna.
Hata hivyo, akijibu salamu hizo za Bakwata, Dk Bilal aliyekuwa mgeni rasmi katika Baraza hilo la Idd, aliahidi kuwa Waislamu nchini kuwa wataona matunda mazuri ya kilio hicho hivi karibuni.
Kuhusu Mahakama ya Kadhi, insha-Allah Mungu atatuwafikisha kuona matunda mazuri muda si mrefu,alisema Dk Bilal
Awali mwanasheria huyo wa Bakwata mbele ya makamu wa rais alisema ,Tunaiomba Serikali yako tukufu iharakishe utaratibu wa kuundwa kwa Mahakama ya Kadhi nchini, ili Waislaam waweze kuendesha shughuli zao kama walivyoelekezwa katika Kur-an.
Matumla alisema Waislamu nchini wana hamu ya kujua hatua iliyofikiwa kuhusu suala la urejeshwaji wa Mahakama ya Kadhi ambapo aliwaambia kuwa, jitihada za kukamilisha suala hilo zinaendelea.
Ni matumaini yetu na kwa hakika matumaini ya Waislamu na Watanzania kwa ujumla kwamba kwa kuwa shughuli ya Uchaguzi Mkuu imekamilika, jopo la masheikh na la serikali watarudi mezani haraka kuendelea na mchakato,alisema
Naye Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Ismail Habibu Makusanya alionya kuwa, iwapo Serikali haitaongozwa kwa mujibu wa katiba na sheria huku viongozi wa dini wakikubali kuchakachuliwa, Tanzania haitakalika tena.
Akitoa nasaha zake, Sheikh Makusanya alisema iwapo vitu viwili havitaangaliwa kwa umakini, amani na mshikamano wa kitaifa utapotea.
Kitu cha kwanza ni Serikali; kama serikali haitaendeshwa kwa misingi ya kikatiba na kisheria, utawala bora na kulinda haki za binadamu, ukweli na uwazi, nchi hii haitakalika kwa sababu tutapoteza amani na mshikamano wetu wa kitaifa, alisema Sheikh Makusanya.
Sheikh Makusanya alifafanua kuwa, Kitu cha pili ni viongozi wa dini; kama viongozi wa dini tutaacha kufuata miongozo ya vitabu vyetu na tukakubali kuchakachuliwa kirahisi na kupafanya mahali patukufu kwenye nyumba za ibada kuwa majukwaa ya kuwagawa watu, ni wazi amani haitokuwapo tena.
Hapa (msikitini) sio mahala pa kuwagawa watu kwa rangi, kabila, dini wala itikadi zao bali ni mahali pa kuhubiri amani, umoja, utulivu na mshikamano wa kitaifa. Viongozi wa dini tusikubali kuchakachuliwa, ni hatari, alisema Sheikh Makusanya.
Aidha, Makusanya aliwakata Waislaam kutumia hekima na busara katika kuikosoa Serikali, kwa jambo hilo limewekewa taratibu zake katika maandiko matukufu.
Hata hivyo, katika baraza hilo, makamu wa rais alizungumzia pia safari za Hija, ambapo aliitaka Bakwata kuchukua jukumu la kuratibu safari za mahujaji ili kuzuia kasoro mbalimbali zinazojitokeza ambazo wakati mwingine husababisha baadhi ya waislamu kushindwa kutimiza nguzo hiyo wakati wamekamilisha taratibu zote zinazotakiwa na taasisi zinazoshughulikia masuala hayo.
Naliomba baraza lichukuwe jukumu la kuratibu shughuli za kuepeleka mahujaji wa Tanzania huko Mecca ili kuzuia kasoro zinazojitokeza mwaka hadi mwaka katika Taasisi mbalimbali zinazoratibu shughuli za Hijja hapa nchini,alisema
Katika salamu zake hizo, Dk Bilal aliipongeza Bakwata kwa jitihada zake za kuimariisha elimu, afya, uchumi na ustawi wa jamii na kulitaka Baraza hilo kuongeza nguvu katika kuimarisha elimu kutoka ngazi ya chekechea hadi chuo kikuu.
Kutoka mkoani Arusha Imamu wa Msikiti Mkuu wa Mkoa huo, Sheikh Mohammed Hambal amewashauri Watanzania kuweka kando itikadi zao za kisiasa, kuungana na kuwa kitu kimoja katika kuipokea na kuikubali serikali iliyopo madarakani kwa lengo la kuimarisha amani, utulivu na upendo uliokwepo tangu awali.
Mkoani Tanga, Waislamu wameitumia swala ya Idd El Haji kwa kuilombea Taifa la Tanzania liendelee kuwa na amani na utulivu katika kipindi hiki ambacho taifa lipo katika mchakato wa kuunda Serikali bada ya Uchaguzi Mkuu.
Maombi hayo ya amani yalifanyika katika msikiti wa Qubba Wilayani Pangani ambako Mjumbe wa Halamshauri Kuu Bakwata Taifa, Shekhe Juma Luwuchu aliongoza hiyo ya swala ya Idd kwa kuswalisha na baadaye kutoa mawaidha ya Idd.
Imeandaliwa na Salim Said, Dar, Burhani Yakub Steven William,Tanga na Moses Mashalla,Arusha- GAZETI - MWANANCHI