Serikali yatoa tumaini Mahakama ya Kadhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yatoa tumaini Mahakama ya Kadhi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ilumine, Nov 18, 2010.

 1. Ilumine

  Ilumine Senior Member

  #1
  Nov 18, 2010
  Joined: Dec 27, 2008
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAKATI jana Waislamu nchini waliungana na wengine duniani kusherehekea Sikukuu ya Idd El Hadj, Serikali imetoa tumaini jipya la kuwapatia Mahakama ya Kadhi.

  Tumaini hilo jipya kwa Waislamu nchini limetolewa jana na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal wakati akijibu salamu za Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata), zilizotolewa wakati wa Baraza la Idd na Mwanasheria wa baraza hilo, Abdallah Rashid Matumla jana Msikiti wa Simba Mbali Temeke Dar es Salaam ambapo pia ilifanyika Swala ya Idd kitaifa.

  Katika salamu hizo, Matumla aliitaka Serikali kurakishe utaratibu wa urejeshaji wa mahakama hiyo nchini ili kuwawezesha Waislaam kuendesha shughuli zao za kiimani kama ilivyoelekezwa katika Kur-an na Sunna.

  Hata hivyo, akijibu salamu hizo za Bakwata, Dk Bilal aliyekuwa mgeni rasmi katika Baraza hilo la Idd, aliahidi kuwa Waislamu nchini kuwa wataona matunda mazuri ya kilio hicho hivi karibuni.

  “Kuhusu Mahakama ya Kadhi, insha-Allah Mungu atatuwafikisha kuona matunda mazuri muda si mrefu,”alisema Dk Bilal

  Awali mwanasheria huyo wa Bakwata mbele ya makamu wa rais alisema ,“Tunaiomba Serikali yako tukufu iharakishe utaratibu wa kuundwa kwa Mahakama ya Kadhi nchini, ili Waislaam waweze kuendesha shughuli zao kama walivyoelekezwa katika Kur-an.”

  Matumla alisema Waislamu nchini wana hamu ya kujua hatua iliyofikiwa kuhusu suala la urejeshwaji wa Mahakama ya Kadhi ambapo aliwaambia kuwa, jitihada za kukamilisha suala hilo zinaendelea.

  “Ni matumaini yetu na kwa hakika matumaini ya Waislamu na Watanzania kwa ujumla kwamba kwa kuwa shughuli ya Uchaguzi Mkuu imekamilika, jopo la masheikh na la serikali watarudi mezani haraka kuendelea na mchakato,”alisema

  Naye Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Ismail Habibu Makusanya alionya kuwa, iwapo Serikali haitaongozwa kwa mujibu wa katiba na sheria huku viongozi wa dini wakikubali kuchakachuliwa, Tanzania haitakalika tena.

  Akitoa nasaha zake, Sheikh Makusanya alisema iwapo vitu viwili havitaangaliwa kwa umakini, amani na mshikamano wa kitaifa utapotea.

  “Kitu cha kwanza ni Serikali; kama serikali haitaendeshwa kwa misingi ya kikatiba na kisheria, utawala bora na kulinda haki za binadamu, ukweli na uwazi, nchi hii haitakalika kwa sababu tutapoteza amani na mshikamano wetu wa kitaifa,” alisema Sheikh Makusanya.

  Sheikh Makusanya alifafanua kuwa, “Kitu cha pili ni viongozi wa dini; kama viongozi wa dini tutaacha kufuata miongozo ya vitabu vyetu na tukakubali kuchakachuliwa kirahisi na kupafanya mahali patukufu kwenye nyumba za ibada kuwa majukwaa ya kuwagawa watu, ni wazi amani haitokuwapo tena.”

  “Hapa (msikitini) sio mahala pa kuwagawa watu kwa rangi, kabila, dini wala itikadi zao bali ni mahali pa kuhubiri amani, umoja, utulivu na mshikamano wa kitaifa. Viongozi wa dini tusikubali kuchakachuliwa, ni hatari,” alisema Sheikh Makusanya.

  Aidha, Makusanya aliwakata Waislaam kutumia hekima na busara katika kuikosoa Serikali, kwa jambo hilo limewekewa taratibu zake katika maandiko matukufu.

  Hata hivyo, katika baraza hilo, makamu wa rais alizungumzia pia safari za Hija, ambapo aliitaka Bakwata kuchukua jukumu la kuratibu safari za mahujaji ili kuzuia kasoro mbalimbali zinazojitokeza ambazo wakati mwingine husababisha baadhi ya waislamu kushindwa kutimiza nguzo hiyo wakati wamekamilisha taratibu zote zinazotakiwa na taasisi zinazoshughulikia masuala hayo.

  “Naliomba baraza lichukuwe jukumu la kuratibu shughuli za kuepeleka mahujaji wa Tanzania huko Mecca ili kuzuia kasoro zinazojitokeza mwaka hadi mwaka katika Taasisi mbalimbali zinazoratibu shughuli za Hijja hapa nchini,”alisema

  Katika salamu zake hizo, Dk Bilal aliipongeza Bakwata kwa jitihada zake za kuimariisha elimu, afya, uchumi na ustawi wa jamii na kulitaka Baraza hilo kuongeza nguvu katika kuimarisha elimu kutoka ngazi ya chekechea hadi chuo kikuu.

  Kutoka mkoani Arusha Imamu wa Msikiti Mkuu wa Mkoa huo, Sheikh Mohammed Hambal amewashauri Watanzania kuweka kando itikadi zao za kisiasa, kuungana na kuwa kitu kimoja katika kuipokea na kuikubali serikali iliyopo madarakani kwa lengo la kuimarisha amani, utulivu na upendo uliokwepo tangu awali.

  Mkoani Tanga, Waislamu wameitumia swala ya Idd El Haji kwa kuilombea Taifa la Tanzania liendelee kuwa na amani na utulivu katika kipindi hiki ambacho taifa lipo katika mchakato wa kuunda Serikali bada ya Uchaguzi Mkuu.

  Maombi hayo ya amani yalifanyika katika msikiti wa Qubba Wilayani Pangani ambako Mjumbe wa Halamshauri Kuu Bakwata Taifa, Shekhe Juma Luwuchu aliongoza hiyo ya swala ya Idd kwa kuswalisha na baadaye kutoa mawaidha ya Idd.

  Imeandaliwa na Salim Said, Dar, Burhani Yakub Steven William,Tanga na Moses Mashalla,Arusha- GAZETI - MWANANCHI
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Nasikitika kusema ndugu zetu Waislamu wata kuwa wame "ingizwa mjini" kwenye haya maswala ya OIC na mahakama ya kadhi. Kama CCM inge taka kuya tekeleza haya wangesha yatekeleza. Ila kila siku Waislamu wana pewa "tumaini" jipya. Ngoja tuone ila kwa hili naona ni siasa tupu mpaka sasa.
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Serikali ikianza kugharamia hizo kadhi sijui nini, nitaacha rasmi kulipa kodi.
   
 4. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kamwe haiwezekani kutumia kodi ya kafiri(Non muslim) kugharamia shughuli za mahakama ya kadhi!.What I know for sure,Tanzania Government is a secular government,it will never be biased in favour of any religion.Hata kama Rais,makamu wa rais ,mawaziri muhimu na viongozi mbalimbali wa serikali wakiwa ni waislamu,kamwe hawataweza kuibadilisha nchi hii iwe ya kiislamu kama ilivyo Ilan au Sudan.Mikakati yote wanayoifanya ni kujidanganya tu na kupoteza muda wao.Nafikiri sasa tumeshachoka amani na tunajaribu kuandaa vurugu!!

  Tanzania bila Mahakama ya kadhi na OIC inawezekana!!!
   
 5. m

  matambo JF-Expert Member

  #5
  Nov 18, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  inshallah Mwenyezi Mungu awape wepesi kulishughulikia kadhia la mahakama ya kadhi, kwani twaisubiri kwa hamu, na pole kwao wasio ifahamu !!
   
 6. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #6
  Nov 18, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hivi hili suala mbona lilipatiwa majibu bungeni katika bunge lililopita kwamba serikali haihusiki na uendeshaji wa masuala yanayohusu imani/dini? Ufafanuzi wa msingi ulikuwa kuwa Serikali ya Tanzania haina dini, inakuwaje hili suala linaendelea kung'ang'aniwa na Waislamu.
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Nov 18, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hatuna haja ya kuifahamu. Tunachotaka na kilicho muhimu kwetu ni accountability ya kodi zetu.
   
 8. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #8
  Nov 18, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 853
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 80
  Mkuu hatuikatai mahakama ya kadhi!!!! Ila kitu ambacho tunakipinga kwa nguvu zoote ni eti itambuluke kikatiba...kwa kuingizwa katika legal framework ya nchi...

  Hii ina maana kwamba Hakimu wa mahakama hiyo alipwe na serikali kupitia kodi za wananchi(both muslims, christians, and others).... Hapa ndio panaleta shida

  Vile vile kwa taratibu za OIC, endapo nchi itaridhia mahakama ya kadhi kikatiba basi automatically nchi hiyo inakuwa ni nchi ya kiislamu (wakati katiba yetu inasema nchi ni ya ki-secular)

  Waislam wanachotakiwa kufanya ni kuunda mahakama ya kadhi ndani taratibu za dini yao. Nothing else!!!
   
 9. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #9
  Nov 18, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Suala kuu ni nani atagharamia hayo mahakama ya kadhi....katu si kwa kodi za Watanzania
   
 10. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #10
  Nov 18, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Jiandae kupigwa mawe
   
 11. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #11
  Nov 18, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Huyo jamaa mgeni katika serikali,labda hakufuatilia bunge lililopita kuwa mahakama ya kadhi haihusiani na shughuli za serikali.Mjadala huu ulishafungwa.Namna yoyote ile ya kuishinikiza serikali igharimie kadhi ni kuleta mgogoro wa kidini nchini.
   
 12. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #12
  Nov 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Mod, tafadhari do ze needful, kuna post tatu zinazungumzia swala hili, ni vizuri zingeunganishwa. Ciao.
   
 13. GITU

  GITU Member

  #13
  Nov 18, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu kama ni hivyo,hata wakristo nao pia watahitaji mahakama yao?Je inamaana nchi itaendeshwaje? Kama si kuleta masuala ya umwagaji damu,kama nigeria naomba kwa jina la MUNGU WA MBINGUNI ISIWEPO MAHAKAMA hiyo kwani,utakuwa ni mwanzo wa uingizwaji wa silaha maana wenzutu kwa kujitoa mhanga ni kawaida! in fact we don't like that.
   
 14. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #14
  Nov 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  kimsingi uwepo wa mahakama ya kadhi ilishaidhinishwa, hatuna haja ya kujadiri tena.
   
 15. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #15
  Nov 18, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,407
  Likes Received: 3,737
  Trophy Points: 280
  Na kwa wanawake wasiolewa wajiandae kuuwawa siku watakapojifungua mtoto bila ya baba wa ndoa............... Na itabidi waanze na wazazi wenzie JK maana ana watoto zaidi ya saba wenye mama tofauti tofauti........... Na Anna Mkapa naye ajiandae baada ya hii Kadhia ya mahakama ya KADHI kupitishwa
   
Loading...