Serikali yatoa siku 4 kwa wafanyabiashara wa Korosho kusema tani wanazohitaji. Baada ya hapo hawataruhusiwa tena kununua

Maigizo bado yanaendelea kumbe now ni Koro-show adi kufikia 2020 tutaelewa maana halisi ya kuiondoa ccm madarakan
 

*Yawataka waandike barua wakionesha tani wanazohitaji na lini watazichukua

*Yasema zaidi ya hapo haitoruhusu kampuni yoyote kununua korosho tena


SERIKALI imetoa siku nne kwa wanunuzi wote 35 waliojiandikisha kununua korosho wawe wamepeleka barua katika Ofisi ya Waziri Mkuu wakionesha kiasi cha tani wanazohitaji na lini watazichukua.

“Hivyo wanunuzi waliojiandikisha wakiwemo na wale wote ambao wamekuwa wananunua kwenye minada lakini kwa kiasi kidogo, wahakikishe ndani ya siku hizo nne kuanzia leo Ijumaa hadi Jumatatu saa 10 alasiri wawe wameleta barua na ofisi yangu ipo wazi saa 24.”

Hayo yamesemwa leo (Ijumaa, Novemba 9, 2018) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akitoa tamko la Serikali kuhusu ununuzi wa zao la korosho, ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma.

Baada ya kupita siku hizo Serikali italazimika kufuta usajili kwa wote waliojisajili kununua zao hilo kwa sababu walikubaliana kwenda kununua lakini hali inayoonekana sasa ni kama kumkomoa mkulima kitu ambacho imesema haitakubaliana nacho.

“Mwenye nia ahakikishe katika siku hizo nne iwe ndio mwisho wa kununua korosho na waandike barua kwani ofisi yangu ipo wazi saa 24 wana nafasi ya kuleta barua wakati wowote wakionesha nia yao na kiwango wanachokihitaji. Zaidi ya hapo Serikali haitoruhusu kampuni yoyote kununua korosho tena.”

Waziri Mkuu amesema kwenye msimu wa ununuzi wa korosho wa mwaka huu, walishuhudia kusuasua kwa minada, ambapo Serikali ilikutana na wanunuzi wa korosho katika kikao kilichoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli ambapo walikubaliana kununua kwa bei inayoanzia sh 3,000 na kuendelea.

“Mjadala ulikuwa wa wazi na wafanyabiashara wenyewe walipendekeza bei ambayo ilikuwa inaanzia sh. 3,000, hata hivyo baada ya kikao hicho ununuzi katika minada imeendelea kusuasua na hata tani zilizokuwa zikinunuliwa zilikuwa kidogo sana. Sisi tunaiona hali hii kama mgomo baridi ambao si sawa sawa sana kwani malengo yetu sisi na sekta binafsi ni kumfanya mkulima apate bei nzuri.

Hali hii haifurahishi kwa sababu Serikali imedhamiria kuboresha mazao yanayolimwa na wakulima kwa kuwasaidia kuanzia katika hatua za utayarishaji wa mashamba, upatikanaji wa pembejeo na masoko ili waweze kunufaika na kilimo na kupata tija katika mazao hayo.”

Waziri Mkuu amesema baada ya kugundua bei imekuwa tatizo Serikali ilifanya jitihada za kupeleka wataalamu wake katika masoko makuu duniani na kupata bei halisi ambayo bado inatosha kumlipa mkulima sh 3,000.

Hatua hiyo imekuja baada ya zao la korosho kuendelea kununuliwa kwa bei ya chini na idadi ya wanunuzi kuwa ya chini licha ya uzalishaji wa mwaka huu kuwa mdogo ukilinganisha na msimu wa mwaka jana.

Amesema msimu wa mwaka jana uzalishaji ulikuwa zaidi ya tani 300,000 na mwaka huu zinatarajiwa tani zaidi ya 200,000 hivyo wafanyabiashara wanao uwezo kununua korosho zilizopo.

Hata hivyo Serikali imewataka wananchi hususani wakulima wa korosho nchini kuendelea kuwa wavumilivu na watulivu wakati ikiendelea kushughulikia suala hilo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
 
Hii ni moja kati ya serikali ya kipumbavu duniani. Inayoamini mabadiliko ndani ya nchi yanaletwa kwa ukali na vitisho vya kijinga.
 
Mbona hivi jamani kweli ndio hii nchi yetu Tanzania? Vitisho vitisho sawa ila kila chenye mwanzo kina mwisho wake
 
kwa hisani ya Sikwangalasyene ..........

1. hali za wakulima zinatia simanzi. Masoko ya mazao ya wakulima yamevurugwa

2. wafanyakazi hawakopesheki kwa kuwa hawajaongezewa mishahara kwa miaka mitatu mfululizo hivyo kutokidhi vigezo vya makato

3. biashara zimevurugwa

4. kodi inakusanywa kwa vitisho

5. biashara kama enzi za ukoloni

6. hakuna uwazi kwenye manunuzi (Ndege zimenunuliwa pasipo kufuata taratibu)

7. kuna double standard kwenye kuwajibisha watumishi (Upendeleo)

8. vyombo vya habari havipo huru tena

9. wananchi wamenyimwa haki ya mijadala ya wazi

10. serikali haipo radhi kukosolewa

11. kila mwenye mamlaka ana kauli ya mwisho (Wakuu wa Wilaya na Mikoa wamekuwa kero)

12. upotoshaji kwenye hali ya uchumi wa nchi ni mkubwa

13. 1.5 trillion hazina maelezo (Kuna wizi na ufisadi mkubwa kuwahi kutokea)

14. polisi wanafanya kazi za CCM na si kwa maslahi ya wananchi

15. usalama wa viongozi ni kipaumbele na si usalama wa nchi
Traffic wanakusanya kod
 
Zamani tulisoma somo lililoitwa Political Economy lililokuwa likiongelea "antagonistic relationship" kati ya "bourgeoisie" na "proletariats" na porojo nyingine nyingi za akina Carl Marx na wenzake. Nadhani hili sasa litakuwa somo jipya la Political business itakuwa pia inahusu antagonistic relationship kama sikosei. Wale wa enzi zangu nadhani mmeelewa.
 
Yasijirudie ya sukari na mafuta h
Sasa issue iko kwwnye maziwa na kuku. Maziwa robo lita sasa ni shs1500/ kutoka tshs 600/ kuku wa kisasa ni 10,000/ kutoka tshs 5500/ ndio serikali ya wanyonge hiyo.. Kila mahali jii serikali ya wanyonge ikitia mkono ni tatizo kwa wanyonge...
 
Sasa issue iko kwwnye maziwa na kuku. Maziwa robo lita sasa ni shs1500/ kutoka tshs 600/ kuku wa kisasa ni 10,000/ kutoka tshs 5500/ ndio serikali ya wanyonge hiyo.. Kila mahali jii serikali ya wanyonge ikitia mkono ni tatizo kwa wanyonge...

Jombaa chips kavu buku mbili sijui hicho kiazi kimechimbwa mererani "mbuguni"
 
Back
Top Bottom