Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Serikali imetangaza rasmi alama za Jumuiya ya Afrika Mashariki zitakazotumika kwenye Ofisi zote za Serikali na katika shughuli zote rasmi za kiserikali.
Aidha Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mindi Kasiga amezitaja alama hizo kuwa ni bendera ya Taifa, bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, wimbo wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na wimbo wa Taifa.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inaratibu upatikanaji wa sampuli ya alama hizo kwa gharama za taasisi, wizara au Ofisi husika.
Pia mkuu huyo wa kitengo cha mawasiliano ndugu Kasiga amesema kuanzia sasa bendera ya Jumuiya hiyo itapepea sambamba na Bendera ya Taifa kwenye Ofisi zote za Serikali huku wimbo wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ukiimbwa sambamba na wimbo wa Taifa katika shughuli rasmi za serikali kuanzia ngazi za Halmashauri hadi Taifa, hii ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa Mkataba wa uanzishwaji wa jumuiya hiyo kifungu cha 7(a).
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa wizara ya mambo ya nje amenukuliwa akisema “Mkataba huu unasisitiza jumuiya hii kuwa jumuiya ya watu, hivyo watanzania watahusishwa katika hatua zote za mtangamano huo, pamoja na kushirikishwa kikamilifu katika hatua mbalimbali za jumuiya ili kujua madhumuni ya kunufaika na fursa mbalimbali zitakazaopatikana ndani ya Jumuiya hiyo”, Mwisho wa kunukuu.
Matumizi ya alama hizi ni njia mojawapo ya kujenga uzalendo na kumfanya Mwananchi ajisikie kuwa sehemu ya ushirikiano huu.
Vilevile, taasisi binafsi zinaweza kutumia alama hizi, huku shule na vyuo vikisisitizwa kutumia alama hizi kama sehemu ya kuelimisha na kuhamasisha vijana kuhusu Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.