Serikali yasitisha matumizi picha ya Rais Magufuli

Serikali yasitisha matumizi picha ya Rais Magufuli

Serikali imesitisha matumizi ya picha ya Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Pombe Magufuli ambayo yalitakuwa kuanza leo kwa ofisi zake.

Uamuzi huo ulitolewa jana muda mfupi baada ya Serikali kuzindua picha hiyo, siku tatu tangu Magufuli kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Serikali inapenda kuzitaarifu ofisi za umma na wananchi kwa ujumlakwamba imesitisha matumizi ya picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Serikali ya Awamu ya Tano, Dk John Joseph Pombe Magufuli mpaka hapo itakapotangazwa tena, ilisomeka taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Idara ya Habari (Maelezo).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, awali majira ya saa 6. 00 mchana jana, Serikali ilitangaza kuhusu kuanza rasmi kwa matumizi ya picha hiyo ambayo ingeuzwa kwa Sh 15,000. Serikali ilisema itazitangazia ofisi hizo na Watanzania kuhusu kuanza tena kwa matumizi ya picha hiyo.

Uamuzi huo wa Serikali ulitolewa muda mfu baada ya kuzindua rasmi picha hiyo. Awali Mkurugenzi wa Maelezo, Assah
Mwambene alisema jana kuwa picha hizo zipo za kutosha na zinapatikana wakati wowote ilimradi iwe siku na muda wa kazi.

chanzo; gazeti la Mwananchi
 
Kama kuna watu wanaitia aibu hii serikali ni wale watu wa habari maelezo na kurugenzi ya mawasiliano ya pale ikulu.
Aisee ni shida kubwa...
 
Hizo gharama za picha 15,000 zilizopo analipa nani?
Hata kwa JK Ilitokea. We never learn!
 
naona muendelezo wa jk....kwanza AG,ukafatia usanii wa kutembelea wizara na sasa picha inabadilishwa kama ilivyobdilishwa ya JK..Nasubiri wasanii waanze kumiminika ikulu....hapa kazi tu.
 
nawaambieni haka kajamaa katazurura hii dunia kuliko jk.
 
Hasara hiyo nani anafidia????!!
Au ni dili hili ziko sita tu halafu waseme zilitengenezwa milioni mbili na zote hazifai??!!!

Maana hawa advanced camera men bhana. . . .
 
Nakuunga mkono ila naongeza.Sitaki Rais wetu avae tai nyekundu,shati jeupe na suti nyeusi,kwani yeye mganga wa kienyeji.Marangi mengine jamani myaachege, wanao yatumia wana maana!Labda kama na ninyi mna maana.
nimesema sitaki tai nyekundu...afadhali kuvaa tai ya bendera yetu....sitakiiiiiii
 
Nakuunga mkono ila naongeza.Sitaki Rais wetu avae tai nyekundu,shati jeupe na suti nyeusi,kwani yeye mganga wa kienyeji.Marangi mengine jamani myaachege, wanao yatumia wana maana!Labda kama na ninyi mna maana.

Tai nyekundu ina tatizo gani mkuu??? Au inawakilisha mambo Fulani Fulani tusiyoyafahamu????
 
Walikurupuka Inaonekana hata hawakumuonyesha! Hata kama ni kitu cha kiserekali nae anapaswa kuiona kwanza!
 
USHAURI- Magufuli kazi ya kwanzani ni ku-overhaul wafanyakzi wa IKULU ili unze nowapa wtakaoktii wewe otherwise utapata tabu.
 
Kama JK vile naona picha linarudiwa tu,ivi camera man bora ndugu Misupu yuko wapi au nae kaenda Msoga?
 
NA bado,mtajutaa sana,unafikiri picha ya Lowassa ingeitaji air brushing
 
Zile za kwanza hela walipiga watu wengine, wameamua kuzidump. Sasa mzee anataka zitengenezwe zingine apate hela za kuanzia kuuaga umaskini. Madili ndo yameshaanza.
 
Kupiga dili kuko pale-pale! Mtu keshajitengenezea ulaji. Eti "picha ziko za kutosha", hakuna kitu hapo - wizi mtupu!
Waweze kuandaa picha inayofaa kwa kampeni halafu hapa washindwe; NYOOOO!
MCC ni ile ile!
 
Back
Top Bottom