Serikali yasitisha matumizi picha ya Rais Magufuli

Serikali yasitisha matumizi picha ya Rais Magufuli

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,096
picha..jpg

Rais John Pombe Magufuli
​
Kwa ufupi
Uamuzi huo ulitolewa jana muda mfupi baada ya Serikali kuzindua picha hiyo, siku tatu tangu Magufuli kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dar es Salaam
Serikali imesitisha matumizi ya picha ya Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Pombe Magufuli ambayo yalitakuwa kuanza leo kwa ofisi zake.

Uamuzi huo ulitolewa jana muda mfupi baada ya Serikali kuzindua picha hiyo, siku tatu tangu Magufuli kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Serikali inapenda kuzitaarifu ofisi za umma na wananchi kwa ujumla kwamba imesitisha matumizi ya picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Serikali ya Awamu ya Tano, Dk John Joseph Pombe Magufuli mpaka hapo itakapotangazwa tena?" ilisomeka taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Idara ya Habari (Maelezo).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, awali majira ya saa 6. 00 mchana jana, Serikali ilitangaza kuhusu kuanza rasmi kwa matumizi ya picha hiyo ambayo ingeuzwa kwa Sh 15,000.

Serikali ilisema itazitangazia ofisi hizo na Watanzania kuhusu kuanza tena kwa matumizi ya picha hiyo. Uamuzi huo wa Serikali ulitolewa muda mfu baada ya kuzindua rasmi picha hiyo.

Awali Mkurugenzi wa Maelezo, Assah Mwambene alisema jana kuwa picha hizo zipo za kutosha na zinapatikana wakati wowote ilimradi iwe siku na muda wa kazi.

Chanzo: Mwananchi
 
Kwahiyo hizo "za kutosha" ndio zinakuwa trashed? Maana yaelekea picha ilikuwa na kasoro, wanapiga nyingine...
 
Ningeshangaa sana kama picha ile ingetumika. Yaani imetoka vibaya na ingetoa taswira mbaya ya rais wetu. Afadhali aliyekuwa na muono kama wangu
 
Walisoma maoni ya humu Jf.Mtu kachoka na kampeni haraka haraka picha.
 
Atumie 360 ili apate goodlooking
 
Wana kurupuka na hela wameshatumia kutengeneza zilizotoka tayari.
 
nimesema sitaki tai nyekundu...afadhali kuvaa tai ya bendera yetu....sitakiiiiiii
 
Hehehe ndo tatizo la kukurupuka,wangesubiri anywe juice za ikulu shavu litoke then wamtwange picha,
 
Kama kawaida wakurupukaji. Magu mwenyewe alikurupuka kuteua AG
 
Kwahiyo hizo "za kutosha" ndio zinakuwa trashed? Maana yaelekea picha ilikuwa na kasoro, wanapiga nyingine...

Mkulu bado kachoka na jua la kampeni.subiri sura inyooke kidogo kwa kiyoyozi cha ikulu tutapiga nyingine
 
Tanzania nchi yangu nakupenda hivyohivyo na vituko vyako!
 
Huu utawala mbona kila kitu wanaiga kwa utawala wa JK? Au ndo yale mambo ya kifaa cha kubadili channel za TV yaliyokuwa yanaelezwa yameanza kuonekana!! Maana kila kitu wanaiga hadi siku ya tukio!! Khaaaa!!!
 
Hii serikali yetu ni kuivumilia tu maana...
 
Back
Top Bottom