Serikali yasitisha mafunzo ya JKT

Kichwa Ndio Mtu

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2014
Posts
3,079
Reaction score
1,719

Maoni yangu:

Mafunzo haya ya JKT yapigwe marufuku kabisa na yafutwe maana hayana faida yoyote wala tija katikaTaifa hili. Binafsi natamani serikali ifilisike kabisa ili isiweze kufadhili mafunzo hata tena.

=================

Kanusho la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuhusu kusitisha mafunzo ya Jeshi kwa mujibu wa Sheria.


 
nani kadunganya serikali imeshndwa hela za kuifandili jakata?
 
Kuna faida na hasara za kupeleka vijana wengi JKT na kuwatupa uraini bila ajira... siku hawa wakiasi itakuwa ni mtafutano, iko wazi kwamba police hawataweza kupambana nao na hivyo kupekea kupambana na wanajeshi wenzao

Ni bora yasitishwe kwa mstakabali mwema wa taifa
 
Serikali ya CCM haina priority kila kiongozi akija anakuja na mambo yake tena kwa kukurupuka,kama ni kweli wala haitashangaza.
 
Wameshtuka eeh. Vijana wakakamavu kuundamana kuelekea ikulu kudai ajira si jambo dogo. Lazima status qou ishituke. Mikakati ni kupromote bongo flava siyo mafunzo ya kijeshi.
 
Msemaji wa hiyo kauli wa kusitisha ni nan?
 
Wenzetu wanaweka mkazo kufudisha vijana wao ujasiliamali na tecnolojia, sisi tumekazana kuifundisha jamii uasikali!
 
itakuwa maajabu ukisema serikali haina hela wakati watu wanaiba mabilioni ya hela kila mwaka je hizo hela zinatoka wapi kama serikali haina hela
 
JKT iendelee angalia hapa vijana walivyowakakamavu safi sana hapa ni parade ya kumaliza mafuzo.
 
Last edited by a moderator:

Wamesitisha mafunzo ya mujibu wa sheria au wamesitisha wa kujitolea hapo hujaeleweka mkuu umecreat uncertainity kwa raia
 
kwa kweli mimi naona haya mafunzo ya JKT walipaswa kushirikiana na VETA wawafundishe vijana vitu vya maana. UKAKAMAVU bila ajira ni sawa na UPROFESA bila HELA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…