Serikali yashauriwa kulifungulia Mwana Halisi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,111
kubenea(1).jpg

Mhariri Mtendaji wa gazeti la MwanaHalisi, Saed Kubenea


Serikali imeshauriwa kukutana na viongozi wa kampuni ya Hali Halisi ili kujadili namna ya kulifungulia gazeti la Mwanahalisi kutokana na Dk. Steven Ulimboka kuweka wazi ofisa usalama wa taifa anayedaiwa kuhusika na kutekwa kwake.

Alisema sababu walizotumia viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kulifungia gazeti la hilo sio za kweli akidai kilichoandikwa na gazeti hilo kilikuwa ni ukweli ambao umethibitishwa na Dk. Ulimboka.

“Dk. Ulimboka kupitia wakili wake aliweka wazi kwamba Ofisa wa Usalama wa Taifa alihusika katika kutekwa kwake na kwamba ofisa huyo ni mdau mkubwa wa tukio hilo… tunasikitika kwamba hadi leo jeshi la polisi na serikali hawajachukua hatua yoyote ya kisheria kwa ofisa huyo na washirika wake” alisema Albani.

Alisema wadau mbalimbali walitegemea kusikia serikali inatoa tamko kwamba imepata uhakika kuhusu ofisa wake kukiuka maadili ya ajira yake na ingetangaza inachukua hatua gani za kisheria dhidi yake kwa kuhusika katika mak
osa ya jinai.

:: IPPMEDIA





CHANZO: NIPASHE
''Mheshimiwa Mkuu wa nchi Rais wetu J.K. Hebu liachie hili gazete wasamehe wahusika kwa heshima yako mkuu Rais wetu Mtukufu''.Mzizimkavu
 
Nikikumbuka kuhusu mwanahalisi kufungiwa kwa sababu za kijinga km hizo huwa nalia mpaka basi
tatizo lao hawatoi habari za uhakika na makini kama vyombo vingine vya habari kama habari leo,uhuru na redio imaan
 
Inchi ishauzwa hii. Na wakilifungulia tu ile ishu ya china lazima iwe hewani. Kubenea sio mropokaji.
 
Serikali haijui kuwa kwa kufungia gazeti kipenzi cha wengi inaendelea kujijengea chuki na wananchi/wapigakura/waajiri wa serikali yenyewe. Mwaka 2015 itavuna inachopanda sasa hivi
 
tatizo lao hawatoi habari za uhakika na makini kama vyombo vingine vya habari kama habari leo,uhuru na redio imaan

Wee ndo kilaza kweli!! Wakati dunia inasonga mbele wewe uko speed ya 200pkm kurudi nyuma.
 
Mwanahalisi msijali, hiyo ndio stail ya utawala wa serikali za kishetani, lakini menemene tekeli na peresi.

Nakuunga mkono mkuu. Kweli mene,mene tekeli na peresi, Danieli 5:25- 28. Wenye kutambua majira na nyakati wanaelewa kinachoendelea. Mwisho wa waovu katika nchi hii umekaribia
 
Hivi hawa jamaa wa Mwanahalisi wana mpango gani mbona wamekuwa kimya sana? Kwanini wasifungue gazeti lingine angalau kwa muda huu?
 
[COLOR=#343434 said:
Alisema sababu walizotumia [/COLOR]viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kulifungia gazeti la hilo sio za kweli akidai kilichoandikwa na gazeti hilo kilikuwa ni ukweli ambao umethibitishwa na Dk. Ulimboka.

Poleni akina kubenea, kwasasa hatuna viongozi mkuu....Tuna akina MULUGO ambao wanaanza kuandika historia mpya ya Africa. Msitegemee viongozi kama hao wakawa na sababu zenye busara na tija kwa jamii.
 
Nakuunga mkono mkuu. Kweli mene,mene tekeli na peresi, Danieli 5:25- 28. Wenye kutambua majira na nyakati wanaelewa kinachoendelea. Mwisho wa waovu katika nchi hii umekaribia
Wewe nii mtabiri? SISIEM haiwezi kushindwa milele,labda mtafute mbinu nyingine!
 
Hivi Ulimbuko bado yupo? anajishughulisha na nini siku hizi? kutibu au bado anaendeleza majungu?
 
Back
Top Bottom