Serikali yasema hakuna upigaji NIC

Apr 4, 2020
16
7
1586166224998.png


SERIKALI imesema hakuna ubadhirifu wowote unaoendelea katika Shirika la Bima la Taifa (NIC) na shirika limeendelea kuboresha mifumo yake ya udhibiti wa mapato na matumizi,ili kukabiliana na washindani wake kibiashara katika sekta ya bima.

Hayo yalibainishwa na jana bungeni jijini hapa na Wizara ya Fedha na Mipango ilipojibu swali la Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), aliyetaka kujua ukweli wa taarifa kwamba ubadhirifu bado unaendelea katika shirika hilo na halina mipango thabiti ya kukabiliana na washindani wake kibiashara.

Katika majibu yake, wizara hiyo ilisema kuwa, katika kujiimarisha kibiashara, shirika limechukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mapato yote yanakusanywa kwa kutumia Mfumo wa Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali (GePG), ulioanza kutumiwa na shirika Novemba mwaka jana na kuondoa ukusanyaji wa mapato kwa fedha taslimu Ilisema hatua nyingine zinazochukuliwa ni kuongeza udhibiti katika ulipaji wa madai na kufanya ukaguzi maalum wa madai yote ya Bima za Maisha ili kujiridhisha juu ya uhalali wa madai hayo.

"Shirika lipo katika hatua za mwisho za kuunganishwa na Mfumo wa Usimamizi wa Shughuli za Kihasibu na Malipo katika Taasisi za Umma (Muse) ambao utaongeza udhibiti katika malipo yote yanayofanyika, kusitisha matumizi ya hundi ambapo kuanzia Desemba 2019, shirika lilisitisha matumizi ya hundi katika malipo yake yote na kuanza kutumia mfumo wa malipo wa kielektroniki, hivyo kuongeza uthibiti wa matumizi na kuzuia uwezekano wa matumizi ya hundi feki," ilisema.

Wizara hiyo iliongeza kuwa serikali pia imechukua hatua mbalimbali kuliimarisha shirika hilo kitaalamu kwa kuliondoa kwenye mashirika yaliyotakiwa kubinafsishwa na kuliwezesha kushiriki katika biashara ya bima kwa ushindani pamoja na kulifanyia mabadiliko ya kiuongozi ili kuongeza tija na kuleta mabadiliko chanya kwenye utendaji na usimamizi wa shughuli zake. Ilisema hatua zingine zilizochukuliwa ni kulisaidia shirika kwa kulipatia wataalamu mbalimbali katika nyanja za mifumo ya Tehama, utendaji kazi na utunzaji kumbukumbu (e-office) ili kuongeza ufanisi wa shirika na kukabiliana na ushindani wa kibiashara.

"Serikali pia imeliimarisha shirika kifedha kwa kuchukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kupata biashara za serikali na kushinikiza malipo ya hapo kwa hapo ya premium ambayo yamesaidia kupunguza malimbikizo ya premium kutoka kwa taasisi za serikali kutoka zaidi ya Sh. bilioni 20 hadi milioni 500 kwa kipindi cha Julai 2019 hadi Februari 2020," wizara hiyo ilibainisha.

Ilisema pamoja na maendeleo mazuri ya shirika, serikali inaendelea kuliimarisha shirika hilo la kimkakati kwa kulisaidia katika kupitia upya mpango mkakati wake ili uendane na mahitaji halisi ya biashara ya ushindani, kuongeza uwekezaji katika mifumo ya Tehama kwa lengo la kuwafikia wateja wengi zaidi, kuongeza ubora wa huduma zake na kulipa madai haraka na kwa urahisi, kujitangaza zaidi na kuongeza uwekezaji wenye tija ili kutoa gawio kubwa kwa serikali na kushiriki katika shughuli za maendeleo ya taifa.
 
NIC/BIMA Hao kuwadhibiti ni kuwaweka sawa wakurugenzi waliojiundia mashirika yao huku wakifanya uharibifu wa shirika la Taifa. Watiwe kibano tu!
 
Ukiachana na Tanesco, hili lilitakiwa kua shirika la pili kwa kuingiza profit kubwa ndani ya nchi. Shirika limetajirisha wengi kwa ufisadi. Pamoja na favour ya taasisi nyingine za serikali kama Tanesco,Udart,nk kufanya biashara na shirika hili kizalendo bado mwishoni mwa mwaka linazidiwa faida na private insurance company kama alliance. Hii ina maanisha huku mtaani Wana kasi ndogo kwenye biashara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiachana na Tanesco, hili lilitakiwa kua shirika la pili kwa kuingiza profit kubwa ndani ya nchi. Shirika limetajirisha wengi kwa ufisadi. Pamoja na favour ya taasisi nyingine za serikali kama Tanesco,Udart,nk kufanya biashara na shirika hili kizalendo bado mwishoni mwa mwaka linazidiwa faida na private insurance company kama alliance. Hii ina maanisha huku mtaani Wana kasi ndogo kwenye biashara.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo ilikuwa ulegevu wa serikali. Kuna wakurugenzi ndani ya shirika, waliamua kuunda kampuni zao au kuwa na shares bubu ktk makampuni ya binafsi. Ni kama uzembe ulioruhusu Mramba kuwa waziri wa uchukuzi wakati akiwa na shares shirika la ndege la binafsi.
 
Back
Top Bottom