Serikali yarejesha misamaha ya kodi kwa taasisi za dini, yatoa masharti mazito

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Serikali imelegeza msimamo wake kuhusu kuondoa misamaha ya kodi kwenye Taasisi za dini badala yake itaongeza udhibiti ili kuzuia mianya ya matumizi mabaya ya misamaha hiyo.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ametoa ufafanuzi huo mjini Dodoma wakati akiongea na vyombo vya habari ili kutoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili bajeti Kuu ya Serikali iliyopitishwa Juzi na Bunge.

Amesema kuwa uamuzi huo wa serikali umefuatia maombi na mapendekezo mbalimbali ya wadau yaliyoitaka serikali iendelee kutoa misamaha ya kodi kwa Taasisi hizo kutokana na umuhimu wake wa kuisaidia jamii kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na taasisi hizo.

"Kwa kutambua mchango mkubwa wa taasisi mbalimbali za kidini katika utoaji wa huduma za elimu, afya, maji; nimeamua kufuta utaratibu nilioutangaza katika hotuba ya bajeti, badala yake serikali itaimarisha zaidi udhibiti wa misamaha hiyo"Alisema Dkt. Mpango

Alizitaja baadhi ya hatua zitakazochukuliwa kuzuia mianya ya matumizi mabaya ya misamaha hiyo kuwa ni kuzitaka Taasisi za dini kuwasilisha orodha ya vifaa vinavyotarajiwa kununuliwa kutoka nje ya nchi kila mwanzo wa mwaka wa kalenda, pamoja na kuthibitisha kama vifaa vilivyosamehewa kodi mwaka uliotangulia vilitumika kwa mujibu wa sheria

Aidha, utaratibu mpya utazitaka Taasisi hizo za dini kuwasilisha majina ya watu waliowaidhinisha kuandika barua za maombi ya msamaha wa kodi zikiainisha cheo, saini, picha, anuani na namba za simu za wahusika.

"Taarifa hizo ni muhimu katika kuiwezesha TRA kufuatilia bidhaa zilizoombewa na kupewa misamaha kama zimepata kibali cha Taasisi husika zimetumika na zimetekeleza miradi iliyokusudiwa" Aliongeza Dkt. Mpango

Dkt. Mpango alisema katika utaratibu huo mpya, wameweka masharti ya kuzilazimisha Taasisi hizo za dini kuiandikia serikali barua ya kumuidhinisha wakala wa forodha waliyemteua kutoa bandarini mizigo itakayokuwa ikiagizwa kutoka nje

Alizitaja hatua nyingine kuwa ni wakati wa kuomba msamaha wa kodi katika bidhaa zinazoingizwa nchini, Taasisi za dini zitalazimika kupata barua ya uthibitisho kutoka kwa Afisa Mtendaji wa serikali ya Mtaa ama kijiji na mkuu wa wilaya mahali Taasisi au Mradi ulipo ili kuthibitisha uwepo wa Taasisi au mradi na mahitaji ya vifaa vinavyoombewa msamaha

Dkt. Mpango alifafanua kuwa magari yatakayoingizwa kwa msamaha wa kodi yatalazimika kuwa na rangi pamoja na namba maalumu za utambuzi mfano TEV 222 AXZ kama njia ya kudhibiti matumizi yake.

Alionya kuwa Taasisi ya dini itakayothibitika kutumia vibaya msamaha wa kodi itafutiwa usajili wake.

Dk Mpango atoa masharti mapya kwa taasisi za dini.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip mpango amesema amefuta utaratibu alioupendekeza bungeni wa taasisi za dini kulazimika kulipa kodi kwanza kwa bidhaa watakazonunua au kuagiza nje na kodi hiyo kurejeshwa baada ya ukaguzi.

Anasema alisema hivyo kwasababu baadhi ya Taasisi za kidini hufanya sivyo ndivyo, sio waaminifu.

========

Serikali imelegeza msimamo wake kuhusu kuondoa misamaha ya kodi kwenye Taasisi za dini badala yake itaongeza udhibiti ili kuzuia mianya ya matumizi mabaya ya misamaha hiyo.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ametoa ufafanuzi huo mjini Dodoma wakati akiongea na vyombo vya habari ili kutoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili bajeti Kuu ya Serikali iliyopitishwa Juzi na Bunge.

Amesema kuwa uamuzi huo wa serikali umefuatia maombi na mapendekezo mbalimbali ya wadau yaliyoitaka serikali iendelee kutoa misamaha ya kodi kwa Taasisi hizo kutokana na umuhimu wake wa kuisaidia jamii kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na taasisi hizo.

“Kwa kutambua mchango mkubwa wa taasisi mbalimbali za kidini katika utoaji wa huduma za elimu, afya, maji; nimeamua kufuta utaratibu nilioutangaza katika hotuba ya bajeti, badala yake serikali itaimarisha zaidi udhibiti wa misamaha hiyo”Alisema Dkt. Mpango

Alizitaja baadhi ya hatua zitakazochukuliwa kuzuia mianya ya matumizi mabaya ya misamaha hiyo kuwa ni kuzitaka Taasisi za dini kuwasilisha orodha ya vifaa vinavyotarajiwa kununuliwa kutoka nje ya nchi kila mwanzo wa mwaka wa kalenda, pamoja na kuthibitisha kama vifaa vilivyosamehewa kodi mwaka uliotangulia vilitumika kwa mujibu wa sheria

Aidha, utaratibu mpya utazitaka Taasisi hizo za dini kuwasilisha majina ya watu waliowaidhinisha kuandika barua za maombi ya msamaha wa kodi zikiainisha cheo, saini, picha, anuani na namba za simu za wahusika.

“Taarifa hizo ni muhimu katika kuiwezesha TRA kufuatilia bidhaa zilizoombewa na kupewa misamaha kama zimepata kibali cha Taasisi husika zimetumika na zimetekeleza miradi iliyokusudiwa” Aliongeza Dkt. Mpango

Dkt. Mpango alisema katika utaratibu huo mpya, wameweka masharti ya kuzilazimisha Taasisi hizo za dini kuiandikia serikali barua ya kumuidhinisha wakala wa forodha waliyemteua kutoa bandarini mizigo itakayokuwa ikiagizwa kutoka nje

Alizitaja hatua nyingine kuwa ni wakati wa kuomba msamaha wa kodi katika bidhaa zinazoingizwa nchini, Taasisi za dini zitalazimika kupata barua ya uthibitisho kutoka kwa Afisa Mtendaji wa serikali ya Mtaa ama kijiji na mkuu wa wilaya mahali Taasisi au Mradi ulipo ili kuthibitisha uwepo wa Taasisi au mradi na mahitaji ya vifaa vinavyoombewa msamaha

Dkt. Mpango alifafanua kuwa magari yatakayoingizwa kwa msamaha wa kodi yatalazimika kuwa na rangi pamoja na namba maalumu za utambuzi mfano TEV 222 AXZ kama njia ya kudhibiti matumizi yake.

Alionya kuwa Taasisi ya dini itakayothibitika kutumia vibaya msamaha wa kodi itafutiwa usajili wake.

Chanzo: Mpekuzi
 
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Serikali imelegeza msimamo wake kuhusu kuondoa misamaha ya kodi kwenye Taasisi za dini badala yake itaongeza udhibiti ili kuzuia mianya ya matumizi mabaya ya misamaha hiyo.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ametoa ufafanuzi huo mjini Dodoma wakati akiongea na vyombo vya habari ili kutoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili bajeti Kuu ya Serikali iliyopitishwa Juzi na Bunge.

Amesema kuwa uamuzi huo wa serikali umefuatia maombi na mapendekezo mbalimbali ya wadau yaliyoitaka serikali iendelee kutoa misamaha ya kodi kwa Taasisi hizo kutokana na umuhimu wake wa kuisaidia jamii kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na taasisi hizo.

"Kwa kutambua mchango mkubwa wa taasisi mbalimbali za kidini katika utoaji wa huduma za elimu, afya, maji; nimeamua kufuta utaratibu nilioutangaza katika hotuba ya bajeti, badala yake serikali itaimarisha zaidi udhibiti wa misamaha hiyo"Alisema Dkt. Mpango

Alizitaja baadhi ya hatua zitakazochukuliwa kuzuia mianya ya matumizi mabaya ya misamaha hiyo kuwa ni kuzitaka Taasisi za dini kuwasilisha orodha ya vifaa vinavyotarajiwa kununuliwa kutoka nje ya nchi kila mwanzo wa mwaka wa kalenda, pamoja na kuthibitisha kama vifaa vilivyosamehewa kodi mwaka uliotangulia vilitumika kwa mujibu wa sheria

Aidha, utaratibu mpya utazitaka Taasisi hizo za dini kuwasilisha majina ya watu waliowaidhinisha kuandika barua za maombi ya msamaha wa kodi zikiainisha cheo, saini, picha, anuani na namba za simu za wahusika.

"Taarifa hizo ni muhimu katika kuiwezesha TRA kufuatilia bidhaa zilizoombewa na kupewa misamaha kama zimepata kibali cha Taasisi husika zimetumika na zimetekeleza miradi iliyokusudiwa" Aliongeza Dkt. Mpango

Dkt. Mpango alisema katika utaratibu huo mpya, wameweka masharti ya kuzilazimisha Taasisi hizo za dini kuiandikia serikali barua ya kumuidhinisha wakala wa forodha waliyemteua kutoa bandarini mizigo itakayokuwa ikiagizwa kutoka nje

Alizitaja hatua nyingine kuwa ni wakati wa kuomba msamaha wa kodi katika bidhaa zinazoingizwa nchini, Taasisi za dini zitalazimika kupata barua ya uthibitisho kutoka kwa Afisa Mtendaji wa serikali ya Mtaa ama kijiji na mkuu wa wilaya mahali Taasisi au Mradi ulipo ili kuthibitisha uwepo wa Taasisi au mradi na mahitaji ya vifaa vinavyoombewa msamaha

Dkt. Mpango alifafanua kuwa magari yatakayoingizwa kwa msamaha wa kodi yatalazimika kuwa na rangi pamoja na namba maalumu za utambuzi mfano TEV 222 AXZ kama njia ya kudhibiti matumizi yake.

Alionya kuwa Taasisi ya dini itakayothibitika kutumia vibaya msamaha wa kodi itafutiwa usajili wake.
yes..kuna wababaishaji wameanzisha makanisa na taasisi za kidini ili kufanya biashara ya kuuza misamaha ya kodi wanayopewa na serikali. ni biashara kubwa hadi wengine wananunua helicopter zao na ndege za ainaaina. wengine wanatajirika hadi kua na kiburi kudharau mamlaka ya taifa.
 
Hapo wote tutakula kwa kutumia Mkono moja sio Wachache wale na mikono Miwili!
 
Picha,makaratasi,mwenyekiti serikali ya mtaa,bomoa bomoa kila chenye uhai nacho hufariki!
 
Huu ni udhaifu mkubwa kwa upande wa serikali na uthibitisho tosha kuwa haijiamini na haiko makini katika suala la kodi. Utaratibu aliotangaza waziri utaongeza urasimu, una gharama kubwa kutekeleza na hauna tija yoyote. Mpango amerudia kigugumizi kile kile kilichoonyeshwa na Mustafa Mkulo wakati akiwa waziri wa fedha kuhusiana na misamaha ya kodi kwa taasisi za kidini. Kimsingi, kwa vile taasisi za kidini pia zinanufaika na huduma zinazotolewa na serikali, zinapaswa kulipa kodi kikamilifu. Kodi siyo adhabu. Mfano, Biblia inasema: "Mpe Kaisari kilicho chake". ("Kaisari" hapa inamaanisha mtawala mwenye dola au serikali na "kilicho chake" ni kodi). Hiki kinachoitwa "misamaha ya kodi" ni aina tu ya ufisadi wa kitaasisi na hakipaswi kabisa kuwepo katika msamiati wa masuala ya kodi nchini. Badala ya kutoa misamaha ya kodi, serikali inaweza kutoa ruzuku pale inapostahili.
 
Ni jambo la kumshukuru sana Mungu kwa kuwa amewafunulia hao watendaji wa serikali kutambua sensitivity ya taasisi za dini.

Ilichokuwa inataka kufanya serikali yetu kwa kufuta misamaha ya kodi kwa taasisi zote za dini ilikuwa sawasawa na kujitafutia laana...........
 
Dini zina mashule yagharama Kweli na zimejificha mgongoni mwa pilato kukwepa kodi ya kaisari!!!!!!!! TOZEN KODI task so za dini zina mabenki ya Escrow zinatakatisha fedha ZITOZWE KODI TU!!!!!!
 
Serikali imelegeza msimamo wake kuhusu kuondoa misamaha ya kodi kwenye Taasisi za dini badala yake itaongeza udhibiti ili kuzuia mianya ya matumizi mabaya ya misamaha hiyo.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ametoa ufafanuzi huo mjini Dodoma wakati akiongea na vyombo vya habari ili kutoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili bajeti Kuu ya Serikali iliyopitishwa Juzi na Bunge.

Amesema kuwa uamuzi huo wa serikali umefuatia maombi na mapendekezo mbalimbali ya wadau yaliyoitaka serikali iendelee kutoa misamaha ya kodi kwa Taasisi hizo kutokana na umuhimu wake wa kuisaidia jamii kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na taasisi hizo.

“Kwa kutambua mchango mkubwa wa taasisi mbalimbali za kidini katika utoaji wa huduma za elimu, afya, maji; nimeamua kufuta utaratibu nilioutangaza katika hotuba ya bajeti, badala yake serikali itaimarisha zaidi udhibiti wa misamaha hiyo”Alisema Dkt. Mpango

Alizitaja baadhi ya hatua zitakazochukuliwa kuzuia mianya ya matumizi mabaya ya misamaha hiyo kuwa ni kuzitaka Taasisi za dini kuwasilisha orodha ya vifaa vinavyotarajiwa kununuliwa kutoka nje ya nchi kila mwanzo wa mwaka wa kalenda, pamoja na kuthibitisha kama vifaa vilivyosamehewa kodi mwaka uliotangulia vilitumika kwa mujibu wa sheria

Aidha, utaratibu mpya utazitaka Taasisi hizo za dini kuwasilisha majina ya watu waliowaidhinisha kuandika barua za maombi ya msamaha wa kodi zikiainisha cheo, saini, picha, anuani na namba za simu za wahusika.

“Taarifa hizo ni muhimu katika kuiwezesha TRA kufuatilia bidhaa zilizoombewa na kupewa misamaha kama zimepata kibali cha Taasisi husika zimetumika na zimetekeleza miradi iliyokusudiwa” Aliongeza Dkt. Mpango

Dkt. Mpango alisema katika utaratibu huo mpya, wameweka masharti ya kuzilazimisha Taasisi hizo za dini kuiandikia serikali barua ya kumuidhinisha wakala wa forodha waliyemteua kutoa bandarini mizigo itakayokuwa ikiagizwa kutoka nje

Alizitaja hatua nyingine kuwa ni wakati wa kuomba msamaha wa kodi katika bidhaa zinazoingizwa nchini, Taasisi za dini zitalazimika kupata barua ya uthibitisho kutoka kwa Afisa Mtendaji wa serikali ya Mtaa ama kijiji na mkuu wa wilaya mahali Taasisi au Mradi ulipo ili kuthibitisha uwepo wa Taasisi au mradi na mahitaji ya vifaa vinavyoombewa msamaha

Dkt. Mpango alifafanua kuwa magari yatakayoingizwa kwa msamaha wa kodi yatalazimika kuwa na rangi pamoja na namba maalumu za utambuzi mfano TEV 222 AXZ kama njia ya kudhibiti matumizi yake.

Alionya kuwa Taasisi ya dini itakayothibitika kutumia vibaya msamaha wa kodi itafutiwa usajili wake.
 
Taasisi za dini zina shughuli za kibiashara, mfano shule zao na Hospitali zina gharama kubwa kuliko hata za watu binafsi.
Magari yatawekewa namba maalum, sawa, Je, bidhaa nyingine zitajulikanaje?. kimsingi ni kwamba Serikali imeufyatua ama kuufyata kwa viongozi wa Dini.
wanatupiga sana hawa jamaa, waumini hawanufaiki hata kidogo na misamaha hii. anayebisha anipe mfano na mimi nitakuja na mifano kadhaa.
 
Serikali isiyo na dira Siku zote Inakurupuka kwa Matamko. Alikuwa wapi kuleta mswaada wa sheria bungeni, unaofuta sheria ya mwanzo iliyoondoa misamaha ya kodi kwa Taasisi na mashirika ya dini?
 
Serikali imelegeza msimamo wake kuhusu kuondoa misamaha ya kodi kwenye Taasisi za dini badala yake itaongeza udhibiti ili kuzuia mianya ya matumizi mabaya ya misamaha hiyo.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ametoa ufafanuzi huo mjini Dodoma wakati akiongea na vyombo vya habari ili kutoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili bajeti Kuu ya Serikali iliyopitishwa Juzi na Bunge.

Amesema kuwa uamuzi huo wa serikali umefuatia maombi na mapendekezo mbalimbali ya wadau yaliyoitaka serikali iendelee kutoa misamaha ya kodi kwa Taasisi hizo kutokana na umuhimu wake wa kuisaidia jamii kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na taasisi hizo.

“Kwa kutambua mchango mkubwa wa taasisi mbalimbali za kidini katika utoaji wa huduma za elimu, afya, maji; nimeamua kufuta utaratibu nilioutangaza katika hotuba ya bajeti, badala yake serikali itaimarisha zaidi udhibiti wa misamaha hiyo”Alisema Dkt. Mpango

Alizitaja baadhi ya hatua zitakazochukuliwa kuzuia mianya ya matumizi mabaya ya misamaha hiyo kuwa ni kuzitaka Taasisi za dini kuwasilisha orodha ya vifaa vinavyotarajiwa kununuliwa kutoka nje ya nchi kila mwanzo wa mwaka wa kalenda, pamoja na kuthibitisha kama vifaa vilivyosamehewa kodi mwaka uliotangulia vilitumika kwa mujibu wa sheria

Aidha, utaratibu mpya utazitaka Taasisi hizo za dini kuwasilisha majina ya watu waliowaidhinisha kuandika barua za maombi ya msamaha wa kodi zikiainisha cheo, saini, picha, anuani na namba za simu za wahusika.

“Taarifa hizo ni muhimu katika kuiwezesha TRA kufuatilia bidhaa zilizoombewa na kupewa misamaha kama zimepata kibali cha Taasisi husika zimetumika na zimetekeleza miradi iliyokusudiwa” Aliongeza Dkt. Mpango

Dkt. Mpango alisema katika utaratibu huo mpya, wameweka masharti ya kuzilazimisha Taasisi hizo za dini kuiandikia serikali barua ya kumuidhinisha wakala wa forodha waliyemteua kutoa bandarini mizigo itakayokuwa ikiagizwa kutoka nje

Alizitaja hatua nyingine kuwa ni wakati wa kuomba msamaha wa kodi katika bidhaa zinazoingizwa nchini, Taasisi za dini zitalazimika kupata barua ya uthibitisho kutoka kwa Afisa Mtendaji wa serikali ya Mtaa ama kijiji na mkuu wa wilaya mahali Taasisi au Mradi ulipo ili kuthibitisha uwepo wa Taasisi au mradi na mahitaji ya vifaa vinavyoombewa msamaha

Dkt. Mpango alifafanua kuwa magari yatakayoingizwa kwa msamaha wa kodi yatalazimika kuwa na rangi pamoja na namba maalumu za utambuzi mfano TEV 222 AXZ kama njia ya kudhibiti matumizi yake.

Alionya kuwa Taasisi ya dini itakayothibitika kutumia vibaya msamaha wa kodi itafutiwa usajili wake.
Vipi kuhusu NGO?
 
  • Thanks
Reactions: ram
Haikutakiwa kurudi nyuma kwa uamuzi ule. Maana yake ni kwamba misamaha ya kodi itaendelea kuwa mwanya wa kukwepa kodi.
 
Naungana na Serikali; misamaha inatakiwa kudhibitiwa sana. Kama mnakumbuka kuna taasisi moja ilidaiwa kuingiza semitrela za kutosha kupitia hii kitu inayoitwa misamaha.
 
Back
Top Bottom