Serikali yapoteza bilioni 33 kila mwezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yapoteza bilioni 33 kila mwezi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 31, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,229
  Likes Received: 4,022
  Trophy Points: 280
  SERIKALI inapoteza Sh bilioni 33 kila mwezi kutokana na uchanganyaji wa mafuta ya taa na dizeli unaofanywa na madereva wa malori ya mizigo nchini.

  Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Chama cha Wamiliki wa Malori ya Kusafirishia Mizigo (TATOA), Zacharia Poppe wakati akizungumza katika Kamati ya Bunge ya Miundombinu.

  Alisema kiwango cha mafuta ya taa kinachochanganywa katika mafuta ya dizeli ni kikubwa na kinapunguza kiwango cha mafuta hayo kuingizwa nchini.

  “Mafuta ya taa hayana kodi, na kutokana na kutumika kuchanganywa katika dizeli kunasababisha kupotea kwa fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kwa miradi mingine ya maendeleo,” alisema Poppe.

  Alisema hivi karibuni malori 88 ya dizeli yaliyokuwa yakitokea Tanzania yalikamatwa nchini Burundi kutokana na kuchanganywa na mafuta ya taa, hali ambayo imefikia hatua ya kuiomba serikali kutoza kodi kwa mafuta ya taa au kuuzwa kwa bei kubwa ili kupunguza vitendo hivyo.

  “Jambo la ajabu pindi dereva anapokamatwa akiwa amechanganya mafuta ya taa kwenye dizeli yeye hakamatwi ila lawama zinamwangukia mmiliki wa gari, kwa nini asishtakiwe kwa kuwa yeye ndio mwizi?” Alihoji Poppe.

  Alisema endapo biashara ya dizeli itaanguka ni hasara pia kwa serikali kwa kuwa itakosa mapato huku vipuri vya magari vikiharibika ovyo.

  Kuhusu ajali za barabarani, Mkurugenzi wa Mipango kutoka wakala wa ujenzi wa barabara Tanroads, Johnson Rwiza alisema ipo haja kwa mamlaka zinazohusika kuwachunguza na kuwachuja madereva mienendo na tabia zao kabla ya kupewa leseni hali ambayo inaweza kupunguza ajali.

  Akichangia mada kuhusu ajali, Mbunge wa Rorya, Philemon Sarungi alisema ipo haja kwa mamlaka zinazohusika kuwapima akili madereva kabla ya kupatiwa leseni ili kujua ukamilifu wa afya zao.

  Alishauri kazi hiyo iende pamoja na kuwashirikisha madaktari ili kuwapima ugonjwa wa kisukari, akili, shinikizo la damu na kwa wale ambao akili zao sio nzuri, wafanyiwe mtihani baada ya miaka mitatu kwa ajili kupimwa zaidi. annet
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,229
  Likes Received: 4,022
  Trophy Points: 280
  Kweli Serikali ilikuwa na nia nzuri kuondoa kodi kwenye mafuta ya Taa lakini wafanyabiashara wachache wenye tamaa wanachanganya mafuta hayo ktk diesel na petrol ni wizi na ufisadi. Ni bora Serikali ilipishe kodi na bei zote ziwe moja,ingawa bei wanayonunulia hazilingani lakini wakae wataalam wa mahesabu wachanganye bei zote tatu halafu bei ipangwe moja tu,hii kuweka rangi wala si dawa.


  Au Serikali iwape fani kubwa madereva pamoja na wenye gari maana ndio wahusika wakubwa sio kutafuta njia rahisi kwa sababu serikali ikipandisha bei ya mafuta ya taa ni watu wa hali ya chini na wanaotumia mafuta ya taa kwa ajili ya umeme hambao ni asilimia 60% na ni matajiri wachache wanaofanya kazi kwa nini serikali ishifanye uchunguzi au polisi ili wakamatuwe kuliko kupandisha bei ....jibu unalo ..
   
Loading...