Serikali yapiga ‘stop’ Shule binafsi kupandisha Ada

Serikali yapiga ‘stop’ Shule binafsi kupandisha Ada

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,813
Reaction score
63,268
Serikali imezipiga marufuku shule zote binafsi za msingi na sekondari kuongeza kiwango cha ada katika mwaka huu wa masomo na kuzitaka shule zote zilizopandisha ada kinyume cha tamko la serikali kusitisha mara moja ongezeko hilo.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ithibati ya Shule, Hadija Mcheka amesema kuwa kufuatia tangazo la serikali la kuzitaka shule binafsi zinazotaka kupandisha ada kuwasilisha maombi yao kwa Kamishna wa Elimu, shule 45 pekee ndizo zilizowasilisha maombi hayo lakini sababu ilizotoa hazikuwa na mashiko.

Alisema kuwa shule nyingine 900 ziliwasilisha maombi ya kuendelea na kiwango cha ada ilichokuwa ikitoza mwaka jana.

Mcheka alieleza kuwa kati ya sababu zilizotolewa na wamiliki wa shule hizo ni pamoja na kuongeza majengo na kuajiri walimu kutoka nje, sababu ambazo Kamishna wa Elimu aliona hazina mashiko kwa kuwa hazimhusu mzazi.

“Mwingine anasema anataka kupandisha ada kwa vile anataka kuajiri walimu kutoka nje ya nchi, hili nalo halimhusu mzazi ndio maana tumewanyima kibali cha kupandisha ada. Sababu zote hizi hazikumridhisha kamishna ndio maana tumewataka watii agizo la Serikali hadi hapo baadaye,” alisema Mcheka.

Akieleza kuhusu mpango wa kuweka ada elekezi, Mcheka alisema kuwa serikali imemuajiri mtaalam mwelekezi atakayefanya kazi ya kubaini gharama za kumsomesha kila mtoto ili kuisaidia serikali kupanga ada elekezi.


Chanzo: Dar24Blog
 
CHA MSINGI SERIKALI IRUDISHE SIFA ZA SHULE ZAKE ILI WATU WA-OPT ZA GOVERNMENT. SHULE KAMA ILIBORU, MZUMBE N.K SASA ZIMEKUWA CHOKA MBAYA ILI HALI NDO ZILIKUWA VINARA
 
Mmeuwa skuli za umma tukakimbilia private sasa mnataka mziuwe hata hizi private schools za hapa bongo ili sisi tukose pakukimbilia alafu nyie watoto wenu muwapeleke nje ya nchi.
 
Hili la michango nalo linagaliwe vizuri kwa sababu wengine hawatapandisha ada ila watachomeka michango kibao ili kufidia. Kuna shule moja iko maeneo ya Goba, wao hawajapandisha ada this time ila wame-introduce michango ya majengo 300,000/=. Uhuni huu ni muhimu ukatafutiwa dawa.
 
Hii nchi matamko yamekuwa mengi mno. Miluzi mingi humpoteza mbwa.
Yaani shule zimeshafunguliwa, ada zimesha pandishwa ndipo wao wanakuja na zuio?? Mbona hatuko serious na mipango yetu jamani??
Mimi nilimlipia mtoto wangu ada ya zamani nilipo peleka risiti ya malipo nikaambiwa wameongeza 40,000/ juu ya ada ya mwaka jana. So natakiwa kuongeza malipo. Tutakuwa na kiburi gani cha kutokulipa hilo ongezeko?? Mtoto atarudishwa shule.

Tunaomba wizara isambaze hili zuio kwa shule zote na libandikwe mlangoni.
Maafisa elemu wafuatilie hili.
 
Kuna watendaji wa serikali akili zao ni ndogo sana, hili swala walilizungumza na hawakufatilia utekelezaji wake kuona kama limetekelezwa au la, ada zimepandishwa na wamiliki wa mashule haya hawana wasiwasi kabisa kwani wanajua hawa watendaji wanachojua ni kutoa matamko tu utekelezaji ni sifuri, tuna safar ndefu sana ubunifu ni zero kwa watendaji wetu, liko wapi swala la wahamiaji haramu na wanaofanya kazi bila vibali halali? wapo mtaani wanaicheka serikali yetu ya kukurupuka.
Ada elekezi hamtaliweza kamwe achaneni nalo tu hangaikieni tu la kwenu la elimu bure.
 
Hili la michango nalo linagaliwe vizuri kwa sababu wengine hawatapandisha ada ila watachomeka michango kibao ili kufidia. Kuna shule moja iko maeneo ya Goba, wao hawajapandisha ada this time ila wame-introduce michango ya majengo 300,000/=. Uhuni huu ni muhimu ukatafutiwa dawa.



Sasa hapo majengo yanamuhusu nini mzazi wakati shule ni mtu binafsi? Kwahyo wazazi wanamjengea shule mmiliki wa shule? Huu unyonyaji mkubwa sana.
 
kabla hatujawa na shule binafsi serikali ilikuwa inapoteza hela nyingi sana kwani.wazazi walikuwa wanapeleka watoto wao nje ya nchi kusoma.mfano katika nchi za Kenya,Uganda,South Africa etc.hata fursa za ajira zilikuwa finyu, ilikuwa mwalimu lazima ufundishe shule za serikali.
madhala ya kupanga ada elekezi hii sector wakati shule za serikali hazina viwango bora wananchi watasita kuwekeza na kutoa huduma bora na nchi kuendelea kupoteza fedha za kigeni kwa wazazi watakao amua wapeleke watoto wao nje ya nchi baada ya elimu ya serikalini na binasfi kuwa mbaya.
 
ni aibu serekali inashindwa kuendesha shule zake sasa inaingilia shule binafsi. asilimia kubwa ya wanaosomesha watoto zao private ni watu wa kipato cha kati yaani hawana uwezo wa kuwasomesha watoto nje ya nchi sasa mkiziuwa hizi private school mzigo wa kuwasomesha hawa watoto utakuwa kwa serekali...
 
Nahisi hii vita ni ya kumkomoa LOWASA matokeo wanaathiri jamii nzima.hii serikali isipojirekebisha italeta umaskini wa kutupwa badala ya neema kwa wananchi.
 
Mmh BOB LUSE YA LOWASA YAMETOKA WAPI?KWANI LOWASA NDO MMILIKI WA SHULE ZA PRIVATE?HAPO UMETEREZA KWA UPANDE WANGU NAONA KAMA HOJA YAKO HAIJAKA VIZURI
 
yani kamishna akijisikia anakubaliana na sababu au hakubali!!!!nilidhani muongozo/sheria/kanuni ndio zinamuongoza!!hatari hii.
 
Yaani hapa dawa ni moja narahisi sana....

Serikali kuboresha shule zake....

Hadhi ya shule za serikali ikirudi hao private watashusha bei wenyewe
 
Kwa hiyo mimi ambaye nimeshalipa ongezeko la ada nikadai chenchi?
 
Back
Top Bottom