Iliboru si ipo top 20 best schools au?uchoka mbaya upi unaongelea tueleweshane kuna ndugu yangu nataka kumfanyia mpango aende huko alifaulu mwaka jana akapangiwa shule ya hovyoCHA MSINGI SERIKALI IRUDISHE SIFA ZA SHULE ZAKE ILI WATU WA-OPT ZA GOVERNMENT. SHULE KAMA ILIBORU, MZUMBE N.K SASA ZIMEKUWA CHOKA MBAYA ILI HALI NDO ZILIKUWA VINARA
Mabadiliko mkuu.Hii hatua ni ya kawaida ili kudhibiti ubepari. Ubepari ni unyama!
Pamoja na hayo kazi kubwa ya serikali ni kuziboresha shule zake kwa kila hali ili ufaulu uongezeke. Hapo wazazi wataanza kuzitamani na kwapeleka watoto wao. ikitokea hivo shule binafsi zitashindana kupunguza ada na nyingine zita collapse. Miaka 20+ iliyopita watu walishindana kusomesha watoto shule za serikali! hii inawezekana pia sasa
unaishauri wizara ikisaidiana na kamishina wa Elimu wafanye ukaguzi wakustukiza kwenye mashule binafsi kwa sababu kuna shule nyingi tu tayari zilishapandisha ada na zingine za ajabu kabisa,mfano unakuta shule imeweka michango mbalimbali ambayo haimhusu kabisa mzazi nikitaja mojawapo ni gharama za graduation wazazi tunaambiwa ni za lazima, pili, ada ya matengenezo hailezwi ni matengenezo ya nini?, matibabu ambapo mtoto yupo chini ya mfuko wa bima ya taifa lakini wazazi tunalazimishwa kumlipia mtoto tena, nk haya yote ukijumlisha na ada ni Maelfu ya pesa sijui wao wamiliki wa shule hizi wanatoa wapi bei kubwa namna hiyo? ni maajabu kusema ukweli wazazi tunabebeshwa mizigo mingine ambayo kimsingi haituhusu kabisa ni wajibu wa wamiliki wa shule.Serikali imezipiga marufuku shule zote binafsi za msingi na sekondari kuongeza kiwango cha ada katika mwaka huu wa masomo na kuzitaka shule zote zilizopandisha ada kinyume cha tamko la serikali kusitisha mara moja ongezeko hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ithibati ya Shule, Hadija Mcheka amesema kuwa kufuatia tangazo la serikali la kuzitaka shule binafsi zinazotaka kupandisha ada kuwasilisha maombi yao kwa Kamishna wa Elimu, shule 45 pekee ndizo zilizowasilisha maombi hayo lakini sababu ilizotoa hazikuwa na mashiko.
Alisema kuwa shule nyingine 900 ziliwasilisha maombi ya kuendelea na kiwango cha ada ilichokuwa ikitoza mwaka jana.
Mcheka alieleza kuwa kati ya sababu zilizotolewa na wamiliki wa shule hizo ni pamoja na kuongeza majengo na kuajiri walimu kutoka nje, sababu ambazo Kamishna wa Elimu aliona hazina mashiko kwa kuwa hazimhusu mzazi.
“Mwingine anasema anataka kupandisha ada kwa vile anataka kuajiri walimu kutoka nje ya nchi, hili nalo halimhusu mzazi ndio maana tumewanyima kibali cha kupandisha ada. Sababu zote hizi hazikumridhisha kamishna ndio maana tumewataka watii agizo la Serikali hadi hapo baadaye,” alisema Mcheka.
Akieleza kuhusu mpango wa kuweka ada elekezi, Mcheka alisema kuwa serikali imemuajiri mtaalam mwelekezi atakayefanya kazi ya kubaini gharama za kumsomesha kila mtoto ili kuisaidia serikali kupanga ada elekezi.
Chanzo: Dar24Blog
Msipeleke watoto Tusiime. Shule mbona ziko nyingi? Kwanini mng'ang'anie huko? Shiriki kikamilifu maendeleo ya shule zilizo jirani ili kuziboresha. Mbona wengine tulisoma shule hizo hizo na tulienda vizuri. Na wakati huo IST ilikuweko na ile ya Moshi ilikuweko. Wafundisheni watoto wenu kukubali hali halisi.Kuna haja ya kuwa na monitoring ya jicho la kipekee kwenye hizi shule binafsi, hasa za watu Binafsi, atleast za mashirika ya dini zina ada reasonable...!
Shule kama TUSIIME, unalipa Ada milion 5, kweli!? Na serikali ipo kimya, ina maana ukimaliza elimu ya msingi TUSIIME unaweza kujiajiri!!?
Msipeleke watoto Tusiime. Shule mbona ziko nyingi? Kwanini mng'ang'anie huko? Shiriki kikamilifu maendeleo ya shule zilizo jirani ili kuziboresha. Mbona wengine tulisoma shule hizo hizo na tulienda vizuri. Na wakati huo IST ilikuweko na ile ya Moshi ilikuweko. Wafundisheni watoto wenu kukubali hali halisi.
Mbona hamna nauli elekezi za ndege, bei elekezi za suti, mishahara je? Mbona hawaitaji? Magari je? Mbona hamdai bei zishuke mwandeshe magari wanayoendesha wabunge na mawaziri. Ruzuku walizopewa wabunge na mawaziri zingeelekezwa kwenye elimu watoto wangekaa kwenye madawati. Walishindwa nini kuwasubirisha.
Na wajue hizo shule za private zimekuwa bora sio tu kwa mawazo mazuri na usimamizi wa karibu wa wenye shule bali pia ukaguzi wa mara kwa mara. Vigezo vinavyotumika shule za private zinapokaguliwa, sio tu kwenye taaluma bali hata kwenye miundo mbinu, vikitumika kwenye shule za serikali, hizo shule zitafungwa dakika hiyo hiyo. Usione vyaelea vimeundwa.
Sijaelewa kinachowasumbua hapa ni nini? Mnachotaka ni kufaidika kwa jasho la wengine. Kama mtu alijenga shule na pesa haramu basi na aadhibiwe kwa hilo, lakini kama alijinyima akapambana na wazazi wasiotaka kulea, vitoto vikorofi, akajinyima starehe fulani fulani, akaweza kuendeleza walimu wake na akafaulisha watoto kwa haki, mnachotaka kukifanya ni haramu.
Magufuli sio Nyerere. Haiwezekani ku copy na ku paste. Waje na original ideas.
Naona hiyo shule umeifuatilia kwa karibu sana. Kama una matokeo ya Jangwani, azania, Tabora girls, Tabora boys, Tosamaganga rusha hapa tuyaone. Tatizo la elimu ni zaidi ya unavyolifikiria.Acha kuongea ndoto! Nani amekuambia kuwa walimu wa TUSIIME ni bora kuliko walimu wengine...! Chukua watoto wa TUSIIME leo, wapeleke shule yoyote unayoijua haifanyi vizuri, lazima wafaulu tu!
Kumbuka hizi shule zinazofaulisha zinachukua watoto BEST, sio Bora Twende. Kama huamini, wachukue watoto wa Jitegemee form 2, wapeleke TUSIIME kama hawajatoka na zero kama kawaida yao, maana ndio akili zao zilivyo, hakuna miujiza hapo..! Na ndio maana kuna michujo, mpaka ufike darasa la saba wanabaki na cream tu. Waende na wote uone nini kitatokea...Utakuta matokeo ya TUSIIME, Form IV DIVISION 1-12, DIV II- 8, Div III-164, Div IV-84, Div 0-8.