Serikali yapiga marufuku mifuko laini ya plastiki na pombe maarufu ya viroba

mr gentleman

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,223
4,681
Leo akiongea na waandishi wa habari Mh January Makamba amepiga marufuku matumizi ya mifuko laini ya plastic na pombe za kwenye mifuko ya plastic maarufu kama viroba.

Utekelezaji utaanza rasmi January 2017.

Source: Mimi mwenyewe
-------------—

May 26 2016 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba imepiga marufuku moja kwa moja, utengenezaji, usambazaji, uingizaji nchini na matumizi ya mifuko ya plastiki nchini kuanzia mwaka 2017 hii pia inahusu matumizi ya mifuko ya plastiki inayofungia pombe maarufu kwa jina la viroba.

Waziri Makamba ameeleza kuwa mifuko ya plastiki imekuwa na changamoto kubwa ya mazingira kwa kuwa sehemu kubwa ya mifuko hiyo hutolewa bure na inasambaa na kuziba mifereji hivyo husababisha mafuriko na athari nyingine kubwa kwa mzazingira.

Waziri Makamba ameongeza kuwa ofisi yake inakamilisha majadiliano ndani ya Serikali na baadae kuwahusisha wadau kuhusu dhamira ya kupiga marufuku moja kwa moja matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.

Serikali itatoa muda kwa waliojiajiri na kuajiriwa na kuwekeza kwenye biashara ya mifuko ya plastiki kujiandaa kuacha shughuli hizo na itawezesha mazingira ya utengenezaji na upatikanaji wa vifungio mbadala’

Tumetuma wataalamu wa Serikali katika nchi zilizofanikiwa kwenye jambo hili ili kujifunza namna bora ya kulitekeleza‘

Waziri Makamba ametoa wito kwa watengenezaji, wasambazaji na waagizaji wa mifuko ya plastiki waanze kujiandaa sasa kwa zuio hilo.
 
Nilikua kwenye mkutano mkuu.. Lazima tulinde mazingira yetu na afya za wanachama wa chadema.
wp_ss_20160529_0001.png
 
Nilikua kwenye mkutano mkuu.. Lazima tulinde mazingira yetu na afya za wanachama wa chadema.
Yaani nyie wapiga Kitwanga na viroba mnakurupuka tuu hata hamjielewi.
This year kuna waziri mnywa viroba alisema anaunga mkono viwanda vya kutengeneza mifuko ya plastic kwa sababu inaongeza ajira viwanda tayari vilikuwa vipo leo hii mnapiga marufuku hivi mnajielewa nyie?

Mtu kachukua mkopo kaanzisha kiwanda Leo unapiga marufuku mtamlipia huo mkopo?
 
Dodoma Wine wangetengeneza Wine ya viroba ikawa mbadala na kunyanyua kiwanda cha dodoma wine
 
Hili LA kuzuia mifuko ya plastiki limeweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa sana Unguja, kwa nini bara inashindikana?
 
May 26 2016 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba imepiga marufuku moja kwa moja, utengenezaji, usambazaji, uingizaji nchini na matumizi ya mifuko ya plastiki nchini kuanzia mwaka 2017 hii pia inahusu matumizi ya mifuko ya plastiki inayofungia pombe maarufu kwa jina la viroba.

Waziri Makamba ameeleza kuwa mifuko ya plastiki imekuwa na changamoto kubwa ya mazingira kwa kuwa sehemu kubwa ya mifuko hiyo hutolewa bure na inasambaa na kuziba mifereji hivyo husababisha mafuriko na athari nyingine kubwa kwa mzazingira.

Waziri Makamba ameongeza kuwa ofisi yake inakamilisha majadiliano ndani ya Serikali na baadae kuwahusisha wadau kuhusu dhamira ya kupiga marufuku moja kwa moja matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.

>>>‘Serikali itatoa muda kwa waliojiajiri na kuajiriwa na kuwekeza kwenye biashara ya mifuko ya plastiki kujiandaa kuacha shughuli hizo na itawezesha mazingira ya utengenezaji na upatikanaji wa vifungio mbadala’

>>>’tumetuma wataalamu wa Serikali katika nchi zilizofanikiwa kwenye jambo hili ili kujifunza namna bora ya kulitekeleza‘

Waziri Makamba ametoa wito kwa watengenezaji, wasambazaji na waagizaji wa mifuko ya plastiki waanze kujiandaa sasa kwa zuio hilo.

Chanzo : Millard ayo blog!
 
Jambo jema linaugumu wake hasa kwa wasiokubali kubadilika, ukweli nchi yetu imeumizwa sana na hii mifuko ya plastic
 
Hili LA kuzuia mifuko ya plastiki limeweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa sana Unguja, kwa nini bara inashindikana?

Nijuavyo kwa Unguja wamefanikiwa kwa sababu wazanzibar tamaduni yao ni kubeba vikapu hata wanaume hubeba waendapo sokoni ila kwa uku bara itakuwa ngumu kwa sababu hadi sasa serikali haijapata mbadala wa hiyo mifuko. Serikali inatakiwa iwe na mbadala kabla ya kupiga marufuku la sivyo yatakuwa yale yale ya sukari
 
Leo akiongea na waandishi wa habari Mh January Makamba amepiga marufuku matumizi ya mifuko laini ya plastic na pombe za kwenye mifuko ya plastic maarufu kama viroba.

Utekelezaji utaanza rasmi January 2017.

Source: Mimi mwenyewe

May 26 2016 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba imepiga marufuku moja kwa moja, utengenezaji, usambazaji, uingizaji nchini na matumizi ya mifuko ya plastiki nchini kuanzia mwaka 2017 hii pia inahusu matumizi ya mifuko ya plastiki inayofungia pombe maarufu kwa jina la viroba.

Waziri Makamba ameeleza kuwa mifuko ya plastiki imekuwa na changamoto kubwa ya mazingira kwa kuwa sehemu kubwa ya mifuko hiyo hutolewa bure na inasambaa na kuziba mifereji hivyo husababisha mafuriko na athari nyingine kubwa kwa mzazingira.

Waziri Makamba ameongeza kuwa ofisi yake inakamilisha majadiliano ndani ya Serikali na baadae kuwahusisha wadau kuhusu dhamira ya kupiga marufuku moja kwa moja matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.

Serikali itatoa muda kwa waliojiajiri na kuajiriwa na kuwekeza kwenye biashara ya mifuko ya plastiki kujiandaa kuacha shughuli hizo na itawezesha mazingira ya utengenezaji na upatikanaji wa vifungio mbadala’

Tumetuma wataalamu wa Serikali katika nchi zilizofanikiwa kwenye jambo hili ili kujifunza namna bora ya kulitekeleza‘

Waziri Makamba ametoa wito kwa watengenezaji, wasambazaji na waagizaji wa mifuko ya plastiki waanze kujiandaa sasa kwa zuio hilo.

Agizo ilitakiwa ianze mara moja. (With immediate effect).
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom