Kikwajuni One
JF-Expert Member
- Mar 18, 2013
- 14,694
- 7,912
Wazazi wanapata gharama kubwa ya kulipia,bado hela ya usafiri,dalala,bodaboda,na wazazi wengine wanakuwa na watoto zaidi ya mmoja, kwa mfano anakuwa na mtoto wa darasa la nne,mtoto wa darasa la saba, mtoto wa kulea, aliyefiwa na mzazi wake, ambaye ni ndugu, wa kidato cha pili na wa kidato cha nne, wote hao,wanatakiwa walipiwe.Kuna shule zinatoza mpaka elfu kumi kwa mwezi,huo ni mzigo mkubwa kwa mlezi au mzazi.Tatizo ni likizo, gharama, waraka wa kamishna, au vyote kwa pamoja!??? Kama ni suala la likizo, mbona private schools hawahusiki!???
Hakika uliyosema.Hii itumike hata private school, zifungweee maana ni kukaririsha tu wanafunzi na pesa tu.
Haya mambo yapo scientifically, ajabu watu wanapiga mwisho matoto yanakua mazezeta mbele.
Watoto waachwewa relax na kutumia kile halisi kilichobaki kichwani na wawapime KWA hilo.
Afu private school wanawachimba mabiti sana wazazi KWA hili.
Waziri kazia hapo watoto wapumzike
Elimu ni gharama; wazazi washauriwe wazae watoto wanaoweza kumudu kuwalisha, kuwalea na kuwasomesha. Lazima tujiulize kama taifa, hivi tunataka watoto wetu wapate elimu au mwanga? Ukweli ni kwamba suala la elimu lisingepaswa kufanyiwa negotiations.Wazazi wanapata gharama kubwa ya kulipia,bado hela ya usafiri,dalala,bodaboda,na wazazi wengine wanakuwa na watoto zaidi ya mmoja, kwa mfano anakuwa na mtoto wa darasa la nne,mtoto wa darasa la saba, mtoto wa kulea, aliyefiwa na mzazi wake, ambaye ni ndugu, wa kidato cha pili na wa kidato cha nne, wote hao,wanatakiwa walipiwe.Kuna shule zinatoza mpaka elfu kumi kwa mwezi,huo ni mzigo mkubwa kwa mlezi au mzazi.
Waalimu wanalazimisha, kwa hiyo kwa wasio na uwezo, wa kulipiwa, wanapitwa kimasomo na wenzao wenye uwezo wa kulipiwa,hii inakuwa kama kuna ubaguzi kimasomo.
Hili Neno!Elimu ni gharama; wazazi washauriwe wazae watoto wanaoweza kumudu kuwalisha, kuwalea na kuwasomesha. Lazima tujiulize kama taifa, hivi tunataka watoto wetu wapate elimu au mwanga!??? Ukweli ni kwamba suala la elimu lisingepaswa kufanyiwa negotiations. Vinginevyo, shule za serikali ziboreshwe kuanzia miundombinu, mazingira, walimu, mitaala, nk ili kuhakikisha kwamba mwanafunzi anapokuwa shule, kweli anapata masomo makini na ya kutosha yanayowiana na muda anaokaa ama kwenda shule, kiasi kwamba hatahitaji tena masomo ya ziada.
Huko Finland (Nchi ya Mapezi), ukifundishwa na mwalimu mmoja kwa nusu saa, ubora unazidi hapa kwetu ukifundishwa na walimu ^war-tar-know^ kutwa nzima au hata ^we-key^ moja. Nachelea kusema kwamba mshabihiano huu ni almost sawa na kulinganisha Ferdausi na Jehanamu. Tofauti kabisa!!!Mimi naunga mkono hoja na sio shule za serikali tu wanafunzi wakipata likizo basi iwe likizo kwa maana wapate muda wa enjoy sio likizo baado homework utasema nyumba ndio imekuwa shule hata watoto kufurahia likizo hakuna unaona bora hata shule. Kuna nchi ambazo ziko number one kielimu duniani kama Finland ni marufuku kitu kinaitwa homework wanataka watoto wasome lakini pia wanataka watoto waishi kama watoto kwa kuamini muda wa utotoni ni gift na wanahitaji enjoyment sababu muda unapita lakini mashuleni Finland ni top. Waziri angepiga marufuku aina yoyote ya homework wakati wa likizo.
Naunga mkono hojaSerikali umepiga marufuku masomo ya ziada kwa shule za Serikali na hasa wakati wa likizo,kwa kubainisha kuwa yanaongeza gharama zisizo za lazima kwa wazazi na ni kinyume na waraka wa elimu namba tatu wa mwaka 2016,ambao unataka wanafunzi wapate likizo ama muda wa kupumzika.
Hayo yamesemwa bungeni na Waziri wa elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof.Joyce Ndalichako wakati akitoa taarifa kwa Mbuge wa Bukoba Vijijini Mh.Jason Rweikiza aliyetaka ufafanuzi wa waraka uliotolewa na kamishina kutoka wizara ya Elimu uliotaka shule zote zifungwe wakati wa likizo.
Waziri Ndalichako amesema kuna baadhi ya shule za Serikali zinazalazimisha wanafunzi na wazazi kuchangia gharama kwa kipindi chote cha likizo ambacho wao wanatumia kufundishwa.
Serikali inajifanya kama inawahurumia sana wazazi, ila mimi naona ni baadhi ya viongozi wao watoto wao wanasoma international Schools, katazo hili la masomo ya ziada haliwahusu, zipo shule zinazo somwa na watoto wa walala hoi ili wazidi kudidimia kielimu, international Schools(walipo watoto wao)watazidi kupeta tu na kuja kufaulu vizuri.Serikali umepiga marufuku masomo ya ziada kwa shule za Serikali na hasa wakati wa likizo,kwa kubainisha kuwa yanaongeza gharama zisizo za lazima kwa wazazi na ni kinyume na waraka wa elimu namba tatu wa mwaka 2016,ambao unataka wanafunzi wapate likizo ama muda wa kupumzika.
Hayo yamesemwa bungeni na Waziri wa elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof.Joyce Ndalichako wakati akitoa taarifa kwa Mbuge wa Bukoba Vijijini Mh.Jason Rweikiza aliyetaka ufafanuzi wa waraka uliotolewa na kamishina kutoka wizara ya Elimu uliotaka shule zote zifungwe wakati wa likizo.
Waziri Ndalichako amesema kuna baadhi ya shule za Serikali zinazalazimisha wanafunzi na wazazi kuchangia gharama kwa kipindi chote cha likizo ambacho wao wanatumia kufundishwa.