Serikali yaondoa tozo ya uhakiki na usajili wa viwanda vidogo vidogo

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Prof. Adolph Mkenda amesema kuwa serikali imeondoa tozo ya uhakiki wa viwango vya ubora na usajili katika kuanzisha viwanda vidogovidogo katika shirika la viwango Tanzania(TBS) ambao sasa unafanyika bure.

Prof Mkenda ameyasema hayo alipokuwa akitoa mada katika uzinduzi wa Jukwaa la kuwezesha wanawake na akaunti ya mkopo ya MALAIKA ambayo imeanzishwa katika benki ya Wanawake Tanzania.

Aidha amesema ameagiza kwa wilaya na vijiji kuanzisha viwanda kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanaunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya Tano na kuinua uchumi wa nchi yetu.

“Bidhaa za kilimo kwa sasa zinapewa dhamana na hivyo basi nawaimiza wanawake waanzE kuanzisha viwanda vidogovidogo kwani uanzishwaji wake ni bure,” alisema Prof Mkenda.

Pia alisema kuwa kipato cha kati nchini kinaongezeka siku hadi siku na kuwataka wanawake kutolima kwa mazoea na kuwataka wafanye biashara kwa faida kwa kutumia teknolojia sahihi ili kuongeza uzalishaji.

Katika upande mwingine aliwataka wanawake kutokata tamaa katika kujiinua kiuchumi kwani Serikali ya awamu ya tano iko makini na inaweka mazingira mazuri kwa wanawake kama kuondoa tozo zisizokuwa za lazima ili kuvutia wawekezaji wa viwanda vidogo vidogo.

Katika uzinduzi huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Bi Samia Suluhu Hassan alizindua jukwaa hilo na akaunti ya mikopo ya wanawake ya MALAIKA kupitia benki ya wanawake ambayo akaunti hiyo itakuwa na mikopo yenye riba nafuu ya asilimia 5 kwa muda wa miezi sita,mafunzo yanatolewa bure,hamna haja ya kuleta mchanganuo wa mahesabu na hakuna hitaji la dhamana yenye lengo la kuwakwamua wanawake kiuchumi.
1-2-702x336.jpg
 
Wangeweka kila mkoa au wilaya vitengenezwe viwanda vidogo vidogo
 
Back
Top Bottom