Serikali yanawa mikono Al-Shabab Mtanzania

Serikali yanawa mikono Al-Shabab Mtanzania

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713

paul-chagonja1-300x225.jpg

WAKATI mama mzazi wa Mtanzania Rashid Mberesero anayetuhumiwa kuwa kati ya wafuasi wa Al-Shabaab walioua wanafunzi 148 wa Chuo Kikuu cha Garissa nchini Kenya akitaka msaada wa Serikali ili akamwone mwanawe huyo, Jeshi la Polisi limesema halina uwezo wa kumsaidia.

Jeshi hilo limesema halina uwezo wa kumsaidia mama huyo, Fatma Ally kutokana na sheria mpya za ugaidi zilizopitishwa nchini Kenya hivi karibuni na kuwekewa pingamizi mahakamani.

Aidha limesema hadi sasa bado halijafuatilia tukio la kukamatwa kwa kijana huyo na kuwa habari zake linazifuatilia kwenye vyombo vya habari tu.

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Paul Chagonja, ameliambia MTANZANIA kuwa hajui msimamo wa Kenya ukoje kuhusu tukio hilo.

Alisema suala hilo ni la kisheria zaidi na sheria zinatofautiana baina ya nchi na nchi ikiwamo utaratibu wa kumwona mtu akiwa mahabusu.

"Jeshi la Polisi hatujui chochote kuhusu mtuhumiwa huyo zaidi ya kusoma kwenye magazeti, kwa hiyo ni ngumu kusema kama mama yake ataweza kumwona au la kutokana na sheria mpya za ugaidi walizopitisha wenzetu hivi karibuni.

"Sijazipitia vizuri sheria hizo, lakini baadhi yake zina makali zaidi, kwa hiyo siwezi kutia neno, tuwaachie uhuru wa sheria zao wenzetu waamue," alisema.

Aidha alipoulizwa kuhusu taarifa za utaratibu wa kijana huyo kuwepo nchini Kenya, alisema hawana taarifa zake zaidi ya kusoma kwenye magazeti kwamba alitoweka nyumbani na shuleni.

Kutokana na hali hiyo, alisema Serikali sasa inategemea huruma ya Kenya katika kumponya ama kumwadhibu kijana huyo kwa mujibu wa sheria zake.

Kwa mujibu wa Fatma alikuwa anajua mtoto wake yupo shuleni Bihawana mkoani Dodoma alipokuwa akisoma kidato cha tano huku uongozi wa shule ukisema alitoroka tangu Novemba mwaka jana.

Sheria mpya ya ugaidi nchini Kenya, ambayo baadhi ya vipengele nane vilipingwa mahakamani inatoa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya dola 55,000 kwa uchapishaji bila ruhusa wa makala au kutafuta habari amzazo zitatatiza uchunguzi ao operesheni ya kupambana dhidi ya ugadi.

CHANZO: Mtanzania
 
Bado mapema sana kwa huyo mama kufikiria kwenda Kenya kumwona kijana wake. Wala hajaikosa hiyo nauli ya kumfikiaha huko na kurudi. Kuihusisha serikali imsaidie jinsi ya kwenda kumwona huyo kijana wake ni sawa na kuijaribu serikali. Sasa asije akajidanganya kujizoa zoa na kuongia Kenya kumlilia balozi wetu kule jibu litakuwa hilo hilo na mbaya zaidi akionyesha pass yenye jina lake mpakqni tu amenganganiwa na maafisa wa immigration wa Kenya. Ajitulize hadi hali ipoe.
 
Yaani huyo mama nae hatari.Watu hata 40 Hawajamaliza wanalilia watoto wao waliouawa na huyo mwanae yeye anataka safari ya kiutalii kwenda kumtalii mwanae.Akikanyaga kenya akivuka mpaka tu watamla nyama wala hafiki hata Nairobi wananchi wenye hasira watamwulilia mbali.Au naye ni gaidi anataka kutoroka nchi kwa kisingizio cha kumwona mwanae?
 
Kama iyo mama peleka huko kenya damu za watu 145 si mchezo
 
Yaani huyo mama nae hatari.Watu hata 40 Hawajamaliza wanalilia watoto wao waliouawa na huyo mwanae yeye anataka safari ya kiutalii kwenda kumtalii mwanae.Akikanyaga kenya akivuka mpaka tu watamla nyama wala hafiki hata Nairobi wananchi wenye hasira watamwulilia mbali.Au naye ni gaidi anataka kutoroka nchi kwa kisingizio cha kumwona mwanae?

Hizo ndugu yangu ndio akili za wenzetu hao. Hivi kweli hana hata mwenza au ndugu wa kumshauri? Hata kama roho ya mama huumia zaidi kwa mwanae anapopata matatizo lakini kwa janga kubwa kama hili hatakiwi kukurupuka labda kama anahusika kwa njia moja au nyingine anaona ajisalimishe mapema. Hivi hafikirii uchungu wa wazazi ambao watoto wao walichinjwa na huyu gaidi? na nasikia wangemaliza kazi salama ilikuwa waje kulipua uwanja wa taifa kwenye tamasha la pasaka. Yeye atulie tu serikali yetu au ya Kenya ikipata connection nzuri lazima iwahoji kwa undani wazazi wa kijana huyo.
 
" Kwa mujibu wa Fatma alikuwa anajua mtoto wake yupo shuleni Bihawana mkoani Dodoma alipokuwa akisoma kidato cha tano huku uongozi wa shule ukisema alitoroka tangu Novemba mwaka jana, "

Mzazi wa aina gani huyu mtoto katoroka shule tangu Novemba leo April ndiyo unaomba msaada wa Serikali kweli?

Ulikuwa wapi kuomba msaada kutoka serikalini au polisi wamtafute mwanao tangu alipotoroka shule Novemba?

Kumekuwa na likizo ngapi mwanao asirudi nyumbani mpaka leo hii unatafuta msada serikalini?

Kama yeye alishindwa kuisaidia serikali kuwa mtoto wake ni gaidi kwanini serikali imasidie?

Huyo mama mtu atakuwa hana akili, akatafute msaada kwa Al Shabaab's symphathisers wenzake huko kama FaizaFoxy et al
 
Last edited by a moderator:
" Kwa mujibu wa Fatma alikuwa anajua mtoto wake yupo shuleni Bihawana mkoani Dodoma alipokuwa akisoma kidato cha tano huku uongozi wa shule ukisema alitoroka tangu Novemba mwaka jana, "

Mzazi wa aina gani huyu motto katoroka shule tangu Novemba leo Aprili ndiyo unaomba msaada wa Serikali kweli?

Ulikuwa wapi kuomba msaada kutoka serikalini au polisi wamtafute mwanao tangu alipotoroka shule Novemba?

Kumekuwa na likizo ngapi mwanao asirudi nyumbani mpaka leo hii unatafuta msada serikalini?

Kama yeye alishindwa kuisaidia serikali kuwa motto wake ni gaidi kwanini serikali imasidie?

Huyo mama mtu atakuwa hana akili, akatafute msaada kwa Al Shabaab symphasizer wenzake huko kama faiza Foxy et al

Mkuu kuna issue kwa huyu mama pia comment zako zimechambua vizuri mno.

Ila la kuhusu FAIZA FOXY msubiri aje akujibu mwenyewe atakuwa bafuni labda anaoga.
 
Wazaz wengine ni wanafiki tu hupata watoto kwa bahat mbaya maana madhumun ya ndoa yao huwa kugegedana tu! Nahisi dogo alikuwa very lonely hakuna aliyemjali hata kidogo! Alichokosea dogo ni kukubali kwenda kuwaua wasio na hatia KABLA ya kwanza kwenda kuwafyagia wazazi wake nafsi yake ikunjuke NDIO MAANA KAKAMATWA!
 
Wamuhoji tujue alisomea madrasa ipi tuanziehapo
 
Pengine huyu mama alimtuma mwanae

Ndio mana anataka akamtetee ATI JAMANI MUACHIENI HURU HANA MAKOSA NI WENZAKE WALIMFUATA SHULENI WAKAMLUBUNI ILI AJIUNGE NA KUNDI HILO NA KUFANYA WALIVYOFANYA
 
Hii ngoma nzito sana halafu bado mbichi huyu mama apewe ushauri akijichanganya akienda huko kwenye kutoa maelezo atajichanganya watamsweka ndani! Somalia watapiga tena mzinga mwingine wa maana wakishinikisa wamwachie huru dogo!
 
Hizo ndugu yangu ndio akili za wenzetu hao. Hivi kweli hana hata mwenza au ndugu wa kumshauri? Hata kama roho ya mama huumia zaidi kwa mwanae anapopata matatizo lakini kwa janga kubwa kama hili hatakiwi kukurupuka labda kama anahusika kwa njia moja au nyingine anaona ajisalimishe mapema. Hivi hafikirii uchungu wa wazazi ambao watoto wao walichinjwa na huyu gaidi? na nasikia wangemaliza kazi salama ilikuwa waje kulipua uwanja wa taifa kwenye tamasha la pasaka. Yeye atulie tu serikali yetu au ya Kenya ikipata connection nzuri lazima iwahoji kwa undani wazazi wa kijana huyo.

Umesikia wapi wewe kuwa walikuwa waje taifa,kaka mabwepande hiyo inakuita
 
Sijamwelewa huyu mama.likizo ya december mwanae alienda nyumban au?na km hakwenda huyu mama alifanya jitihada gan kumtafuta mwanae?kiukweli haiingii akilini tokea nov hadi april ina maana hawakuwa na mawasiliano au changa la macho?
 
Ndio mana anataka akamtetee ATI JAMANI MUACHIENI HURU HANA MAKOSA NI WENZAKE WALIMFUATA SHULENI WAKAMLUBUNI ILI AJIUNGE NA KUNDI HILO NA KUFANYA WALIVYOFANYA

akipatikana na hatia wala asinuse bongo kabisa
 
Back
Top Bottom