Serikali yamruka mkurugenzi Tanesco

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


JUMANNE, JULAI 24, 2012 06:02 NA BAKARI KIMWANGA, DAR ES SALAAM


*Yasema haikumsimamisha kazi bali ni bodi
*Yasisitiza hakuna mgawo wa umeme nchini

SERIKALI imesema haijahusika kwa namna moja au nyingine kusimamishwa kazi kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), William Mhando.

Kauli hiyo, imetolewa mjini Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, alipokutana na waandishi wa habari ofisini wake.

"Naomba tuelewane waandishi, napenda kuwahakikisha kwamba Serikali haihusiki hata kidogo kusimamishwa kazi kwa Mhando, bali uamuzi huo umefanywa na bodi ya shirika husika.

"Kwa vile uamuzi huu umefanywa na Bodi ya Wakurugenzi, hauna uhusiano wowote na wizara yangu."

Alisema kutokana na suala hilo kuwa katika uchunguzi, ni vyema jamii ikawa na subira na kusubiri maamuzi yatakayotolewa na watumishi wengine waliosimamishwa kazi.

"Ninapenda ieleweke, Mhando hajafukuzwa kazi, ila amesimamishwa kama ilivyo kuwa watumishi wengine wa Serikali na katika hili wizara haihusiki na kusimamishwa kwake, kwani kilichofanyika ni maamuzi ya bodi ya wakurugenzi ambayo ni halali kwa mujibu wa sheria," alisema Maswi.

Akizungumzia hatari ya nchi kuingia kwenye mgawo wa umeme, Maswi alisema kuna akiba ya kutosha ya umeme, jambo ambalo hatarajii kutokea kwa mgawo kutokana na juhudi mbalimbali zilizofanywa na Serikali.

Alisema taarifa mbalimbali zinazotolewa kupitia baadhi ya vyombo vya habari hazina ukweli na kwamba zinakusudia kuwapa wananchi wasiwasi wa bure.

"Ni vizuri ikaeleweka, kiasi cha upatikanaji wa umeme kwa sasa kinakidhi mahitaji… hakuna suala la nchi kuingia gizani au kufanya kuwepo mgawo wa umeme, nasema halipo.

"Mahitaji ya umeme kwa sasa ni wastani wa kati ya MW 650 hadi 720, uwezo wa ufuaji umeme utokanao na maji, gesi asili, na mafuta ni MW 720.

"Mitambo ya nguvu za maji itazalisha kati ya MW 120 HADI 151 (wastani wa MW 132), ambapo kituo cha Mtera kinazalisha MW 22, Kidatu MW 54, Kihasi MW 60, Nyumba ya Mungu MW 3, Hale MW 3 na New Pangani Falls MW 9," alisema Maswi.

Alisema mitambo ya gesi asili itakuwa wastani wa MW 348 kwa mchanganuo wa Songas MV 180, Ubungo Gas Plant 1(wartsilla) MW 77, Tegeta Gas plant MW 41, Ubungo Gas plant 11 (Jacobsen) MW 50.

"Kwa hali hiyo mitambo ya mafuta itakuwa na wastani wa MW 240 kwa mchanganuo wa IPTL mw 100, Symbion Dodoma MW 40, Symbion Arusha MW 40 na Symbion Ubungo (Jet A1) MW 60.

"Kuna baadhi ya wanaodhani suala la mkopo wa Sh bilioni 408 kwa TANESCO, ndiyo njia pekee ya kuhakikisha upatikanaji wa umeme.

"Na kati ya Agosti 2011 na Juni, 2012 Serikali imeshatoa jumla ya sh bilioni 222.4 ambazo ni ruzuku na siyo mkopo kwa TANESCO.

Alisema hivi karibuni Serikali imetoa Sh bilioni 25 ili kuhakikisha mafuta ya kutosha yanapatikana, ili umeme wa uhakika uwepo.

Alisema Serikali inachukua hatua za makusudi kuhakikisha umeme wa kutosha unapatikana na ndiyo maana imetoa Sh bilioni 247.4 mpaka sasa.

 
Siku hizi ni Bodi inakusimamisha Kazi; Safi Sana...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom