Serikali yamkomoa msaidizi wa Mkapa... NSA KAISI!!!

Serikali yamkomoa msaidizi wa Mkapa... NSA KAISI!!!

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
[TABLE="class: contentpaneopen, width: 728"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen, width: 728"]
[TR]
[TD]Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: createdate"]Jumanne, Januari 15, 2013 05:20[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
Kanali mstaafu Nsa Kaisi, ambaye amekuwa Msaidizi wa Rais Benjamin Mkapa kwa miaka mingi, amepokwa shamba lenye ukubwa wa ekari 14 katika eneo la Pugu Mwakanga mkoani Dar es Salaam.
Uvamizi huo umefanywa na kundi la watu mnamo Oktoba 19, 2011. Pamoja na kuwa na hati zote za umiliki halali wa eneo hilo, Serikali pamoja na vyombo vyake, hasa Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam, imegoma kumsaidia.

Kaisi ambaye amewahi kuwa mkuu wa wilaya na mikoa mbalimbali, amehangaika kwa muda wote huo katika ngazi nyingi, lakini ameshindwa kabisa kupata msaada wa kumwezesha kupata haki yake.


Kwa mujibu wa Mipango Miji, eneo hilo limeteuliwa na kutengwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya huduma za viwanda, na yeye amekuwa akilipia hati zote tangu alipomilikishwa eneo hilo .
Kova amtosa, ataka aende mahakamaniHata Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Saalam, Suleiman Kova, amekataa kumsaidia kuwaondoa wavamizi hao.

Kaisi analithibitisha hilo kwa kusema, "Nilipoona sipati jibu kwa barua yangu ya Januari 10, 2012 nilikwenda kuonana na DCP Kova.

Alinielekeza kwamba siyo kazi ya polisi kuondoa wavamizi na akanitaka nionane na DC (Mkuu wa Wilaya ya Ilala) ili nipewe barua kwenda mahakamani kupata ‘Court Order'.


"Nilipokwenda kwa wanasheria kutaka ufafanuzi zaidi, walishangaa kwa wasimamizi wa sheria na kanuni wamenieleza hivyo; kutokana na kwamba wavamizi wa eneo langu wameachiwa kuharibu mali yangu halali kisheria, pamoja na kwamba wametenda kosa jingine kufuatana na Penal Code: Under Section 299, Sub-section (a) and (b) ambayo inazungumzia ‘Criminal Trespass'."
Mwanzo wa matatizo yoteUchunguzi unaonyesha kuwa Novemba 24, 2011 alimwandikia barua aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni , Jordan Rugimbana; Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile; (kwa wakati huo) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime; akiwaeleza juu ya uvamizi huo, lakini kote huko hakusaidiwa.

Katika barua hiyo, Kaisi alisema, "Kwa heshima nakuja mbele yenu kuomba msaada wa kuwaondoa, kuwakamata na kuwafikisha mbele ya sheria kundi la wavamizi ambao Oktoba 19, 2011, majira ya saa tatu usiku walivamia na kuingia eneo langu ninalomiliki kisheria, ambalo lipo Pugu Mwakanga, Mtaa wa Kigogo Fresh, Kata ya Pugu.

"Baada ya kutokea uvamizi, msimamizi wa eneo hilo , Omari Nyangala, alitoa taarifa kwenye uongozi wa Serikali ya Mtaa, Kigogo Fresh. Viongozi hao walichukua jukumu la kuwaita wawakilishi wa wavamizi na kuwaeleza kuwa eneo linamilikiwa na mimi kisheria, pamoja na kuwaonya kwamba Serikali ya Mtaa haiwatambui na inawataka waondoke katika eneo hilo; wao waliwajibu viongozi wa Serikali ya Mtaa kwamba, ‘sisi siyo wavamizi ila tumekuja kuishi baada ya kukuta kuna shamba pori, mwenyewe ameshindwa kuliendeleza kwa muda mrefu kwa mujibu wa wenyeji walivyosema. Tulikuwa hatuna mahali pa kukaa, tumeamua tuishi hapo…Tupo watu 240 na tutaendelea kuwepo, iwapo kuna mtu amejitokeza anasema pake atupeleke mahakamani ili tukasikilizwe maelezo yetu'."

Imeelezwa kuwa baada ya mahojiano na wavamizi, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa aliyetajwa kwa jina moja la Maguno alipeleka taarifa kwa Kamanda wa Polisi Wilaya ya Sitakishari, akiomba msaada wa kuwaondoa wavamizi.


Kituo cha Polisi Sitakishari kilifungua jalada STU/RB/16093/2011/KUINGIA/JINAI. Novemba 19, 2011 Mkuu wa Kituo (OCD) hicho, Jumanne Muliro alifika eneo la tukio na kuwakuta baadhi ya wavamizi wakiendelea na ujenzi.


"OCD aliwafahamisha kwamba eneo walilovamia lilikuwa na mmiliki halali kisheria na kuwaelekeza kwamba iwapo walihitaji eneo la kujenga na kuishi inabidi wapeleke maombi yao kwa viongozi wa Serikali ya Mtaa.


"Pamoja na ushauri wa OCD, wavamizi bado wapo wanakalia eneo langu na kuendelea kuleta uharibifu mkubwa…tayari wameshateketeza mali zangu nyingi na kupora vitu mbalimbali pamoja na kuvuruga mazingira," amesema Kaisi katika barua yake kwenda kwa Rugimbana.


Kaisi, anawaomba viongozi wanaohusika katika utatuzi wa mgogoro huo kwa kusema, "Ninawasihi viongozi wangu mchukue hatua zipasazo za haraka za kushughulikia wavamizi hawa na kulikomboa eneo langu.


Kitendo chao ni cha jinai, kinavunja sheria na Katiba ya Tanzania …binafsi nilionalo baya zaidi, ni kule kuwepo katika jamii yetu makundi ya wahalifu ambao wamejiandaa kufanya na kuendeleza vitendo vya kijinai with utter impunity na wakati huo huo wakitishia amani miongoni mwa jamii.
Kwa upande mwingine, inaashiria kuwa kikundi cha watu 240 kilichovamia eneo langu ni mojawapo tu ya vikundi vingine ‘crime active and operating' katika Wilaya ya Ilala na Jiji kwa jumla."

Hata hivyo, ana maswali mengine anayojiuliza: Je, hivi viko vingapi? Pamoja na uvamizi wa ardhi, vinaendeleza uhalifu gani mwingine? Viongozi wa vikundi hivi ni nani? Je, upo uwezekano kwamba vikundi hivi vya wahalifu vinashirikiana na baadhi ya viongozi wa Serikali za Mitaa, watendaji wa Kata, na makatibu tarafa? Kwanini wanavikundi wajigambe na kujieleza kuwa wao ni Wakurya? Ni kweli kwamba makao makuu ya vikundi hivi ni maeneo ya Kitunda na Mombasa-Ukonga?


Kaisi anahitimisha kwa kutoa ombi, "Viongozi wangu, nikiwa raia mwema, nina imani na mfumo wetu wa kulinda watu na mali zao, pamoja na kudumisha amani katika nchi yetu kwa kuzingatia na kuheshimu sheria; yaani kuwepo kwa utawala wa sheria. Kwa hiyo, ninaendelea kuwasihi kunipa msaada wa kushughulikia ipasavyo wavamizi wa eneo langu, pamoja na kuwaondoa, kuwakamata na kuwafikisha mbele ya sheria."
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam azungumzaKwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck, amezungumza na JAMHURI na kusema hana taarifa za uvamizi wa shamba la Kanali Kaisi.

"Kwa kweli sina habari, bahati mbaya kwa sasa nipo Mwanza, wasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala inawezekana yeye akawa na uelewa wa suala hilo.


"Kila kitu kinakwenda kwa utaratibu na sheria, tutaangalia namna alivyovamiwa na tutafikia mwafaka.


"Nakumbuka tuliagiza operesheni ifanyike katika wilaya zote za Dar es Salaam kuondoa waliovamia ardhi ili irejeshwe kwa wamiliki halali, Nadhani suala la Mheshimiwa Kaisi litakuwa kati ya hayo, wiki ijayo (wiki hii) nitakuwa ofisini, nakuhakikishia kuwa haki itatendeka," amesema Meck.
Kauli ya DC wa IlalaMkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, ameiambia JAMHURI kuwa ana taarifa zote zinazohusu uvamizi wa mashamba na viwanja vya wananchi katika maeneo mengi ya Wilaya ya Ilala, yakiwamo ya Pugu, Chanika na Msongola.

"Juhudi zinaendelea kufanywa kukabiliana na hali hii, najua kabisa uvamizi upo, lakini kusema ukweli sikujua kama Mzee Kaisi naye yupo kwenye matatizo haya.


"Inawezekana kweli akawa na tatizo hilo kwa sababu kuna wakati alimtumia mtu mmoja kuweka miadi ya kuonana na mimi. Nikawapa siku na muda wa kuonana naye, lakini sikumwona," amesema.


Amesema kama mtu anamiliki ardhi, na akatokea mtu akaingia kwa jinai, ni wajibu wa polisi kumwondoa mvamizi au wavamizi.


" Kama ni civil matter inabidi iingie mahakamani, Mahakama itoe order. Sisi Serikali, polisi ni wajibu wetu kusimamia kumtoa huyo mvamizi.


Kama ni sura ya criminal, yule aliyeingia kwa jinai akamatwa, anafunguliwa kesi mahakamani. Kwa wasio na hati kuna mlolongo mrefu kwa sababu inabidi Mahakama isikilize na kutoa uamuzi; kama Mzee Kaisi ana hati hilo ni suala la kuwaondoa wavamizi tu," amesema.


Hata hivyo, Mushi ametoa rai kwa vyombo vya habari kuhakikisha vinawaelimisha wananchi ili wasiwe kikwazo wakati wa kuwaondoa wavamizi.


"Watu wanavamia maeneo ya watu wengine kwa makusudi, tukitumia nguvu kuwaondoa utasikia mara ooh haki za binadamu zinavunjwa, polisi wanatumia nguvu…Haiwezekani kukawa na watu ambao kazi yao ni kuvamia tu, na pale wanapoondolewa ndipo ionekane haki za binadamu zinavunjwa.

"Vyombo vya habari vitusaidie kukabiliana na wahalifu hawa, amesema Mushi."
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Sawa, Mkuu huyu Nsa Kaisi kama ulevi wa madaraka basi alilewa akawa chakali, habari zisizothibitisha huyu jamaa hana mken wala mtoto, mke wake alikuwa madaraka aliyokuwa nayo. Akiwa ni mkuu wa mkoa wa mtwara kwakutumia madaraka yake anamiliki eneo kubwa zaidi ya eka 10 kwa wanaoishi Mtwara eneo hilo liko wazi hadi hivi leo limepakana na VETA na nyumba za kilimo pale shangani, pia aliacha gari mpya kabisa mpaka sasa inaoza pale yadi za VETA, Pickup fulani hivi,, eneo hilo la shangani watu wanalimezea kweli, kumbe ana eneo lingine kama hilo huko Pugu, nawaunga mkono wanainchi waliovamia, kuna usemi unaosema kwamaba "ukishiba sana usimwonyeshe mungu tumbo" sasa Nsa kaisi amshiba sana anahozi maeneo hawezi kuyatumia wacha wenye shida watumie.
 
Duuuh_pole nsa kaisi,...ila kweli ulikua jembe enzi zako ...ingawa watu wengine wanakubeza.
 
Hili jamaa limezeeka sasa. Alifukuzwa na mishale kwenye mkoa mmoja kipindi cha Nyerere akiwa RC.
 
Nsajigwa Kaisi alikuwa noma sana enzi zake. Heri angekomolewa hata bosi wake maana wote walilewa madaraka na kujisahau sana. Sijui kama alliishaoa huyu jamaa Kanali wa jeshi mpenda makuu. Natamani hata mke wa Mkapa anyang'anhywe mali alizotuibia kama vile maghorofa ya Msimbazi na nyingine nyingi. Waliasisi ujambazi sasa wanaanza kulipia. Shame on them!
 
Mimi sijui sheria ,ila kwa maelezo ya hiyo habari naona Nsa Kaisi ana stahili apewe haki yake ya umiliki.Ila kama hataweza endeleza kwa miaka mingine mingi ijayo nadhani sheria inabidi iwepo ya kuchukua hilo eneo na kuwapa watu ambao wanaweza endeleza.
 
Sawa, Mkuu huyu Nsa Kaisi kama ulevi wa madaraka basi alilewa akawa chakali, habari zisizothibitisha huyu jamaa hana mken wala mtoto, mke wake alikuwa madaraka aliyokuwa nayo. Akiwa ni mkuu wa mkoa wa mtwara kwakutumia madaraka yake anamiliki eneo kubwa zaidi ya eka 10 kwa wanaoishi Mtwara eneo hilo liko wazi hadi hivi leo limepakana na VETA na nyumba za kilimo pale shangani, pia aliacha gari mpya kabisa mpaka sasa inaoza pale yadi za VETA, Pickup fulani hivi,, eneo hilo la shangani watu wanalimezea kweli, kumbe ana eneo lingine kama hilo huko Pugu, nawaunga mkono wanainchi waliovamia, kuna usemi unaosema kwamaba "ukishiba sana usimwonyeshe mungu tumbo" sasa Nsa kaisi amshiba sana anahozi maeneo hawezi kuyatumia wacha wenye shida watumie.

Wacha wivu na majungu wakati Huo umepita, tafuta zako na utumie unavyopenda.
 

Kanali Mstaafu Kabenga Nsa Kaisi inaonekana ni mtu mhangaikaji sana katika kutafuta maisha na hivyo haki zake kisheria ziheshimiwe

Mifano ya uhangaikaji wake katika KILIMO-KWANZA
TM Plantations is a subsidiary of TM Global Holdings, an investment fund set up by Tony Tan that is registered in Delaware, US and that focuses on investments in emerging markets. In July 2007, TM Plantations paid preliminary survey fees to the Kasulu District government of Tanzania to investigate the feasibility of establishing an oil-palm plantation on 50,000 ha, and the company is also pursuing land acquisitions for forestry. In 2007, Colonel Kabenga Nsa-Kaisi, former chief counsellor to Tanzanian President Benjamin Mkapa, was appointed to the board of TM Plantations.Source: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...i-iliyonyakuliwa-na-wawekezaji-wa-kigeni.html
[h=4]Former Chief Cousellor to President Mkapa appointed to board of TM PLANTATIONS LTD.[/h]
NSAKAISI.jpg
From Left: Colonel (rtd) Kabenga Nsa Kaisi chatting
with Mr. Tony Tan
On August 1st, 2007, Colonel (rtd) Kabenga Nsa-Kaisi, the former chief counsellor to Tanzanian President Benjamin Mkapa was appointed as an independent non-executive director to the board of TM PLANTATIONS LTD.
Colonel Nsa-Kaisi is currently serving as Group Chairman of TM ACACIA HOLDINGS LTD, a subsidiary of the TM GLOBAL HOLDINGS Group. INVESTMENTS INTO EMERGING MARKETS. - Newsflash 4
TM ACACIA HOLDINGS LTD subsidiaries are involved in plantations, property development, marketing and food-processing activities.
 
Huyo anayesema alikuwa mchumia tumbo cjui,ila kwa wakati aliokuwa mtwara alifanya mengi mazuri,humpati RC anayekaa na wanafunz na kudiscus naye mambo ya kijamii au hata ile hulka yake ya kutembea kwa miguu mitaan kukutana na wananchi wake.
 
Huyu jamaa hafai kabisa.Ngoja nae aipate tena bado,na mimi ningekuwa naweza ningemshughulikia nikikumbuka alivyo wafanyia wazee wet enzi za kilichoitwa uhujumu uchumi,watu walitafuta mali zao kwa haalali yeye akazitaifisha, akawafunga na kuwatesa,sasa wenzie wameshakufa akina Sokoine yeye muache na kabla hajafa asubiri ataona mengi maluuni mkubwa
 
Nsajigwa Kaisi alikuwa noma sana enzi zake. Heri angekomolewa hata bosi wake maana wote walilewa madaraka na kujisahau sana. Sijui kama alliishaoa huyu jamaa Kanali wa jeshi mpenda makuu. Natamani hata mke wa Mkapa anyang'anhywe mali alizotuibia kama vile maghorofa ya Msimbazi na nyingine nyingi. Waliasisi ujambazi sasa wanaanza kulipia. Shame on them!

Kanali Nsa Kaisi anaweza kuwa aikuwa na matatizo yake kama binadamu lakini ukweli unabaki kuwa kama kiongozi wa nchi hii alikuwa mzalendo wa ukweli tofauti na viongozi wa siku hizi ambao uongozi wao uko katika kujali matumbo yao. Nsa Kaisi alikuwa ni mchapa kazi, mjamaa na anayezingatia maadili ya kazi. Hakuwa na mchezo kazini alikuwa ni mtu wa uwazi na ukweli na mkali kiutendaji kwa faida ya nchi hii iliyojaa, kwa sasa, viongozi wapiga majungu na wanafiki. Kaisi hakuwa mnafiki.
 
Nchi ambayo haiheshimu sheria haiwezi kupata maendeleo yoyote. Kinachokufanya uwe na uhakika wa chochote unachomiliki ni sheria bila ya sheria ina maana watu wanaweza kujikusanya wakati wowote, wakawa wengi wakaja kuchukua chochote wanachotaka.

Kama Kaisi anamiliki eneo hilo kisheria, ni kosa kubwa kwa serikali kushindwa kuhakikisha sheria daima inafuatwa na kulindwa. Jukumu kubwa na la msingi la serikali yoyote halali Duniani ni kusimamia sheria. Iwe ni Kaisi au mtu mwingine yeyote, kuvamiwa eneo lake analomiliki kisheria ni kosa, ni kosa kubwa. Wanaoshabikia uvamizi hawajui wanachoshabikia.

Fikiria kidogo unachomiliki, watu wakaja wakakichukua kwa nguvu, utasema ni halali kwa sababu wao hawana hata hicho kidogo?
 
Inapaswa aende mahakamani apate court order, ndio polisi wataitumia kuzuia wavamizi kuendelea na shughuli zao. Sio rahisi kwa polisi kushughulika na kila mtu anayaenda kituoni kudai eneo lake limevamiwa. Mtu anaweza kwenda kudai ikulu ni eneo lake polisi wakaenda kutoa watu maofisini kama ni hivyo!!
 
Wanaoporwa ardhi nchii hii ni wengi mno nenda dodoma ushuhudie migogoro ya ardhi kati ya cda na wananchi hao ndio zao la uporaji!!!!!!!!!!!!!!
 
"Nilipoona sipati jibu kwa barua yangu ya Januari 10, 2012 nilikwenda kuonana na DCP Kova..."
Wazee wetu hawa mpaka leo masikini hawaelewi concept nzima ya utawala bora. Mzee Kaisi, ulipata access ya kuonana na Kamanda Kova wewe kama nani?

Nchi za wenzetu huwezi kuibuka tu ofisini kwa, lets say Chief of Police Kelly wa New York, ukasema nimeibiwa kiwanja changu huko Brooklyn nataka unisaidie, huwezi, Chief of Police wa mji kama huo ana schedule imejaa mwezi mzima na asingependa kuonekana ana toa privileged access kwa wachache fulani. The fact kwamba Kova ameonana nae na akasema nenda mahakamani na ikatoka kwenye press tayari hiyo ni big push toward justice, wavamizi wamesikia, mahakama imesikia, na wananchi wamesikia. Kova haelewi, Kaisi haelewi, Kikwete haelewi!

News press nayo hivyo hivyo, hawaelewi, hii ni kesi ya Mtanzania mmoja amevamiwa kiwanja, haina u-special case wowote, watu wanavamiwa viwanja na mashamba na matapeli, wawekezaji, wafugaji, madalali, matajiri, kiiiiiila siku ya Mola na hakuna headline inaandikwa "Bi Mwantumu Kijakazi avamiwa kiwanja," lakini Mr. Nsa Kaisi yes, atapewa access to DCI and press coverage to boot.

Why?
 
Pole Mzee Kaisi, ila si unajua mjini hakuna tena mashamba bali ni viwanja na inabidi uendeleze!! Wewe ukukalia kufuga nyoka na kenge wenzio hawana pa kuishi!!

Ila kwa wavamizi, imekula kwao!! Kama ana tittle hata kama hajaendeleza ni mali yake!! Cha msingi hukumu itawataka wavamizi waondolewe kwa nguvu na kuharibi kila walichokiendeleza bila fidia na Kaisi atapewa muda wa kupaendeleza. Na kwa neema yake atapauza!! Kwa hiyo wavamizi kama wanajenga pale wajue kuwa itakula kwao miaka michache ijayo kesi ikimalizika!! Ndivyo sheria za ardhi zilivyo!! Kama asingekuwa na hati ingekuwa historia nyingine!! Mwenzio mzee kileo ile nyumba yake mtaa wa Ohio ni mavumbi tu maana tingatinga lilifanya kazi yake jana!! Ila naye mbishi serikali ilimpa nyumba nyingine Mbezi Beach naona hakuifurahia kulinganisha na thamani ya kiwanja na nyumba yake maana alishamilikishwa na TBA na hati anazo!! Kiuhalali angeweza kuingia share na mwekezaji, the So called Investiment Bank!! Tanzani hakuna haki ya kusikilizwa!!
 
Back
Top Bottom