Serikali yamjibu Mh Lowassa kisaikolojia!

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,184
11,201
Sio siku nying nilisema mh Lowasa anapaswa kujibiwa.

Leo ktk taarifa ya habari TBC1 Napenda kunuku maneno ya Mh Glaudensia Kabaka waziri wa Vijana na ajira. "Sii kweli kwamba serikali imesema imelifungia macho swala la ajira".

Ndugu msomaji hivi majuz Mh Lowasa aliinyooshea vidole serikal kwa kutokulithamini swala la ajira kwa vijana. Mh Lowassa alienda mbali kwa kusema swala la ajira kwa vijana ni bomu linalongojea kulipuka.

Kutokana na maneno yake hayo leo Waziri husika amejibu mapigo. Take from me Serikali imemjibu kwa kishindo ila kisaikolojia waziri hajamtaja jina ila mwenye masikio haambiwi sikia, habari ndio hiyo. Atafute jingine.

Source TBC1
 
Hata jana ENL alirudia maneno hayo ya vijana na ajira! Nadhani waziri amejibu kufuatia alichosema jana ama juzi.
 
Najiuliza ni kwa nini serikali isubiri mtu atamke kwanza ndo ije na majibu ya zima moto?! kwa nini pasiwe na mrejesho katika wakati maalum walau wananchi wajue kinachoendelea?!

Mi nadhani ni moja ya viashiria vya uzembe!

Ila hata majibu yake hayajajitosheleza! nimemsikiliza kiasi ila naona ni siasa tu, au niseme wanajitetea! Alichokielezea kinajulikana na kimekuwa kikisemwa, namna ya kutekeleza ndo lingekuwa jibu sahihi; kwa mtazamo wangu!
 
Ajira kwa vijana ni bom kweli, mtu anamaliza chuo anatembea na bahasha hadi viatu vinaisha,hakuna ajira. Mbaya zaidi bodi wanajifanya kudai mikopo mtu atalipa hela ya bodi bila kazi. Serikal inadai vijana wajiajiri imewahi kufikiria hata kutoa mitaji kwa kundi hili la vijana. Hivi utafanya ujasiliamari bila mtaji inawezekana? Hilo bomu litalipuka kweli we ngoja wacheze na maisha ya watu.
 
Wahakikishe na Arumeru wanamjibu kwa kusimamia haki maana ni wazi mkwe wake atashindwa.
 
Huyo waziri katoa majibu legelege (mipasho) badala ya kujibu hoja thabiti ya fisadi EL
Ndio serikali ya JK ilivyo, mipasho mipasho mipasho.. (JK vs TUCTA, JK vs MAT, JK vs EL, JK/Pinda vs Magufuli, Manumba vs Mwakyembe/Sitta/Mponda/Nahodha, Simba vs Kilango, Rostam vs Nape, Mkapa vs Nyerere......)
 
kwa mtazamo wako serikali imejibu hoja?

Zile ajira milioni tano alizoahidi kikwete ziko wapi?

Bado serikali haiko makini na mimi nadhani uwezo wao wa kufikiri umefika mwisho
 
wanajuana hao.mwingine anatetea kitumbua mwingine anatafuta kitumbua wote sawa tu.
 
Tatizo la ndugu yetu huyu ni kutafuta umaarufu na kuonewa huruma katika mbio zake za 2015 ambazo nadhani zinaishia sakafuni. Sio kweli kwamba Serikali imelifumbia macho ila imezidiwa na aliyesababisha yote haya ni pamoja na yeye LOWASA NA ROSTAM NA WENZAO walioiibia Serikali hadi kufikia kushindwa kumudu wingi wa vijana wanaotafuta kazi mitaani.

Chukulia mfano mdogo tu wa Sioi Sumari, kwani katika mchakato si kulikuwepo vijana wazuri sana wa kutuwakilisha Arumeru lakini kwavile ni watoto wa masikini nani awape nafasi?
 
Leo ktk taarifa ya habari TBC1 Napenda kunuku maneno ya Mh Glaudensia Kabaka waziri wa Vijana na ajira. "Sii kweli kwamba serikali imesema imelifungia macho swala la ajira"
haitwi waziri wa vijana na ajira ila anaitwa waziri wa wazee na ajira sababu ni hizi
1.hana takwimu ya vijana walioajiriwa
2.hana takwimu ya vijana ambao hawana ajira
3.wazee ndio wanazidi kupata ajira mfano wakuu wa mikoa walioapishwa ikulu leo hii.

Angalizo:
Acha waendeleze mipasho tu ipo siku itawatokea puani fisadi mwenyewe kisha pima ipo siku itatokea noma
 
Hakuna asiyelijua hilo, lkn tujiulize chanzo pia ni wapi? Nani kasababisha yote haya? kwani mwaka 2008 alipokuwa PM hali ilikuwaje?
 
Kamjibu je sasa mbona unakimbilia kuweka source kama utadhani wote tumebahatika kuangalia hiyo habari
 
Ajira kwa vijana ni bom kweli, mtu anamaliza chuo anatembea na bahasha hadi viatu vinaisha,hakuna ajira. Mbaya zaidi bodi wanajifanya kudai mikopo mtu atalipa hela ya bodi bila kazi. Serikal inadai vijana wajiajiri imewahi kufikiria hata kutoa mitaji kwa kundi hili la vijana. Hivi utafanya ujasiliamari bila mtaji inawezekana? Hilo bomu litalipuka kweli we ngoja wacheze na maisha ya watu.

Si ndo maana wanajitahidi kutumia risasi za moto ili kuwapunguza na pindi litakapo lipuka ndo mtapigwa hizo risasi mpika mjute kuzaliwa Tz nchi iliyoko chini ya ccm
 
Huyo waziri katoa majibu legelege (mipasho) badala ya kujibu hoja thabiti ya fisadi EL
Ndio serikali ya JK ilivyo, mipasho mipasho mipasho.. (JK vs TUCTA, JK vs MAT, JK vs EL, JK/Pinda vs Magufuli, Manumba vs Mwakyembe/Sitta/Mponda/Nahodha, Simba vs Kilango, Rostam vs Nape, Mkapa vs Nyerere......)

Alafu uniambie ccm hapo itapona?
 
Huyo waziri katoa majibu legelege (mipasho) badala ya kujibu hoja thabiti ya fisadi EL
Ndio serikali ya JK ilivyo, mipasho mipasho mipasho.. (JK vs TUCTA, JK vs MAT, JK vs EL, JK/Pinda vs Magufuli, Manumba vs Mwakyembe/Sitta/Mponda/Nahodha, Simba vs Kilango, Rostam vs Nape, Mkapa vs Nyerere......)
Hahahahaa!!!!
Yani wao kwa wao sio??
Wanabishana tu tangu wa Nagy iwe
 
Hakuna asiyelijua hilo, lkn tujiulize chanzo pia ni wapi? Nani kasababisha yote haya? kwani mwaka 2008 alipokuwa PM hali ilikuwaje?
Siku hizi anajifanya anawajali sana vijana. Amejua lini kuwa vijana wanahitaji ajira? Tumuulize bilioni 111 tunazodaiwa na RICHMOND/DOWANS zingetoa ajira ngapi za vijana? naona speed yake ya kujifanya anauchungu na vijana inaongezeka kila tunapozidi kuikaribia 2015.
 
Back
Top Bottom