Serikali yamfungia Msanii kwa kuweka picha ya utupu Mtandaoni, na BASATA yawataka watayarishaji wa Muziki wajisajili

wasaniii kama wanao kiuka maadaili ya kitanzania wachukuliwe hatua Kali ili iwe fundisho kwa wengine!!!
kamwe tusiwachekee
 
Don't judge a book by its cover! Ni wazuri machoni , usitake kujua ubovu wao uko wapi.....
 
Msanii mchanga anayetafuta kiki kwa nguvu anayekwenda kwa jina na Pretty Kind amefungiwa kujishughulisha na shughuli za muziki kwa muda wa miezi sita (6). Kauli ya kufungiwa kwake imetolewa na Naibu Waziri mwenye dhamana na Sanaa Mhe. Juliana Shonza.

Msanii mwingine Gigy Money naye ametajwa na Waziri huyo kuwa ni miongoni mwa wasanii waliopost picha zao chafu kwenye mitandao. Aidha wasanii hao wameshirikiana kutoa wimbo wa Viwashawasha ambao ndani yake wamecheza nusu uchi.

Gigy Money bado hajaitikia with wa Waziri. Msanii Pretty Kind ameiomba radhi jamii ya Watanzania wamsamehe kwa kuvaa nguo za chumbani hadharani.
 
Maskini ka fruit kangu si katapauka sasa coz dau la 50 au laki huwa hakakibu sms labda kuanzia laki tano kwenda mbele
 
Hakuna aliye salama, wakitumaliza sisi watahamia kwenu. Hata viongozi wa dini walidhani wako salama, sasa imeonyesha hawako salama tena. LISSU'S VOICE
 
Hivi hayo yanayoitwa maadili ya mwafrika au mtanzania ni yapi? Maana nguo zililetwa na wazungu,

Asili ya mwafrika ni kukaa uchi na sehemu nyeti zilikuwa zinafunikwa na magome ya miti, sehemu zilizobaki zilikuwa wazi.

Labda turudi katika historia ya mwafrika maana kuna watu wanataka kuchanganya Asili ya mzungu na mwafrika

NI WAKATI WA KUHOJI SASA
 
Back
Top Bottom