Serikali yalipongeza Shirika la Nyumba (NHC) kwa kuokoa mabillioni ya pesa

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
10,327
6,850
Source: Apongeza shirika kuokoa mabilioni

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)kwa kuokoa mabillioni ya pesa yaliyokuwa yatumike kujenga Kitega Uchumi cha Mtukula kilichoko Misenyi mkoani Kagera

Mabula alitembelea mradi wa ujenzi wa jengo hilo wakati akiwa kwenye ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi katika Wilaya ya Misenyi mwishoni mwa wiki.

Alieleza kufurahishwa na gharama ndogo zilizotumika katika ujenzi wa kitega uchumi hicho cha NHC Mtukula baada ya kuelezwa na Mhandisi wa Ujenzi, George Shanel, kuwa hadi sasa, gharama yake imefikia Sh. milioni 800 wakati jengo limefikia asilimia 80 ya ujenzi.

Kiwango hicho ni tofauti na makadirio yaliyoelezwa awali kuwa lingegharimu Sh. bilioni tatu kama ujenzi huo ungefanywa na kampuni ambayo ingepewa zabuni.

Mabula alilipongeza shirika kwa kuokoa fedha nyingi kwa kutumia kampuni yake ya ujenzi na kutoa wito kwa taasisi mbalimbali nchini kulitumia shirika hilo kujenga ofisi na nyumba za watumishi kwa kuwa lina uwezo mkubwa katika ujenzi.

Jengo la kitega uchumi la NHC Mtukula liko mpakani mwa Tanzania na Uganda, litakapokamilika, litakuwa na ofisi mbalimbali zikiwamo za benki na maduka 36.

Mabula alisema kufanya vizuri kwa shirika hilo kumejionyesha katika kazi za ujenzi wa ofisi za wizara mbalimbali katika Mji wa Serikali Ihumwa mkoani Dodoma, linakojenga ofisi za wizara mbalimbali zikiwamo Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Wizara ya Fedha na
Mipango.

Alidai ujenzi unaotekelezwa na shirika hilo Ihumwa unakwenda kwa haraka na ubora wa uhakika.
 
Hata picha ndugu? Maana hao IPP Media nao wamekwepa kuweka picha yenye uzito wa habari badala yake wameweka picha ya mipasho ya Naibu Waziri akisaini mgongongoni mwa msaidizi wake.
 
Back
Top Bottom