Serikali yakiri kudaiwa na walimu shilingi bilioni 67.3

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Serikali imesema bado inadaiwa na walimu deni linalofikia Sh67.3 bilioni, ikiwamo mishahara.

Katika swali lake, mbunge huyo alitaka kujua Serikali imechukua hatua gani kumaliza madai ya walimu ya muda mrefu nchini.

Pia, alihoji kuhusu madai ya walimu waliosahihisha mitihani ya kidato cha nne mwaka jana ambao hawajalipwa hadi sasa.

Naibu Waziri huyo alisema Serikali imeendelea kulipa madeni ya walimu kupitia mamlaka zake kila yanapojitokeza.

“Mfano, Oktoba 2015, Serikali ililipa Sh20.1 bilioni na Februari mwaka huu imelipa Sh1.17 bilioni za madeni ya walimu nchi nzima,” alisema Jaffo.

Alitoa mchanganuo kuwa kati ya kiasi kinachodaiwa, alisema Sh17.5 bilioni ni madeni yasiyo ya mishahara wakati madeni ya mishahara yanafikia Sh49.8 bilioni ambayo kwa pamoja yanafanyiwa uhakiki.

Kuhusu malipo ya walimu waliofanya kazi ya kusahihisha mitihani alisema baadhi ya mikoa haijapeleka madai yao hadi sasa licha ya kuwa mwisho wa kupelekwa ilikuwa ni Aprili 15.

Alisema mikoa tisa tu ndiyo ilipeleka na kuitaja kuwa ni Mbeya, Mara, Tanga, Arusha, Kigoma, Lindi, Mtwara, Kilimanjaro na Iringa.

Alisema madeni hayo ya mikoa hiyo yanahakikiwa ili walimu walipwe.
 
Tangu niajiriwe mwaka 2012 bado wanahakiki,tuliambiwa kupanda madaraja ni mwezi wa pili,jana mshahara umeingia bila mabadiliko yoyote
Njoja niendelee kuwa mtoro na kuimarisha biashara zangu
 
Tangu niajiriwe mwaka 2012 bado wanahakiki,tuliambiwa kupanda madaraja ni mwezi wa pili,jana mshahara umeingia bila mabadiliko yoyote
Njoja niendelee kuwa mtoro na kuimarisha biashara zangu
Kwa hiyo siku yakifanyika mabadiliko ya mshahara vipindi ulivyokosa kufundisha watoto wetu utavifidia. Nakubaliana na Lissu, mzazi anayepeleka mtoto shule ya umma ni kwa sababu tu hana uwezo wa pesa.
 
Kwa hiyo siku yakifanyika mabadiliko ya mshahara vipindi ulivyokosa kufundisha watoto wetu utavifidia. Nakubaliana na Lissu, mzazi anayepeleka mtoto shule ya umma ni kwa sababu tu hana uwezo wa pesa.
Namimi nani atafidia riba ya fedha iliyocheleweshwa nilianza kazi kwa mshahara wa 469,200/= sikulipwa miezi miwili yaani 938,400/=
Kulingana na gharama za maisha mshahara umepanda hadi 716,000/= hayo madeni yalipwe kwa viwango vipya vya mshahara
Ungekuwa mwalimu usingeandika haya
Bado mshahara halali ulitakiwa kuwa 940,000/=kulingana na muda niliofundisha ambao ni miaka minne sasa
 
Back
Top Bottom