Serikali yaitaka chenji yake kashfa ya rada


jamadari

jamadari

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2010
Messages
295
Likes
12
Points
0
jamadari

jamadari

JF-Expert Member
Joined Feb 13, 2010
295 12 0
SERIKALI jana imetoa msimamo wake kuhusiana na ‘chenji ya Pauni milioni 28’ ambazo zinatarajiwa kurejeshwa nchini na serikali ya Uingereza baada ya kubainika kwamba Kampuni ya British Aerospace Engineering (BAE System) ilifanya udanganyifu katika kuiuzia Tanzania rada. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema jana kuwa fedha hizo zikirejeshwa zisipelekwe kwenye asasi zozote bali zirudi serikalini kwani zilikuwa ni za walipa kodi. Ingawa Waziri Membe alisema hadi sasa serikali haifahamu kiasi cha fedha zilizotajwa na Serikali ya Uingereza kwamba zitarudishwa nchini zipo taarifa kuwa Tanzania itarudishiwa Pauni milioni 28. Uchunguzi uliofanyika Uingereza kuhusu kashfa hiyo ya rada ulionesha kuwa Kampuni ya BAE Systems ilimlipa dalali zaidi ya Sh bilioni 12 kwa kufanikisha Serikali ya Tanzania kununua rada ya kijeshi kwa Sh bilioni 40. Kampuni hiyo ilikiri kosa na kuahidi kurudisha fedha Tanzania. Katika mazungumzo na waandishi wa habari Waziri Membe alisema ripoti ya uchunguzi wa tuhuma za rushwa katika ununuzi wa rada, inatarajiwa kufikishwa nchini wakati wowote kwa lengo la kutumiwa na serikali kuchukua hatua zinazostahili. Membe ambaye alikutana na mabalozi wa nje waliopo nchini na kuzungumzia mambo mbalimbali ikiwemo suala la rada na kuhusu uamuzi wa Bunge kufunga mjadala wa mkataba tata baina ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Kampuni ya Richmond Development LLC kabla ya kuzungumza na waandishi, Membe alisema ripoti ya Serikali ya Uingereza kupitia Makachero wa Uchunguzi wa Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) ndiyo itakayoiongoza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kukamilisha uchunguzi wake. Mkutano huo uliombwa na mabalozi hao. Alisema taarifa hiyo ndiyo itakayosaidia serikali namna ya kuhitimisha suala hilo katika utaratibu unaokubalika. “Tunasubiri ripoti. Tutatoa uamuzi kulingana na ripoti ya Uingereza,” Membe aliwaambia waandishi wa habari baada ya mkutano na mabalozi hao na akasema ripoti hiyo ambayo serikali ndiyo imeifuatilia kufahamu yaliyomo, italetwa wiki hii inayomalizika kesho. Kwa upande wa Tanzania, Mkurugenzi wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah hivi karibuni aliwaambia waandishi wa Dar es Salaam kwamba uchunguzi unaendelea na akasema kwamba ofisi yake inasubiri taarifa rasmi na nyaraka kutoka SFO ambayo ilikiri kuwapo rushwa katika ununuzi wa rada hiyo. Miongoni mwa wanaotuhumiwa katika suala hilo ni aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa wakati huo, Andrew Chenge na dalali, Saileth Vithlani. Katika hatua nyingine, Waziri Membe akizungumzia suala la Richmond, aliwaeleza mabalozi mchakato wote na namna ambavyo Bunge liliridhia kufunga mjadala kutokana na kuridhishwa na hatua za serikali katika kutekeleza maazimio ya Bunge. Mjadala ulifungwa katika Mkutano wa 18 wa Bunge ulioahirishwa wiki iliyopita. Aliwaambia kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakikugawanyika nchi nzima isipokuwa waliokuwa wamegawanyika ni wabunge juu ya suala hilo la Richmond. Alisema hata hivyo suala lenyewe pia limekwisha na kilichobaki ni serikali kukubali changamoto ya kutekeleza mambo yaliyobaki kulingana na maazimio ya Bunge. Kuhusu rushwa, Membe aliwaambia mabalozi hao kwamba vita dhidi ya ufisadi inafanyika nchini kwa kuzingatia maslahi ya taifa. Alisema katika kuonesha kuwa serikali iko makini katika hilo, zipo kesi mahakamani na nyingine uchunguzi wake unaendelea. Katika hatua nyingine, Membe amewafahamisha rasmi mabalozi wa nje kwa kuwataka wenye nia ya kufadhili vyama au wagombea binafsi katika Uchaguzi Mkuu ujao, wawe tayari kutangaza fedha watakazotoa na malengo yake ni nini kwa kuzingatia Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2009 ambayo inasubiriwa kusainiwa na Rais baada ya Muswada wake kupitishwa bungeni hivi karibuni. Vilevile aliwaeleza mabalozi uamuzi uliofikiwa wa kuwepo Serikali Shirikishi Zanzibar. Alisema kwa kuzingatia uamuzi wa Butiama, kutakuwa na makamu wawili wa Rais; mmoja akiwa ni wa chama kilichoshinda na mwingine kutoka chama cha upinzani. Aliwafafanulia pia suala la mgombea binafsi kwa kuwaambia Serikali haina pingamizi kuwepo isipokuwa suala hilo haliwezi kutekelezwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kwa kuwa linahitaji mabadiliko ya Katiba. Kwa upande wake, Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ((DRC), Juma Mpango ambaye ni Mkuu wa Mabalozi Nchini, alishauri Waziri Membe aweke utaratibu wa kukutana nao kila mwezi kwa lengo la kufahamishwa mambo mbalimbali yanayojiri kuliko kuegemea taarifa za vyombo vya habari pekee. http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=5823
 
RRONDO

RRONDO

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2010
Messages
33,199
Likes
35,092
Points
280
RRONDO

RRONDO

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2010
33,199 35,092 280
mazingaombwe?viini macho??tamthilia au maigizo?? hii rada ilinunuliwa na nani?kwa niaba ya nani?
 
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined
May 19, 2009
Messages
13,211
Likes
385
Points
180
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined May 19, 2009
13,211 385 180
Kuhusu rada: "No one can benefit from his own wrong!" Kuhusu mgombea binafsi, mwaka 1993 Mtikila alishinda kesi, mgombea binafsi akaruhusiwa na Mahakama Kuu, Serikali ikakata rufaa. Wakati rufaa iko pending Serikali ikapeleka haraka Muswada Bungeni ili kubadili Katiba kisha ikatoa rufaa Mahakama ya Rufani. Kwa hiyo hukumu ya Mahakama Kuu ikawa haina nguvu tena. Mtikila hakukata tamaa tena alipeleka kesi Mahakama Kuu na alishinda 2006! Serikali imekata rufaa Mahakama ya Rufani tena. Tangu 2006 Serikali haijakimbilia tena Bungeni kupeleka Muswada wa kubadili katiba kama ilivyofanya miaka ya 90 na kudai ETI muda hautoshi! Mbona kwenye kesi ya mwanzo muda ulitosha? Kwa nini tangu 2006 hadi 2010 eti muda hautoshi? Wanataka wapewe muda hadi lini?
 
B

Bulesi

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2008
Messages
7,039
Likes
1,233
Points
280
B

Bulesi

JF-Expert Member
Joined May 14, 2008
7,039 1,233 280
Utata wa wapi hizo hela za rada zitakakokwenda unatoka wapi? Hawa wahuni walituingiza mkenge wa kununua hiyo rada kwa bei ya kuruka lakini serikali haikuwa na fedha taslimu za kulipia ndio maana walikwenda kukopa Barclays Bank na Andy Chande alifacilitate transaction hiyo. Sasa kama hizo hela tulikopa na nadhani kwa riba kubwa tu kwanini zitakaporudishwa tusizitumie kulipia mkopo huko Barclays Bank? In one way or another huo mkopo wa Barclays lazima ulipwe na tukiliquidate deni hilo mapema so much the better for the country.
 
A

August

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2007
Messages
4,641
Likes
802
Points
280
A

August

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2007
4,641 802 280
halafu hela inayo takiwa kulipwa au ilioamriwa kulipa ni kidogo kuliko kilicho ongezwa, na kiliamriwa na waamerika kwa makubaliano na sfo , je pccb wanafanya nini kuipiga penalty hiyo bae system kama 200% ya kiasi kilicho ongezwa? halafu memba anajidai kudandia issue iliyo amriwa amerika/uk kwamba fedha zisiende kwenye ngo bali zirudishwe serikali .
 

Forum statistics

Threads 1,236,237
Members 475,029
Posts 29,251,058