Serikali yafuta umiliki wa mashamba 17

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
12439266_1022243414506783_4246458994422264260_n.jpg
 
Kibaha. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema Serikali imefuta umiliki wa mashamba 17 ambayo hayajaendelezwa katika Mkoa wa Pwani.

Akizungumza na viongozi wa mkoa huo, Lukuvi alisema Serikali imefuta mashamba hayo baada ya mkoa kutoa mapendekezo ya kutaka yafutwe kwa sababu hayajaendelezwa.

“Baada ya kupata mapendekezo ya mkoa tumefuta miliki ya mashamba lakini wamiliki ni wananchi wa kawaida, mbona vigogo wenye mashamba yasiyoendelezwa hamjawagusa, mnawaogopa? ” aliwahoji viongozi hao.

Lukuvi aliagiza ukaguzi ufanyike kwenye mashamba yote mkoani na kutoa mapendekezo kwa wizara ili yafutwe bila kuangalia cheo wala rangi ya mtu.

Alisema migogoro ya ardhi haiwezi kumalizika kama viongozi watakuwa wanafanya kazi kwa kuangalia vyeo vya watu.

“Msimuogope mtu hata kama ni kigogo lakini msimuonee mtu, tendeni haki,” alisema.

Lukuvi alisema kuna wamiliki 35 wa mashamba mkoani humo ambao wametumia hati za mashamba hayo kukopa mamilioni ya fedha benki, lakini fedha hizo wamezitumia kwenye miradi mingine isiyo na uhusiano wa mashamba hayo.

Alisema pamoja na kukopa fedha hizo, lakini mashamba waliyotumia kupata mikopo wameyatelekeza bila kuyaendeleza.

“Wako watu wamekopa kwa kutumia mashamba ya Mkoa wa Pwani lakini fedha walizopata wamekwenda kujenga nyumba za kupangisha Kigamboni (Dar es Salaam) na mashamba hawayaendelezi tutawanyang’anya,” alisema.

Lukuvi alisema atatoa orodha ya watu hao kwa uongozi wa mkoa ili uweze kuyakagua na kutoa taarifa kwa wizara.

“Hatuwezi kuwatajirisha watu wa Dar es Salaam kwa kutumia mashamba ya Mkoa wa Pwani,” alisema.

Lukuvi alitoa orodha ya mashamba 50 ambayo yamenunuliwa kwenye vijiji vya mkoa huo, lakini hayajaendelezwa na kusababisha migogoro ya ardhi.

“Kutoendeleza mashamba kunasababisha migogoro ya ardhi kwani hivi sasa kuna watu wanayavamia,” alisema.

Bei elekezi ya viwanja

Waziri alisema wizara itatoa bei elekezi katika uuzaji wa viwanja kwa lengo la kupunguza bei.

Alisema hivi sasa halmashauri zimekuwa zikichukua mashamba na kupima viwanja na kuviuza kwa mamilioni ya fedha ambayo si rahisi kwa mwananchi wa kawaida kumudu.

Alisema matokeo yake, viwanja hivyo vimekuwa vikinunuliwa na matajiri kwa malengo ya kuviuza kwa bei kubwa huku watu wa kawaida wakiendelea kujenga kwenye maeneo yasiyopimwa.

“Halmashauri msifanye biashara katika viwanja, hii ni huduma sasa tunaweka bei elekezi ili kila mwananchi aweze kununua,” alisema.

Alizitaka halmashauri zilizochukua mashamba ya watu na kuyapima viwanja kuwalipa fidia kabla ya Juni.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Mgeni Baruani alimueleza waziri kwamba mkoa huo una migogoro ya ardhi hasa zile zinazopakana na Mkoa wa Dar es Salaam

Source:- Mwananchi
 
Hivu hawa wanao piga picha gazeti na kuweka hapa Jf wana maana gani. Ni vyema muwe mnaweka na muhtasari wa kilichopo kwenye hilo gazeti. Sio mnaweka kivhwa cha habari bila maelezo.
 
Yaani watu tumeumizwa kweli kweli tumaiziwa arthi ya nchi yako bei utafikiri mgeni...
Mbaya hio kuthulumia eneo we watanunua kwa 500,000 wao wanapima na kuuza bei kubwa sana utasikia sq mita 10,000
 
Yaani watu tumeumizwa kweli kweli tumaiziwa arthi ya nchi yako bei utafikiri mgeni...
Mbaya hio kuthulumiwa eneo lako we we watanunua kwa 500,000 wao wanapima na kuuza bei kubwa sana utasikia sq mita 10,000
 
Kibaha. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema Serikali imefuta umiliki wa mashamba 17 ambayo hayajaendelezwa katika Mkoa wa Pwani.

Akizungumza na viongozi wa mkoa huo, Lukuvi alisema Serikali imefuta mashamba hayo baada ya mkoa kutoa mapendekezo ya kutaka yafutwe kwa sababu hayajaendelezwa.

“Baada ya kupata mapendekezo ya mkoa tumefuta miliki ya mashamba lakini wamiliki ni wananchi wa kawaida, mbona vigogo wenye mashamba yasiyoendelezwa hamjawagusa, mnawaogopa? ” aliwahoji viongozi hao.

Lukuvi aliagiza ukaguzi ufanyike kwenye mashamba yote mkoani na kutoa mapendekezo kwa wizara ili yafutwe bila kuangalia cheo wala rangi ya mtu.

Alisema migogoro ya ardhi haiwezi kumalizika kama viongozi watakuwa wanafanya kazi kwa kuangalia vyeo vya watu.

“Msimuogope mtu hata kama ni kigogo lakini msimuonee mtu, tendeni haki,” alisema.

Lukuvi alisema kuna wamiliki 35 wa mashamba mkoani humo ambao wametumia hati za mashamba hayo kukopa mamilioni ya fedha benki, lakini fedha hizo wamezitumia kwenye miradi mingine isiyo na uhusiano wa mashamba hayo.

Alisema pamoja na kukopa fedha hizo, lakini mashamba waliyotumia kupata mikopo wameyatelekeza bila kuyaendeleza.

“Wako watu wamekopa kwa kutumia mashamba ya Mkoa wa Pwani lakini fedha walizopata wamekwenda kujenga nyumba za kupangisha Kigamboni (Dar es Salaam) na mashamba hawayaendelezi tutawanyang’anya,” alisema.

Lukuvi alisema atatoa orodha ya watu hao kwa uongozi wa mkoa ili uweze kuyakagua na kutoa taarifa kwa wizara.

“Hatuwezi kuwatajirisha watu wa Dar es Salaam kwa kutumia mashamba ya Mkoa wa Pwani,” alisema.

Lukuvi alitoa orodha ya mashamba 50 ambayo yamenunuliwa kwenye vijiji vya mkoa huo, lakini hayajaendelezwa na kusababisha migogoro ya ardhi.

“Kutoendeleza mashamba kunasababisha migogoro ya ardhi kwani hivi sasa kuna watu wanayavamia,” alisema.

Bei elekezi ya viwanja

Waziri alisema wizara itatoa bei elekezi katika uuzaji wa viwanja kwa lengo la kupunguza bei.

Alisema hivi sasa halmashauri zimekuwa zikichukua mashamba na kupima viwanja na kuviuza kwa mamilioni ya fedha ambayo si rahisi kwa mwananchi wa kawaida kumudu.

Alisema matokeo yake, viwanja hivyo vimekuwa vikinunuliwa na matajiri kwa malengo ya kuviuza kwa bei kubwa huku watu wa kawaida wakiendelea kujenga kwenye maeneo yasiyopimwa.

“Halmashauri msifanye biashara katika viwanja, hii ni huduma sasa tunaweka bei elekezi ili kila mwananchi aweze kununua,” alisema.

Alizitaka halmashauri zilizochukua mashamba ya watu na kuyapima viwanja kuwalipa fidia kabla ya Juni.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Mgeni Baruani alimueleza waziri kwamba mkoa huo una migogoro ya ardhi hasa zile zinazopakana na Mkoa wa Dar es Salaam

Source:- Mwananchi
Tunakoelekea sasa siko kabisa. Huo mkopo umetokana na fund special ya kuendeleza hayo mashamba? Au mtu kaweka shamba kama collateral? Mimi kama mtanzania nina haki ya kutumia kitu changu ninachokimiliki halali sehemu yeyote Tanzania au hata cha mtu mwingine (kwa maelewano) kupata mkopo. Lakini endapo mikataba ya kununua hayo mashamba ili stipulate au kama kuna sheria inayotaka sehemu iendelezwe ndani ya kipindi fulani sasa hiko ni kitu kingine.

Akimaliza uko aende Oysterbay. Tunavyosikia terms za mikataba ya kununua nyumba za serikali zimekiukwa.

Sio kila mtanzania ni fisadi au mpiga dili. Ukinunua kiwanja kwanza unatulia, unajipanga upya. Ukishadunduliza vihela vyako unaenda kwenye msingi.
 
Back
Top Bottom