Serikali yafunga ushahidi kesi ya Ponda

Serikali yafunga ushahidi kesi ya Ponda

Jangakuu

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2012
Posts
513
Reaction score
221
na Happiness Katabazi

UPANDE wa jamhuri katika kesi ya uchochezi na kuiba malighafi zenye thamani ya sh milioni 59 inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, na wenzake 48, umefunga ushahidi katika kesi hiyo. Hayo yalisemwa jana na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka, mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, muda mfupi baada ya shahidi wa 17 upande wa jamhuri D/C F8586 Ismail wa kituo cha polisi Chang'ombe kumaliza kutoa ushahidi wake.

Hadi jana upande wa jamhuri ulikuwa umeleta mashahidi 17 na vielelezo 13 ambavyo vilipokelewa mahakamani. Baada ya wakili Kweka kutoa maelezo hayo wakili wa Ponda, Juma Nassor, aliomba mahakama iwapatie muda hadi Machi 4 ili wakajiandae kuwasilisha maombi ya wateja wao 49 kuwa hawana kesi ya kujibu.

Hata hivyo Hakimu Nongwa alisema jukumu la kupanga tarehe ya kufanya majumuisho ni vyema ikaachiwa mahakama na hakimu huyo akatoa amri kuwa majumuisho hayo yatafanyika kesho, Februali 27 na akautaka upande wa utetezi uwe wa kwanza kuwasilisha majumuisho yao kwa njia ya mdomo. Kabla ya jamhuri kufunga maelezo yake mahakama ilisikiliza mashahidi watatu ambao ni shahidi wa 15, F3929 D/C , Constebo Eliaeli (35), shahidi wa 16 Sajenti Amos wa kituo cha polisi Kati na shahidi wa 17 askari mpelelezi Na. F8586 D/C Ismail.

Shahidi wa 17, D/C Ismail aliieleza mahakama kuwa Oktoba 17, mwaka jana, alipewa kazi na mkuu wake wa kazi na kati ya saa 2-9 alasiri alikuwa kituo cha polisi Kijinyoma akiwahoji washtakiwa ambao walikamatwa katika kiwanja cha Chang'ombe Marskas wakikabiliwa na makosa ya kuingia kwa jinai katika kiwanja hicho.

Ismail alidai kumhoji mshtakiwa Fiswaa ambaye alimweleza kuwa kati ya tarehe, mwezi na saa isiyofahamika akiwa nyumbani kwake Mlandazi, mkoani Pwani, akiwa anasikiliza Redio Iman, alisikia tangazo lililokuwa likiwataka waumini wa dini ya Kiislamu kwenda kuongeza nguvu ya kujenga msikiti katika kiwanja kilichovamiwa cha Chang'ombe Markas ambacho ni mali ya Waislamu na si BAKWATA.

Shahidi huyo alidai kuwa mshtakiwa huyo alimweleza kuwa aliitikia wito huo na kufunga safari toka Mlandizi kuja kuungana na wenzake ambapo kiongozi wao walipokuwa kwenye kiwanja hicho ni mshtakiwa wa kwanza ambaye ni Ponda.

"Sululu, mapanga vilitumika kama vifaa vya kujengea msikiti wa muda katika kiwanja hicho na ndipo usiku wa kuamkia Oktoba 17, mwaka jana, tukiwa tumekaa kwenye kiwanja hicho nikasikia sauti ikisema, tupande kwenye gari na sikuwa na kumbukumbuku yoyote," alidai Ismail.

Maelezo ya mshtakiwa huyo yalipokelewa kama kilelezo cha 13 na hakikupingwa na mawakili wa utetezi. Shahidi wa 16, Station Sajenti Amos, alidai kuwa Oktoba 17 mwaka jana alipewa jukumu la kumhoji mshtakiwa Hussein Ally ambaye alimweleza kuwa alipokea maelekezo kutoka kwa masheikh wake wa msikiti wa Kinyerezi yakimtaka afike katika kiwanja cha Markas na alienda na kukutana na wenzake ambapo walianza kufanya kazi wakiongozwa na Ponda katika kiwanja ambacho tayari mashahidi wengine toka BAKWATA walisema ni mali ya kampuni ya Agritanza Ltd siyo BAKWATA tena.

Aidha shahidi wa 15 D/C Konstebo Elieli alidai kuwa Oktoba 17, mwaka jana, alipewa jukumu na mkubwa wake wa kazi la kuandika maelezo ya mshtakiwa Mohamed Ramadhan ambaye alimweleza kuwa siku hiyo yeye alikwenda kusali katika eneo la kiwanja hicho akitoka Oysterbay Dar es Salaam.

Elieli alieleza kuwa mshtakiwa huyo alimweleza kuwa alikwenda kusali swala ya alfajiri hapo Chang'ombe Markas kwa sababu alikuwa anauguliwa na ndugu yake anayeishi Keko ambapo hakwenda kusali misikiti ya Keko kwa vile hali ya usalama ilikuwa mbaya.

"Mshtakiwa akanieleza eti baada ya kusali hapo alfajiri ya Oktoba 17, mwaka jana, ndiyo ghafla alishtukia anakamatwa na polisi. Nilipomhoji kama analifahamu vuguvugu la Waislamu kudai haki zao, mshtakiwa alikubali na kwamba pale alikuwa katika kutetea na kudai haki yao ya kurejeshewa kiwanja kile ambacho ni mali ya Waislamu na si BAKWATA," alidai Elieli. Hata hivyo mahakama ilikataa kupokea maelezo hayo kama kielelezo kwa sababu ya dosari nyingi za kisheria.



Source; Tanzania Daima
 
kumbe Ponda mbali ya ugaidi pia mwizi??hawa watu wanatumia dini ku cover maovu yao??Dini zote huwa zinahubiri amani., upendo ila wachache wanabadili maandiko ili kukidhi maovu yao!
 
kumbe Ponda mbali ya ugaidi pia mwizi??hawa watu wanatumia dini ku cover maovu yao??Dini zote huwa zinahubiri amani., upendo ila wachache wanabadili maandiko ili kukidhi maovu yao!
Kuwa na adabu, imeandikwa anakabiliwa na tuhuma za wizi, hizo tuhuma bado hazijathibitika pasipo na shaka. Mwizi baba ako..!
 
Kuwa na adabu, imeandikwa anakabiliwa na tuhuma za wizi, hizo tuhuma bado hazijathibitika pasipo na shaka. Mwizi baba ako..!

Wewe na wewe UAMSHO nini maana kitambulisho chenu matusi, ila CIA wapo safari mtanyolea bati,.waislamu wenzako wamethibitisha pasi na shaka kuwa alipora mali wewe unamtetea?? au na wee ni mshirika??,.ila nashukuru pia umekanusha la wizi ila ugaidi umeli accomodate!
 
Kuwa na adabu, imeandikwa anakabiliwa na tuhuma za wizi, hizo tuhuma bado hazijathibitika pasipo na shaka. Mwizi baba ako..!
Acha hasira.


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Wewe na wewe UAMSHO nini maana kitambulisho chenu matusi, ila CIA wapo safari mtanyolea bati,.waislamu wenzako wamethibitisha pasi na shaka kuwa alipora mali wewe unamtetea?? au na wee ni mshirika??,.ila nashukuru pia umekanusha la wizi ila ugaidi umeli accomodate!
Te teh teh teh..! Naomba nikanushe na hilo la ugaidi..! Pia hili la kunyolea bati ngoja nilifanyie kazi ili tunyoe kwa bati lenye makali lising'oe mavituzi..!
 
Atakma na ugaidi wake sweka ndani chezea serikali weye, hapo majini hayana nafasi tena too late.
 
soon dola ya kiislamu itaenea middle east, west africa, east africa and all over the world so jiandaeni wneye chuki na uislam khilafa is coming
 
  • Thanks
Reactions: lum
na happiness katabazi

upande wa jamhuri katika kesi ya uchochezi na kuiba malighafi zenye thamani ya sh milioni 59 inayomkabili katibu wa jumuiya na taasisi za kiislamu, sheikh ponda issa ponda, na wenzake 48, umefunga ushahidi katika kesi hiyo. Hayo yalisemwa jana na wakili mwandamizi wa serikali, tumaini kweka, mbele ya hakimu mkazi victoria nongwa wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu dar es salaam, muda mfupi baada ya shahidi wa 17 upande wa jamhuri d/c f8586 ismail wa kituo cha polisi chang’ombe kumaliza kutoa ushahidi wake.

Hadi jana upande wa jamhuri ulikuwa umeleta mashahidi 17 na vielelezo 13 ambavyo vilipokelewa mahakamani. Baada ya wakili kweka kutoa maelezo hayo wakili wa ponda, juma nassor, aliomba mahakama iwapatie muda hadi machi 4 ili wakajiandae kuwasilisha maombi ya wateja wao 49 kuwa hawana kesi ya kujibu.

Hata hivyo hakimu nongwa alisema jukumu la kupanga tarehe ya kufanya majumuisho ni vyema ikaachiwa mahakama na hakimu huyo akatoa amri kuwa majumuisho hayo yatafanyika kesho, februali 27 na akautaka upande wa utetezi uwe wa kwanza kuwasilisha majumuisho yao kwa njia ya mdomo. Kabla ya jamhuri kufunga maelezo yake mahakama ilisikiliza mashahidi watatu ambao ni shahidi wa 15, f3929 d/c , constebo eliaeli (35), shahidi wa 16 sajenti amos wa kituo cha polisi kati na shahidi wa 17 askari mpelelezi na. F8586 d/c ismail.

Shahidi wa 17, d/c ismail aliieleza mahakama kuwa oktoba 17, mwaka jana, alipewa kazi na mkuu wake wa kazi na kati ya saa 2-9 alasiri alikuwa kituo cha polisi kijinyoma akiwahoji washtakiwa ambao walikamatwa katika kiwanja cha chang’ombe marskas wakikabiliwa na makosa ya kuingia kwa jinai katika kiwanja hicho.

Ismail alidai kumhoji mshtakiwa fiswaa ambaye alimweleza kuwa kati ya tarehe, mwezi na saa isiyofahamika akiwa nyumbani kwake mlandazi, mkoani pwani, akiwa anasikiliza redio iman, alisikia tangazo lililokuwa likiwataka waumini wa dini ya kiislamu kwenda kuongeza nguvu ya kujenga msikiti katika kiwanja kilichovamiwa cha chang’ombe markas ambacho ni mali ya waislamu na si bakwata.

Shahidi huyo alidai kuwa mshtakiwa huyo alimweleza kuwa aliitikia wito huo na kufunga safari toka mlandizi kuja kuungana na wenzake ambapo kiongozi wao walipokuwa kwenye kiwanja hicho ni mshtakiwa wa kwanza ambaye ni ponda.

“sululu, mapanga vilitumika kama vifaa vya kujengea msikiti wa muda katika kiwanja hicho na ndipo usiku wa kuamkia oktoba 17, mwaka jana, tukiwa tumekaa kwenye kiwanja hicho nikasikia sauti ikisema, tupande kwenye gari na sikuwa na kumbukumbuku yoyote,” alidai ismail.

Maelezo ya mshtakiwa huyo yalipokelewa kama kilelezo cha 13 na hakikupingwa na mawakili wa utetezi. Shahidi wa 16, station sajenti amos, alidai kuwa oktoba 17 mwaka jana alipewa jukumu la kumhoji mshtakiwa hussein ally ambaye alimweleza kuwa alipokea maelekezo kutoka kwa masheikh wake wa msikiti wa kinyerezi yakimtaka afike katika kiwanja cha markas na alienda na kukutana na wenzake ambapo walianza kufanya kazi wakiongozwa na ponda katika kiwanja ambacho tayari mashahidi wengine toka bakwata walisema ni mali ya kampuni ya agritanza ltd siyo bakwata tena.

Aidha shahidi wa 15 d/c konstebo elieli alidai kuwa oktoba 17, mwaka jana, alipewa jukumu na mkubwa wake wa kazi la kuandika maelezo ya mshtakiwa mohamed ramadhan ambaye alimweleza kuwa siku hiyo yeye alikwenda kusali katika eneo la kiwanja hicho akitoka oysterbay dar es salaam.

Elieli alieleza kuwa mshtakiwa huyo alimweleza kuwa alikwenda kusali swala ya alfajiri hapo chang’ombe markas kwa sababu alikuwa anauguliwa na ndugu yake anayeishi keko ambapo hakwenda kusali misikiti ya keko kwa vile hali ya usalama ilikuwa mbaya.

“mshtakiwa akanieleza eti baada ya kusali hapo alfajiri ya oktoba 17, mwaka jana, ndiyo ghafla alishtukia anakamatwa na polisi. Nilipomhoji kama analifahamu vuguvugu la waislamu kudai haki zao, mshtakiwa alikubali na kwamba pale alikuwa katika kutetea na kudai haki yao ya kurejeshewa kiwanja kile ambacho ni mali ya waislamu na si bakwata,” alidai elieli. Hata hivyo mahakama ilikataa kupokea maelezo hayo kama kielelezo kwa sababu ya dosari nyingi za kisheria.



source; tanzania daima

wakili mkirsito. Jaji mkiristo dhidi ya sheikh. Angalikuwa padri upesi wangalisema hana kesi ya kujibu. Mwalimu nyerere mungu amrehemu. Katuachia matatizo malkubwa ya udini hapa tanzania
 
wewe na wewe uamsho nini maana kitambulisho chenu matusi, ila cia wapo safari mtanyolea bati,.waislamu wenzako wamethibitisha pasi na shaka kuwa alipora mali wewe unamtetea?? Au na wee ni mshirika??,.ila nashukuru pia umekanusha la wizi ila ugaidi umeli accomodate!
wameletwa na makanisa? Acha ujuha wewe. Pakitokea machafuko waislam vs wakiristo cia hawatakuwa upande wakiristo. Mbona rwanda walikimbia wakaachia wauane wenyewe kwa wenyewe? Halau unajiita mkiristo msomi
 
Acha Matusi wewe!!! Tuhuma? Wakati gaidi jizi Ponda liliiba!!!! Nataka serikali impige vua 20 ili iwe mfano kwa magaidi wenzake Kama Ilunga

Ww ndio mwizi fisadi mpenda rushwa
Shekh atatoka siku moja na mapambano yanaendelea maana wanaomfuata ni wengi waisilamu wamefumbulia mengi na huyu jamaaa.
M
 
kweli mkuu, na ndio maana askari hawafany masihara kukaa nae mbali. Pamoja na kumfunga mbingu


si unajua makafiri huwa woga sana wakimuona muislam. wanaweza wakawa 100, marisadi tele, mbwa mizinga. lkn wakimuona muislam 1 wanaona kama wapo watu 1000. huu ni moja ya miujiza mikubwa hapa duniani
 
Hizo ni kelele za chura haziwazui tembo kunywa maji.....Wataangaika saana mwisho wa yote PONDA ataachiwa huru na baadae Sheikh PONDA ataifungulia serikali kesi ya kumdharirisha na atalipwa mahela mengitu na harakati zitaendelea km kawa...Hakuna anaeweza kumfunga Sheikh PONDA serikali inajua impact yake mwanzo mwisho nini inakifanya sasa ni kuwatishia kisaikolojia....FUNGA UONE MAJIVU YATAKVYOKUA SEHEMU YA MICHANGA
 
Hizo ni kelele za chura haziwazui tembo kunywa maji.....Wataangaika saana mwisho wa yote PONDA ataachiwa huru na baadae Sheikh PONDA ataifungulia serikali kesi ya kumdharirisha na atalipwa mahela mengitu na harakati zitaendelea km kawa...Hakuna anaeweza kumfunga Sheikh PONDA serikali inajua impact yake mwanzo mwisho nini inakifanya sasa ni kuwatishia kisaikolojia....FUNGA UONE MAJIVU YATAKVYOKUA SEHEMU YA MICHANGA
hiyo impact kama ni negative wala siyo kitu cha kujisifia kabisa.
mtawajumuisha mpaka na wale wasio na hatia.
 
Redio iman imetumika ktk uhalifu
kumbe Ponda mbali ya ugaidi
pia mwizi??hawa watu wanatumia dini ku cover maovu yao??Dini zote huwa
zinahubiri amani., upendo ila wachache wanabadili maandiko ili kukidhi
maovu yao!
 
wakili mkirsito. Jaji mkiristo dhidi ya sheikh. Angalikuwa padri upesi wangalisema hana kesi ya kujibu. Mwalimu nyerere mungu amrehemu. Katuachia matatizo malkubwa ya udini hapa tanzania

huwezi kuchangia bila kuweka udini we mfuasi wa sheikh Ponda?
 
Back
Top Bottom