Serikali yafanya kufuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yafanya kufuru

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng'wanza Madaso, Oct 11, 2009.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Serikali yafanya kufuru Sunday, 11 October 2009 15:04 *Yanunua mashangingi 80 kwa 15/-bilioni
  *Ni baada ya Pinda kutaka ibane matumizi

  Na Edmund Mihale

  WAKATI Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda, akizitaka wizara, idara na taasisi mbalimbali za Serikali kuacha kununua magari ya kifahari, Serikali imenunua magari ya kifahari 80 maarufu kama mashangingi katika kipindi cha mwaka mmoja.

  Agizo hilo la Bw. Pinda ni la pili kutolewa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tangu ateuliwe kuishika madaraka hayo. Hata juzi alipokwenda nchini Indonesia alipendekezewa ziwe zinavaliwa nguo za batik alizovaa kiongozi wa nchi hiyo, alipoeda kumtembelea. Bw. Pinda alisema na yeye na msafara wake waliamua kuvaa mavazi ya aina hiyo na kuondokana na suti.

  Uchunguzi ulifanywa na Majira Jumapili na kuthibitishwa na mmoja wa watumishi Idara ya Ufundi iliyo chini ya Wizara ya Miundombinu umebaini magari hayo aina ya Toyota Land Cruiser VX V8 ambayo ni toleo jipya tayari yameanza kutumika katika wizara, idara na taasisi mbalimbali za serikali.

  Magari hayo ambayo awali yalikuwa yakiuzwa sh.112,496,497 kabla hayafanyiwa marekebisho na kuwa ya kisasa zaidi, sasa yanauzwa sh.187,760,261.

  Uchunguzi huo umebaini magari yote 80 yameigarimu serikali jumla ya Sh bilioni 15. 02 ikiwa ni nje ya gharama za mafuta, vipuri na matengenezo. Endapo mawaziri wote 47 watachangamkia magari hayo, Serikali italazimika kutumia sh. 8,824,732,267, mbali na viongozi wengine wa taasisi za umma wanaotamani kutembelea magari hayo mapya.

  Gharama hiyo itakuwa na ongezeko la sh. bilioni mbili ikilinganishwa na gharama za magari yaliyonunuliwa kwa ajili ya mawaziri na Naibu mawaziri 61 mwaka 2006 ambapo zaidi ya sh .bilioni 6 zilizotumika kwa ajili hiyo. Rais Kikwete alilazimika kupunguza ukubwa wa baraza lake la mawaziri mwaka juzi ili kuongeza ufanisi na kupunguza gharama serikalini.

  Magari mengine yanayotumiwa na serikali nayo yamepanda bei kama Land Cruiser Hard Top milango mitano ambalo sasa linauzwa sh 106,918,103 wakati awali lilikuwa likiuzwa kwa sh. milioni 70 na Toyota Land Cruiser lenye uwezo kwa kuchukua abiria 13 linauzwa kwa sh. 99,556,166. Awali liliuzwa kwa sh milioni 60.

  Wakati viongozi na wakuu wa taassisi na idara mbalimbali za serikali wakishindana kutumia magari hayo ya kifahari, tayari baadhi ya Idara kama Mahakama imeshatoa malalamiko kutokana na kuwa na bajeti ndogo hali ambayo inashusha utendaji wa wa idara hiyo nyeti.

  Mbali na Iadara ya Mahakama, bajeti ya Wizara ya Afya na Utawi wa Jamii,nayo bado ni ndogo hali inayosababisha kukosekana kwa vitendea kazi huku idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi vikiwa bado tishio.

  Kwa sasa bajeti ya sekta ya afya ni asilimia 11 na ili hali iwe shwari katika sekta hiyo, bajeti yake inapaswa kufikia asilimia 15.

  Uchunguzi huo umebaini kuwa idara ya mahakama hadi sasa inatumia teknolojia ya kizamani katika undeshaji wa kesi, usafiri duni na malazi kwa watendaji wake. Hadi sasa baadhi ya majaji wamekuwa wakitumia magari ya kukodi ili kufanikisha majukumu mengine ya kitaifa. Hata waliokuwa na magari, hayana hali nzuri kutokana kutumika kwa zaidi ya miaka 10 hadi 15 na wengine wakiwa hawana nyumba za kuishi.

  Malalamiko mengine ni upungufu wa walimu katika shule za kata ambapo Majira Jumapili imebaini kuwa shule nyingi za kata hazina walimu. Baadhi ya shule zina wanafunzi hadi 2,000 kwa shule moja yenye walimu wanne ikiwa na uhaba wa madawati, vitabu maabara na nyenzo nyingine.

  Chanzo cha habari kutoka ndani Wizara ya Miundombinu kiliambia Majira Jumapili kuwa kilio Bw. Pinda kutaka kusitishwa kwa ununuzi wa magari hayo ni sawa machozi ya samaki ndani ya maji.

  Alisema kimsingi maombi ya ununuzi wa magari hayo hufanywa kupitia katika Wizara ya Miundombinu, Idara ya Ufundi na baada ya kupitiwa kwa kina maombi hayo hupelekwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Philmon Luhanjo ambaye ni mtu pekee aliye na mamlaka ya kupitisha au kukataa kwa maombi hayo.

  Hata hivyo chanzo hicho kilisema kuwa utaratibu wa mwanzo ulikuwa kwa mtindo wa kuachiana magari kwa mtindo wa kigogo wa juu kulitumia kwa kilometa kadha na kumwachia aliye chini yake, lakini kwa sasa jambo hilo limeshindikana kwa kuwa kila mkuu wa idara amekuwa akiomba gari jipya na kupewa tofauti na ilivyo mwanzo.

  "Magari ya mawaziri yanatembea kwa kilometa fulani kutokana na madaraka yake hivyo kilometa hizo zikiisha humuachia gari hiyo naibu wakea au katibu makuu ambaye naye ana kilometa zake na mwisho wake gari hilo hubakia kuwa la kusambaza barua na kama limechoka zaidi huuzwa kwa njia ya mnada" alisema.

  Source:Majira

  My take: Hii ndio Tanzania yetu ya kusema bila vitendo. Je kuna haja ya kuendelea kumsikiliza Mheshimiwa Pinda kwa kila analoongea? Kama kashindwa kutekeleza hili aliloliongea mara zaidi ya moja je ni lipi atakaloongea na kutekeleza?
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,312
  Likes Received: 1,783
  Trophy Points: 280
  Nafikiri tunasahau kuwa kama tunachosema hakiendani na tunachofanya basi suala la credibility yetu linawekwa kwenye mizani.Hapa Mheshimiwa sijui anataka kusema kuwa walio chini yake wana nguvu kuliko yeye mpaka kupindisha maamuzi ambayo alikwisha toa au ndio kusema tuu ili kufurahisha genge. Uzuri siku hizi yote yanaandikwa. Kama wanahaidi ili siasa zifanyike tu ipo siku wataulizwa kulikoni
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,061
  Likes Received: 5,552
  Trophy Points: 280
  Nyie amumjui yule tapeli wa kisiasa

  namshauri akae kimya asijiaribie;ukiwa kwenye syste ya majambazi lazima ufwate majambazi
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  pinda hawezi kuheshimiwa na walio chini yake kwa kuwa anakurupuka mno kutoa maagizo.Huyu alishawahi kusema semina zote lazima zipate kibali chake nani alitimiza hilo
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,061
  Likes Received: 5,552
  Trophy Points: 280
  kaka mbona hiyo sio kufuru ushaona walichonunu mwaka jana..??
  walichofanya kupunguza idadi ya magari na kuongeza uthamani wa magari
  i like stupid gov like this
   
Loading...