Naomba ninene kidogo kwenye hizi ajira.
Kwanza kabisa niunge mkono hoja ya mwanzilishi wa huu uzi kwa kuchangia kama ifuatavyo
Hizi ajira zimetoka kwa namna ambayo kiasi kwamba ukiamua ufuatilie kiundani utapata maswali mengi kuliko majibu. Tumeona kuna watu mbali mbali wameajiriwa mara mbili tena katika vituo viwili tofauti na wengine wameajiriwa nje ya vigezo vilivyokuwa vimewekwa kwenye tangazo la ajira.
Ninachojiuliza je hawa wanaopangiwa vituo mara mbili ni hewa nyongine inaingia serikalini??
Je ni wale ambao wameajiriwa kwa michongo ndo maana imepelekea majina yao kuajirika mara mbili??
Ni kwanini katika awamu hii kipengele cha vyuo walivyosoma hakijawekwa tukajua na miaka yao ya kumaliza?? Kwanini wafiche wakati mara kadhaa wamekuwa wakikiweka hiki kipengele??
Hii yote inadhihirisha ni kwa namna gani kuna madudu kwenye hizi ajira ambayo yamefanyika.
Hapa pichani ni mmoja kati ya waliopangiwa vituo mara mbili ambapo kituo cha kwanza kapangiwa iringa kingine kigoma. Kilichofanyika wameacha majina yale yale, center number yake ya shule (O level) ile ile isipokuwa wamebadili mwaka wake wa kuhitimu masomo ambapo mwanzoni inaonyesha kamaliza kidato cha nne 2012 na kamaliza kidato tena cha nne mwaka 2013 NOTE:majina ni yale yale. Nimewawekea picha hapa ili muweze kuitazama
Naomba mrejee kwenye jina namba 3244 na 3245 kwenye ajira za waliopangiwa kwenda sekondari. Naomba pia mrejee katika jina namba 3251 alafu mje tujuzane hapa maana mhusika tajwa kwenye hiyo namba amemaliza kidato cha nne 1994 je kwa sasa atakuwa na umri gani na ataitumikia serikali kwa miaka mingapi(ikumbukwe watu wa zamani walikuwa wanasoma wakiwa wakubwa kidogo)