Serikali yaajiri walimu 3,081 kupunguza uhaba wa walimu wa sayansi, sanaa ina ziada ya walimu 7,463

Msafiri Kasian

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,133
661
JAMHURI YAMUUGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZAMITAA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU AJIRA MPYA ZA WALIMU WA MASOMO YA HISABATI NA SAYANSI KWA MWAKA 2016/2017

Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imetangaza ajira mpya kwa Walimu wa masomo ya Hisabati na Sayansi leo tarehe 12 Aprili, 2017. Majina ya Walimu yaliyotangazwa yanatokana na tangazo la nafasi ya kazi ya Ualimu lililotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mnamo tarehe 01 Desemba, 2016.

Jumla ya Walimu wapya wapatao 3,081 wakiwemo 1,544 ni wa ngazi ya Shahada na Walimu 1,537 ni wa Stashahada. Walimu hao watatakiwa kuripoti kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri na baadaye kwenye Shule walizopangiwa kuanzia tarehe 18 Aprili, 2017 hadi tarehe 25 Aprili, 2017. Walimu wote waripoti wakiwa na vyeti halisi vya taaluma vya kidato cha nne (IV) na kidato cha sita (VI), vyeti halisi vya kitaalaam vya kuhitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada na Shahada na Cheti cha kuzaliwa. Angalizo :
  1. Walimu waliopangiwa vituo ni wa masomo ya Hisabati na Sayansi waliohitimu hadi mwaka 2014/2015.
  2. Kituo cha kazi cha mwalimu ni shule aliyopangiwa na sio makao makuu ya Halmashauri.
  3. Mwalimu atakayeripoti na kuchukua posho ya kujikimu na baadae kuondoka atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
  4. Walimu wote watakiwa kuripoti katika vituo vyao kuanzia tarehe 18 Aprili, 2017 hadi 25 Aprili, 2017, watakaochelewa nafasi zao zitajazwa na mwalimu mwingine.
  5. Hakutakuwa na uhamisho ndani ya Mkoa au Halmashauri. Majina ya Walimu hao yanapatikana katika tovuti ya Ofisi ya RaisTAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz

Imetolewa na: Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI
 

Attachments

  • PRESS-RELEASE-AJIRA-WALIMU-WA-HISABATI-NA-SAYANSI-2017.pdf
    210.3 KB · Views: 304
  • Orodha-ya-Walimu-wa-Shahada-wa-Ajira-Mpya-kwa-Masomo-ya-Sayansi-na-Hisabati.pdf
    1.7 MB · Views: 316
JAMHURI YAMUUGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZAMITAA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU AJIRA MPYA ZA WALIMU WA MASOMO YA HISABATI NA SAYANSI KWA MWAKA 2016/2017 Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imetangaza ajira mpya kwa Walimu wa masomo ya Hisabati na Sayansi leo tarehe 12 Aprili, 2017. Majina ya Walimu yaliyotangazwa yanatokana na tangazo la nafasi ya kazi ya Ualimu lililotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mnamo tarehe 01 Desemba, 2016. Jumla ya Walimu wapya wapatao 3,081 wakiwemo 1,544 ni wa ngazi ya Shahada na Walimu 1,537 ni wa Stashahada. Walimu hao watatakiwa kuripoti kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri na baadaye kwenye Shule walizopangiwa kuanzia tarehe 18 Aprili, 2017 hadi tarehe 25 Aprili, 2017. Walimu wote waripoti wakiwa na vyeti halisi vya taaluma vya kidato cha nne (IV) na kidato cha sita (VI), vyeti halisi vya kitaalaam vya kuhitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada na Shahada na Cheti cha kuzaliwa. Angalizo : i. Walimu waliopangiwa vituo ni wa masomo ya Hisabati na Sayansi waliohitimu hadi mwaka 2014/2015. 2 ii. Kituo cha kazi cha mwalimu ni shule aliyopangiwa na sio makao makuu ya Halmashauri. iii. Mwalimu atakayeripoti na kuchukua posho ya kujikimu na baadae kuondoka atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. iv. Walimu wote watakiwa kuripoti katika vituo vyao kuanzia tarehe 18 Aprili, 2017 hadi 25 Aprili, 2017, watakaochelewa nafasi zao zitajazwa na mwalimu mwingine. v. Hakutakuwa na uhamisho ndani ya Mkoa au Halmashauri. Majina ya Walimu hao yanapatikana katika tovuti ya Ofisi ya RaisTAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz Imetolewa na: Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI
Stashahada hawajaweka?
 
Serikali imesema jumla ya walimu 3,081 wakiwemo walimu 7 wa shule ya Sekondari Omumwani Kagera, wameajiriwa, hivyo bado kuna nafasi ya walimu 1.048 kati ya nafasi 4,129 za walimu wa Sayansi na Hisabati zilizotolewa kibali cha ajira.


Taarifa hiyo imetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene alipokuwa akizungumza na Waandishi Habari,ofsini kwake ambapo amewataka walimu wote walioajiriwa wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi kuanzia tarehe 18 hadi 25 mwezi huu.


Amesema walimu walioajiriwa wamepangwa moja kwa moja na TAMISEMI katika halmashauri zote nchini ambazo zina upugufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati.


Simbachawene amesema kati ya walimu hao walioajairiwa walimu 1,537 ni wa Shahada na walimu 1,544 ni wa Stashahada.


“Sehemu kubwa ya walimu wa Shahada wamepangwa kwenye shule za kidato cha tano na sita na wachache kwenye shule za kidato cha kwanza hadi cha nne’’ alisema.


Simbachawene amekiri kuwa kuna upungufu wa walimu 26,026 wa masomo Sayansi na Hisabati katika shule mbalimbali za sekondari nchini.


“Moja ya changamoto kubwa ambazo zinaikabili sekta ndogo ya elimu ya sekondari ni upungufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati upungufu uliopo katika shule 3,602 ni 26,026 sawa na asilimia 60.14 ya walimu 43,248 wanaohitajika” amesema Simbachawene


Amesema walimu wanaohitajika kwa masomo hayo ni walimu 43,248 lakini waliopo kwa sasa ni 17,252 pekee.


Amesema kwa sasa serikali ina shule za sekondari 3,602 na kati ya hizo shule 333 ni za kidato cha tano na sita huku zingine 54 za kidato cha tano zimeanzishwa .


Aidha amesema shule hizo za sekondari kwa upande wa masomo ya Sanaa ina ziada ya walimu 7,463 ambapo waliopo ni walimu 63,240 na wanaohitajika ni walimu 55,777.


“Kutokana na ziada hiyo ya walimu wa Sanaa serikali imeanza kuchukua hatua yawahamisha walimu hao katika shule za msingi ili kuziba upungufu wa walimu katika shule hizo’’ alisema.
 
Ajira za walimu wa Science kwa walio hitimu vyuoni mwaka 2015
List hii Hapa
 

Attachments

  • Orodha-ya-Walimu-wa-Shahada-wa-Ajira-Mpya-kwa-Masomo-ya-Sayansi-na-Hisabati.pdf
    1.7 MB · Views: 146
Back
Top Bottom