Halmashauri zenye uhaba wa Walimu kupewa kipaumbele kwenye ajira mpya

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,323
1,113
Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI (Elimu), Mhe. Zainabu Katimba (Mb) amesema katika Ajira mpya za Kada ya Ualimu zitakazotolewa hivi karibuni mgawanyo wa walimu hao utazingatia Halmashauri zenye uhaba wa walimu.

Mhe. Katimba ameyasema hayo katika mkutano wa 15 kikao cha 52 cha Bunge la Bajeti linaloendelea jijini Dodoa leo tarehe 24.06.2024w

Amesema kwa mwaka 2024/25 Serikali inatarajia kuajiri walimu elf kumi na mbili wa shule za msingi na sekondari ambao wanatapangiwa vituo vya kazi hususani kwenye Halmashauri zenye upungufu wa walimu.

Akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini, Mhe. Mhe. Emmanuel Adamson Mwakasaka, Mhe. Katimba amesema manispaa ya tabora inaupungufu wa walimu kwa shule za msingi na sekondari na katika awamu inayokuja, Manispaa ya Tabora itapata mgao huo wa walimu watakao ajiriwa. Pia mgao huo utajali uwiano kwa kila mkoa, halmashauru na mahitaji ya nchi nzima itapata mgao huo wa walimu wapya watakao ajiriwa.

Aidha, Mhe. Katimba amesisitiza halmashauri kufanya msawazo wa walimu kwa kupunguza walimu mjini na kuwapeleka vijijini ili kupunguza ukali wa upungufu wa walimu katika maeneo ya vijiji huku serikali ikiendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa kujenga nyumba na kuendelea kuboresha mazingira ya walimu.

Katimba amesema Katika mgao wa walimu watakao ajiriwa watazingatia halmashauri ambazo zina uhitaji wa walimu pia amesema wamepokea maoni na ushauri kwa kuwazingatia swala la walimu wanao jitolea ili waweze kupata ajira.

‘Ombi hilo limepokelewa na kwa kushirikiqna na Ofisi ya Rais - Utumishi tunaangalia namna nzuri ya utekeezaji wa swala hilo.

IMG-20230530-WA0033.jpg
GQ18NAgWoAAdMe9.jpg
 
Back
Top Bottom