PreGE2025 Serikali yaahidi kufikisha huduma ya maji kwenye makazi ya watu, Msomera

PreGE2025 Serikali yaahidi kufikisha huduma ya maji kwenye makazi ya watu, Msomera

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Nipe Maji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
335
Reaction score
190
Serikali imejipanga kuhakikisha huduma ya maji inaimarishwa kwa wananchi walioamua kuhamia eneo la Msomera, Handeni.

Naibu Katibu Mkuu Bi. Agness Meena akiongea kwa Niaba ya Waziri wa Maji kuhusu huduma ya maji amesema kazi kubwa inafanyika kuhakikisha miundombinu ya maji inafika katika maeneo yote ya makazi pamoja na kujenga mabirika ya mifugo.

Amesema kazi ya ujenzi inafanyika kwa awamu na hivi sasa ni awamu ya nne, ambapo bwawa la maji la Msomera pamoja na kutoa huduma lipo katika hatua za mwisho za utekelezwaji pamoja na matanki ya ukubwa mbalimbali ya kuhifadhi maji.

Msimamizi wa mradi wa RUWASA Mhandisi Nobert Temba ameainisha usanifu wa kazi hiyo ni uwezo wa kuhudumia bila tatizo kwa miaka 20

Bi. Meena katika ukaguzi wa kazi hiyo ameongozana menejimenti ya Wizara ya Maji, RUWASA na uongozi wa wananchi wa Msomera.
IMG-20250531-WA0043-1024x682.jpg
IMG-20250531-WA0046-1024x682.jpg
IMG-20250531-WA0051-1024x682.jpg
IMG-20250531-WA0049-1024x682.jpg
 
Back
Top Bottom