Serikali yaahidi kuendelea kutoa kipaumbele kwa makandarasi wazawa

Serikali yaahidi kuendelea kutoa kipaumbele kwa makandarasi wazawa

Nipe Maji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
335
Reaction score
190
Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega amesisitiza kuwa ni dhamira ya serikali ya awamu ya sita katika kuwawezesha, kuwazingatia na kutoa kipaumbele kwa makandarasi wazawa kama ambavyo wabunge wameshauri wakati wa mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara yake ya Ujenzi kwa mwaka 2025/2026.

Wakati akihitimisha mjadala huo Mei 06, 2025, Bungeni Mjini Dodoma, Waziri Ulega kadhalika ameeleza kuwa sheria na kanuni mbalimbali zimetungwa katika kutoa fursa zaidi kwa wakandarasi hao ikiwemo mfuko wa makandarasi wazawa unaotegemea tozo kutoka Bodi ya Makandarasi, akieleza mpango wa serikali ni kushirikiana na bodi hiyo pamoja na Benki ya CRDB ili kuutunisha mfuko huo utakaotumika kama sehemu ya kulipa malipo ya awali kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya maendeleo nchini Tanzania.

 
Back
Top Bottom