Serikali yaagiza maduka ya dawa yaliyo karibu na hospitali ya rufaa Ligula Mtwara yafungwe

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aagiza maduka yote ya dawa yanayoizunguka Hospitali ya Rufaa Ligula- Mtwara kufungwa kwa kuwa wagonjwa wanaelekezwa kununua dawa huko.

Chanzo: Mwananchi
 
Wafungue duka la dwa la MSD dawa ziuzwe bei nafuu, hilo la mtaani litatoweka lenyewe, waache kutafuta chuki na wafanyabiashara. Halafu akitoka hapo anaenda kwenye mabenki kuhamasisha yakopeshe kwa riba nafuu wafanya biashara wakope, wakati wanaweka mazingira magumu ya biashara.
 
Hii sio haki kabisa ,maamuzi ya kukurupuka haya,basi wawaambie na wauza masanduku ya maiti waondoke karibu na hospital,
muhimu tuhoji hizo dawa mgonjwa anaagizwa kwenda kununua hospital zao zipo au hakuna?
walisema watafungua maduka ya MSD kila mkoa na wilaya imekuwaje?
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aagiza maduka yote ya dawa yanayoizunguka Hospitali ya Rufaa Ligula- Mtwara kufungwa kwa kuwa wagonjwa wanaelekezwa kununua dawa huko
chanzo:mwananchi
Hahahhaha, msimu huu tutashuhudia mengi sana ila mwisho wa siku sifa zikizidishwa zinaharibu kila kitu na watu watasahau yale ya nyuma. Sijaona logic hapo
 
Hapa Muhimbili yapo
UDA hadi leo haifanyi kazi
Umeya Dar hadi leo haluna kitu
 
Biashara ni ushindani,MSD wafungue maduka yao kwenye hospitali zote,wauze dawa kwa bei nafuu maduka ujanja ujanja yatakufa natural death,na sio kuyafunga wakati hatujaandaa mbadala.
 
KWANI HAYO MADUKA YAMO MAWODINI?! AU HUMO HOSPITALINI?! KAMA MTU YUKO KWENYE NYUMBA YAKE KWANINI AINGILIE MATUMIZI YA NYUMBA ZA WATU?! AMESHINDWA KAZI HUYO! BADO ANASUMBULIWA NA KASUMBA ZA UJAMAA HUYO!
 
Back
Top Bottom