Natumai wale watumiaji wanufaika na huduma za maji kutoka Mamlaka za maji wamepata ujumbe unaowataarifu mabadiliko ya tuzo ya huduma hizo
Sina ugomvi na mabadiliko hayo ila najiuliza maswali yafuatayo:
1. Taarifa ya mabadiliko imetolewa jana ikisema tuzo hizo zitaanzia tarehe mosi desemba 2019, kwanini wamezitumia kwenye units zilizosomwa kabla ya tarehe moja desemba? Ki utaratibu si ilitakiwa matumizi ya kuanzia tarehe moja Desemba ndio yahusike na tuzo hizo mpya?
2. Ni sababu zipi/maboresho yapi yamepelekea mabadiliko ya tuzo hizo hasa huku kwetu Morogoro tunapopata huduma ya maji kwa mbinde kwa baadhi ya mitaa?
3. Tumeelezwa mabadiliko hayo ni kwa mujibu wa sheria, hivi hawa watunga sheria hizi ndio sheria za kumsaidia mnyonge?
4. Ni lini serikali hii inayojinadi kuwa serikali ya wanyonge itaacha kuwanyonga hawa wanyonge?
Tumeona NHIF na vifurushi vyao si rafiki kwa wanyonge, sasa Mamlaka za maji nazo tozo zake si rafiki kwa wanyonge! Sasa hawa wanyonge wanaponea wapi?
5. Hivi raia wanaoshangalia pale serikali inaposifiwa kwamba inawajali wanyonge, huwa wanaona nini? Ni wapi serikali imewapa wanyonge kipaumbele?
Ni kwenye afya? Sina hakika! Kwenye Maji? Nisaidieni! Labda kwenye Elimu! Tujiulize, shule zetu zinakidhi vigezo? Watoto wa wakubwa wanasoma na wakwetu madarasa hayo hayo?
Sasa ni wapi wanyonge wanapopewa nafuu! Labda wenzangu mnisaidie!